Je, ipo siku Taifa la Tanganyika litafufuka? Je, itakuwaje? Je, Zanzibar itakuwepo ama?

mkuu ukiongelea habari nzito kama hizi ujue kuna watu flani unawaumiza moyoni vibaya mno hii kitu yaani wanatamani waweke sheria asisikike mtu yoyote akiongelea hii habari ya muungano huu FEKI. na wanahisi kwamba kuna siku hii kitu itakuwa hakuna ubishi itakuja tu.. je wataikubali vipiii,,, ndo wanalotakiwa wawaze vinginevyo waanze mapemaaa kutafuta pa kuelekea kuhifadhiwa
 
... Ni kukosekana kwa viongozi wenye maono ya mbele na mipango, ila wangekuwepo kuna siku Unguja na Pemba zingekuwa Mikoa kama ilivyo Mafia kuwa wilaya ya Pwani. sababu vizazi vya sasa havijui kuilinda historia vinahadahika kiwepesi mno.
 

Makabila hayakuchangia kuiunda Tanganyika, ni wazungu ndiyo walichora mistari kwenye ramani wakaita Tanganyika. Ilikuwa ni nchi bandia tuu. Ndiyo maana husikii mtu anajiita mtanganyika. Unasikia wanajiita watanzania au wasukuma au wahaya lakini hakuna anayejitambulisha kama Mtanganyika. Hakuna hilo taifa.
 
Wazungu walikuja wakakuta mipaka ya makabila, walichofanya ni kuliita eneo walilotawala kwa jina la Tanganyika. Kwa nini wabara hawajiiti watanganyika hivi sasa? ... Sababu ni mchakato wa muungano ulioasisiwa kinyemela na watu wawili kwanza, Karume na Nyerere kisha kutangaza kwa wananchi kuwa sasa tumeungana kuwa nchi moja Tanzania. Kabla ya muungano nimeshuhudia nchi ikiitwa hivyo, radio zikitangaza hivyo, nimeshuhudia bendera ya Tanganyika na wimbo wa Taifa wa Tanganyika. Wananchi wa bara waliukubali huu muungano, ingawa mimi nikiwa mtoto sikulielewa lengo la kuibadilisha Tanganyika kuwa Tanzania. Nina wasiwasi na wazanzibari, kama wote waliukubali huu muungano hivyo ni wazi wale walioporwa mamlaka na umiliki wa visiwa, kwa vyovyote watakuja kudai uhuru wa visiwa vya Zanzibar na Pemba. Swali linakuja, Zanzibar nje ya muungano inarudi kwa mwenye himaya yake ... Oman? Je mapinduzi yaliyofanywa matakatifu yataendelea kuwa hivyo au walioporwa mamlaka watadai chao. Kwangu mimi naitaka Tanganyika irudi na Zanzibar na Pemba pia zirudi kama zilvyokuwa kabla ya muungano ili tuulizane kama huu muungano tunautaka kweli na kama tunautaka basi tuamue kuupanga uwe na manufaa kwa wote na hapa suruhisho ni kuwa na Serikali moja tu.
 
Hakuna kitu chochote wazanzibari wanachopewa bure kutoka bara. Wanalipia kila kitu na vya ziada pia
 

Hayo makabila yaliishi kama nchi moja kabla ya wazungu?
 
Wewe unapoteza nini kwa dola ya Tanzania iliyopo?
 
Hayo makabila yaliishi kama nchi moja kabla ya wazungu?
Hapana, kulikuwa na tawala za kimakabila (Kimila)ambazo msingi wake ulijengwa kutokana na ukoo uliosimikwa toka enzi za mababu na mabibi ndizo zilizotoa viongozi kwa kuzingatia vigezo walivyojiwekea. Viongozi hawa walioulikana kama machifu,watemi, mangi, mwami, wafalme na malkia walitawanyika katika eneo lote la Tanganyika na mifano ipo.
Huko Iringa kwa wahehe, kulikuwa na chifu Mkwawa na ukichimba sana utakuta kuwa wahehe walikuwa na eneo lao la utawala. Wanyamwezi walikuwa na chifu wao wa unyanyembe Milambo, waha walikuwa na mwami wao,akina Mtare, Ruhinda, Ruhaga, Ruyangwa nk. Huko Moshi kulikuwa na Mangi, akina Shangali, .... Tanga akina Kimweri, Kusini kule akina Mputa.
Hawa wote walikuwepo hata kabla ya wakoloni kuingia Afrika na wakati huo utaratibu wa Utaifa na maeneo yake kutengwa kama nchi ulikuwa bado haujaingia.
 

Na ndiyo maana Tanganyika ni nchi bandia. Kabla ya mkoloni kuileta haikuwepo, watu walikuwa wanaishi kikabila kwa mila na desturi zao. Ukisema Tanganyika irudi unazungumzia hiyo Tanganyika aliyoleta mkoloni, hakuna nchi ya Tanganyika kihistoria. Hakuna taifa lilioitwa Tanganyika kihistoria. Taifa ni Zanzibar na ndiyo maana Wanzanzibari wanajitambua kama Wazanzibari hata ukiwakuta popote pale duniani.
 
Najaribu kuelewa mantiki ya hoja yako, sipati picha unalenga nini. Unaposema wazungu ndio walioileta Tanganyika, waliileta kutoka wapi? Hao watu waliokuwa wanaishi kikabila walikuwa wanaishi wapi? Tarehe 9 December ya kila mwaka huwa tunasherehekea uhuru wa nchi gani kama siyo Tanganyika?

Hiyo Zanzibar yenyewe unayoinadi kama taifa ilipata uhuru wake December 10, 1963 ingawa huwa haisherehekewi!. Watu wa Zanzibar ni mkusanyiko wa watu waliotoka bara, na kundi la waarabu kutoka Ghuba ya Oman, wana tofauti gani kama taifa na mchangnyiko wa makabila yaliyoko bara?

Unachonadi ni mwendelezo wa ghiriba na mazingaombwe ya kisiasa kwenye utata unaoghubika muungano, ambapo wanasiasa wachache ndio wanaofaidika na hawako tayari kuona mtego huu ukiteguliwa.
 

Tanganyika ililetwa na Waingereza. Kabla hawajaja hakuna aliyeongelea Tanganyika kama nchi au sehemu. Watu walikuwa wanaishi Busukuma, Uhehe, Buhaya n.k. siyo Tanganyika. Makabila tofauti yaliishi kwa mila na desturi zao, hayakuishi kama taifa moja. Na Tanganyika aliouwa Nyerere ikifufuka itasambaratika tuu.

Wazanzibari wa asili wameshajinganya na kuishi pamoja kama Wazanzibari tangu ya karne ya 1. Ni Wazanzibari kama taifa moja. Na ndiyo maana ukitembea dunia yote ukikutana na Mzanzibari anajijua kama Mzanzibari. Mie katika mazunguko yangu duniani hii sijawahi kukutana na Mtanganyika. Nimekutana na watanzania tele, wachaga, wazaramo, wasukuma n.k. Lakini Mtanganyika bado.

 
Kwa maana hiyo ni heri huu muungano uvunjwe,tena haraka sana ili Zanzibar ibakie kama taifa huru na sisi bara tubaki na Tanganyika yetu tuliyoletewa na wazungu. Tatizo kubwa ni kundi dogo la wanasiasa wanaonufaika na muungano hivi ilivyo sasa.
 
Mnajivunia kujiita watanganyika kwa lipi hasa ambalo hilo jina linamaanisha? Kama sio ukoloni au Kuna lingine la kujivunia kwa hilo jina???

Wazanzibar wanajivunia kuitwa wazanzibar sababu wao bado wanahisi wanavina Saba na watu wa Oman ambao usultan ulitawala

Zanzibar walifanya mapinduzi kutoa uongozi wa usultan ila walikataa kufanya mapinduzi la jina la taifa lao wakabaki na wasalia ya jina la kisultan na hadi leo wanahisi ndugu zao ni waoman waarabu kuliko watu wa bara.

Watanganyika ndio hawa wanaojiita watanzania

Wazanzibar wanaojiita wazanzibar wala hawajiiti watanzania

Tanzania lipo badala la jina la Tanganyika kwa hiyo hakuna Cha Tanganyika hatuwezi kurudia matapishi ya miaka 60 mapitio ya wakoloni
 
Wewe unapoteza nini kwa dola ya Tanzania iliyopo?
Napoteza utanganyika huku uzanzibar ukiwepo. Zanzibar ndo ilifanya neno tanganyika lipotee why yenyewe haipotei ili wote tuwe watanzania tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…