Je, Israel ana combat superiority dhidi ya Iran?

View attachment 2969643
Katika nchi zenye uwezo kijeshi Israeli mtoe, ule uongo mliokua mkidanganya marahii umefika mwisho. Hana uwezo hata wa kupigana na wanamgambo, mwezi wa sita huu anahangaika na Hamas. Kuporomosha majumba na kuuwa wanawake na watoto huo ni wendawazimu sio vita.
We mtoto wa nyoka ukimuona humuui
 
Ndio maana nikamwambia afananishr GROSS NATIONAL INCOME ya Iran na Nigeria.
Pia atizame sehemu zingine za uzalishaji kama sekta ya teknolojia na viwanda kati ya Iran na Nigeria nani amepiga hatua.
Tatizo watu wengi ni kujitia ujuaji hali yakuwa ni weupe kichwani.
 
Iran ana jeshi kubwa sana ,yaani idadi ya wanajeshi, lakini kwa suala la air supremacy Israel wako vizuri kwa sababu alichonacho USA ujue hicho ni cha Israel, hizo ndege za F-35A Israel anazo ambazo Iran hana uwezo wa kuzuia ndege hizo, pale Syria zipo S400 za Russia kwanini ndege za Israel zinaingia na kutoka bila kunasa? Pia hakuna namna ya kuishinda taifa lenye nyuklia, wana slogan yao ya Samson Option ambayo wanasema endapo kuna kitisho cha kufuta taifa la kiyahudi pale middle East Israel iko tayari kufyatua makombora ya nyuklia na kumuangamiza adui kabla hajawaangamizwa. Pia kutokana na kila nchi ya kiarabu na Ulaya kubwa na wayahudi, hao nao wako kazini, unashangaa kuona wanajeshi wa kiyahudi waliko maarifa ya ulaya na America, Africa, Austlaria, nchi za kiarabu ikitokea vita huwa wanaenda kwa ajili ya kupigana upande wa Israel, hawa wana utaalam mbalimbali wa kijeshi tofauti na Iran. Tunakumbuka kile kisa cha mwanajeshi wa Iraq alivyotoroka na ndege ya jeshi la Iraq na kuipeleka Israel , hiyo ndege ilikuwa made on Rusia . Kitu kingine ni vyepesi kupata watu wa Iran ambao wanaweza kusaliti nchi yao kutokana na upinzani uliopo hasa wale wenye ninasaba na utawala wa Shaa iliyopinduliwa miaka ya 1970 kuliko kupata wasaliti ndani ya Israel.
Hiki ndo iran ameamua kukifanya kwa sasa ameamua na yeye kuanza kutengeneza sihlaha zan ykila kwa usalama wake .maana nyukilia inatumika kama immunity
 
Hujui lolote kuhusu uchumi huko tusiende.
Wana vikwazo zaidi ya miaka 40 lakini wamekomaa na wapo mbali, sasa huyo Israel mtembeza bakuli, kupambana tu na Hamas ameomba pesa asaidiwe hadi bunge la US likakaa juzi hapa kupiga kura.
niliuliza swali, kabla ya hiyo miaka 40 ya kuwekewa vikwazo walikua wana uchumi gani?
 
hakuna vita ambayo israel amewahi kukimbia sabab vita ndio maisha ya israel, yeye bora afie vitani lakini sio kukimbia, atleast US anaweza kukimbia vita kama akiona haina maslahi yake na anatumia gharama kubwa, ila sio israel, bila vita israel hawezi kusurvive, unalijua hilo?
Ashukuru anasehem za kuchotewa silaha na kumwagiwa dollar za bure .huo mrija kuna siku utaka tu dunia ya leo sio ya kesho
 
niliuliza swali, kabla ya hiyo miaka 40 ya kuwekewa vikwazo walikua wana uchumi gani?
Hivi ww jamaa una elimu gani maana unauliza maswali yasiyo kuwa na msingi.
Kwani China au Indonesia walikuwa na Uchumi gani mwaka 1980 na sasa hivi wana uchumi gani?

Hivi hujui kuwa mifumo ya uchumi ilikuwa inabadilika kutokana zama mbali mbali.
 
Iran ana jeshi kubwa sana ,yaani idadi ya wanajeshi, lakini kwa suala la air supremacy Israel wako vizuri kwa sababu alichonacho USA ujue hicho ni cha Israel, hizo ndege za F-35A Israel anazo ambazo Iran hana uwezo wa kuzuia ndege hizo, pale Syria zipo S400 za Russia kwanini ndege za Israel zinaingia na kutoka bila kunasa? Pia hakuna namna ya kuishinda taifa lenye nyuklia, wana slogan yao ya Samson Option ambayo wanasema endapo kuna kitisho cha kufuta taifa la kiyahudi pale middle East Israel iko tayari kufyatua makombora ya nyuklia na kumuangamiza adui kabla hajawaangamizwa. Pia kutokana na kila nchi ya kiarabu na Ulaya kubwa na wayahudi, hao nao wako kazini, unashangaa kuona wanajeshi wa kiyahudi waliko maarifa ya ulaya na America, Africa, Austlaria, nchi za kiarabu ikitokea vita huwa wanaenda kwa ajili ya kupigana upande wa Israel, hawa wana utaalam mbalimbali wa kijeshi tofauti na Iran. Tunakumbuka kile kisa cha mwanajeshi wa Iraq alivyotoroka na ndege ya jeshi la Iraq na kuipeleka Israel , hiyo ndege ilikuwa made on Rusia . Kitu kingine ni vyepesi kupata watu wa Iran ambao wanaweza kusaliti nchi yao kutokana na upinzani uliopo hasa wale wenye ninasaba na utawala wa Shaa iliyopinduliwa miaka ya 1970 kuliko kupata wasaliti ndani ya Israel.
S 400 hapo Syria haipo activated kutungua ndege za Israel ila kulinda Kambi za Russia na hizo ndege za Israel hazifiki maeneo hayo kama zinaweza zikaangushe bomu kwenye maeneo alipo mrusi, ndio maana mrusi yupo hapo Syria ila Israel hajawahi kuua mrusi hata mmoja
 
Hivi ww jamaa una elimu gani maana unauliza maswali yasiyo kuwa na msingi.
Kwani China au Indonesia walikuwa na Uchumi gani mwaka 1980 na sasa hivi wana uchumi gani?

Hivi hujui kuwa mifumo ya uchumi ilikuwa inabadilika kutokana zama mbali mbali.
sasa kama ni hivo point ya kusema iran ipo tangu miaka 2500 nyuma, mara sijui ilitawala dunia inatoka wapi? au umuhimu wa point hiyo hasa?
 
Bro unaonekana umeanza kufuatilia mzozo wa Iran na Israel juzi.
Israel imeshalipua sanaaaaa vinu vya nuclear vya Iran na kuvihujumu sana tu,kama ingefanikiwa mara hii basi ingekua ni mara zaidi hata ya tano au sita.
Ushahidi upo wa Israel kuhujumu vinu vya nuclear vya Iran.
Na nuclear facility za awamu hii ndio zimejengwa kiutofauti na za awamu za kwanza,kama Iran angejenga nuclear facility kwa mtindo ule wa zamani kama alivyokua anajenga basi ungesikia kimelipuliwa tena.
Kitu pekee Israel anachohofia kwa Iran ni uwezo wa Iran kuunda silaha za nuclear.
Kaa fuatilia hilo.
Kililengwa kinu cha nuclear.
Wew kichwani. Ni mtupuu sana uikisiokia cyber attack sio sawa. Na kushamvbulia physical. Hicho ulichhokiasema hakijawahi kutokea na hakitaakaa kitookee.
 
sasa kama ni hivo point ya kusema iran ipo tangu miaka 2500 nyuma, mara sijui ilitawala dunia inatoka wapi? au umuhimu wa point hiyo hasa?
Mkuu ndio maana nimekuambia mifumo ya kiuchumi ilikuwa inabadilika kutokana na zama.

Na ndio maana kila zama ina taifa lake ambalo lilikuwa na nguvu kijeshi na kiuchumi.
Zama hizi za karne ya 20 na 21 mfumo wa kiuchumi umetawaliwa nchi za Magharibi japo kwa sasa utawala huo unaanza kuanguka polepole.

Mpaka mwaka 1979 Iran alikuwa na GDP 79$ bilion kwa kipindi hicho kilikuwa ni kiwango kizuri tu.
 
Naomba ukweli tu ndio usemwe nani mwenye uwezo wa kimedani Kati ya mahasimu hawa wawili kati ya muyahudi na waajemi. Kuna watu wanapenda mambo ya medani japo vita ni kuzimu(hell) ila ni hulka ya binadamu kujipa uhalali kiuwezo na kiplopaganda. Israel alianza kutoa mapigo kisha akajibiwa je, nani mwenye military edge kumuwin mwenzake? Religion sympathy sio mahala pake hapa I want only facts to spoken.
Kabla ya fact. Tumia kwanza logic hii. Iran aliwahi kupigana vita gani? Israel maonesho yake ya silaha yana fanyika kwenye action halisi vitani. Irani silaha zake hua anazisifia mwenyewe. Ukiacha shaheed ambazo nyingine ziliruka zika nasa kwenye nguzo za umeme sijaona silaha yoyote ya iran kwenye action ikawa tishio vitani kiasi cha kuzishindanisha na silaha zingine
Pili. Hata makombora ya irani irani atatakiwa kurusha makombora 200 na shahid 700 ili kupata target moja israel atatumia ndege moja kupata target mia.
Nawasilisha
 
Israel is ahead of Iran kwenye izo anga. Juzi amezuiwa tu na Marekani kwasababu marekani aliogopa iran itafunga mlango wake wa bahari na uchumi ungeenda kuwa shida. walichofanya ni kupiga rada za kinu chao cha Nukes pekee ili asiweze kabisa kuwarushia makombora ya nuclear. Ndege zilizoenda kupiga huko unaambiwa hazikuonekana hata iran ilikiri kwamba hawajajua ni nani kapiga hadi sasaivi, manake radar za iran hazikuiona. kama ukiwa na uwezo huo manake unaweza kuamua kupiga mtu bila yeye kukujua.

Pia, marekani ana uwezo mkubwa sana kiteknolojia kumzidi hata urusi. kama unakumbuka siku mrusi anaenda kupiga ukraine, marekani alishatangaza kuwa siku fulani ndio imepangwa kwenda kupiga, na siku iran anapiga marekani ilishatangaza kua siku fulani iran atapiga. tuseme urusi aliitaarifu marekani siku anayoanza vita ukraine? tuseme iran aliitaarifu marekani? ni wanakusoma hapohapo ulipo

kuna siri kubwa sana, aidha kuogopa vita vya baridi kuanza upya kwa urusi na china kuungana na iran ili kuishambulia marekani, au kuna kitu cha siri, kwasababu kwa tulivyozoea na tunavyoijua marekani, haiwezi kushambuliwa na nchi kama iran ikanyamaza kimya, lazima kuna mchezo waliusoma wa urusi na china. Unakumbuka Iran aliishambulia marekani kwenye kambi zake za iran siku ile alipoua kamanda wao suleiman? hivyo hata juzi wamemzuia Israel asifanye kitu kitakachoamsha vita mpya ambayo nadhani kwa ustawi wa dunia marekani hataki kabisa ije kwasababu ameshawasoma hao wenzake china na urusi wanachomuwazia.

Na iran naye nadhani ana busara, kambi zake iraq na syria zimechakazwa, na radar yake ya nukes imechakazwa, akaona hapa naweza kula hasara akasema mapema kabisa kwamba hata kama tumepigwa hatutarudisha kisasi. tuseme Iran ameogopa nini? ati Iran aseme hata kama Israel amerusha chochote sisi hatutarudisha kisasi? tuseme walikubaliana na marekani israel naye arushe kitu ili ionekane israel hajashindwa? na iran akakubali? tangu lini marekani na iran ni marafiki? since revolution iran na marekani hawapendani, nini kiliwafanya wanyamaze juzi, walipigwa mkwara gani hadi wakaamua kuufyata? waliambiwa ukirudishia tutaingia na tutakufumua. possibly.

all in all, Marekani inasemekana ni taifa la kifreemason, kuna wakati naamini kwasababu ushoga na dhambi za ajabuajabu zimezidi mno marekani, shetan asingewaacha lazima angekaa kwenye kiti cha ili arun dunia.
Ukisikia mahaba Niue ndo haya bilashaka ww ni mlokole
 
niliuliza swali, kabla ya hiyo miaka 40 ya kuwekewa vikwazo walikua wana uchumi gani
Israel hata kupambana na Tanzania haiwezi ukitoa msaada wa silaha, fedha na mbinu.
Kama wanapelekeshwa na kikundi kidogo cha migambo wataweza kupambana hata na Burundi kweli.
 
Wew kichwani. Ni mtupuu sana uikisiokia cyber attack sio sawa. Na kushamvbulia physical. Hicho ulichhokiasema hakijawahi kutokea na hakitaakaa kitookee.
Doh!
Mbona umekuja kwa kukurupuka?
Embu kafuatilie nilichokiandika ndio uje hapa tuzungumze.
Usije na mipasho njoo na ushahidi ili tujadiliane nahitaji mjadala sio mipasho mkuu.
 
Kabla ya fact. Tumia kwanza logic hii. Iran aliwahi kupigana vita gani? Israel maonesho yake ya silaha yana fanyika kwenye action halisi vitani. Irani silaha zake hua anazisifia mwenyewe. Ukiacha shaheed ambazo nyingine ziliruka zika nasa kwenye nguzo za umeme sijaona silaha yoyote ya iran kwenye action ikawa tishio vitani kiasi cha kuzishindanisha na silaha zingine
Pili. Hata makombora ya irani irani atatakiwa kurusha makombora 200 na shahid 700 ili kupata target moja israel atatumia ndege moja kupata target mia.
Nawasilisha

Vita alizopigana Iran.
-Iran-Iraq war 1980-1988.
-Israel-Lebanese war IRGC iliisapoti hizbollah kisilaha 2006.
-Syria kupambana dhidi ya waasi wa Assad ikiwemo ISIS.
-Vita za Yemeni za houthi 2014-2022.

Silaha za Iran zipo sehemu nyingi na zinafanya maafa vizuri.
-Lebanon wanatumia silaha za Iran.
-Yemeni wanatumia silaha za Iran.
-Syria wanatumia silaha za Iran.
-Russia anatumia makombora na drone za Iran dhidi ya Ukraine mpaka sasa.

Silaha za Iran ndizo hizo zinazofanya maafa red sea ambazo Houthi Yemen ndio anazitumia.
Na kaa utambue Iran kuishambulia Israel ililenga kutuma ujumbe na ndio maana ilitumia drone za bei rahisi na unguided missiles.
Ila kama Iran ingekusudia kuichakaza Israel ingetumia guided missiles ambazo huwa zinakwepa interceptors kama walizopiga kambi ya US Iraq kulipiza kifo cha Qassem Soleiman.
Guided missiles kumi tu zingetosha.
Kusini mwa Lebanon Hizbollah wamelipua kambi ya Galilee kwa kutumia kombora ambazo ni Iranian made.
 
Na kuna wakristo bongo meno yote nje wakifurahia kuuawa kwa watoto/Raia wasio na hatia
Mzee Israel co wakristo! Nenda wikipidia cheki dini zilizopo Israel
1 Judaism
2 Islamic
Ndoo zinafuata taka nyingine.... Kwa kifupi wale ni ndugu wanapigana. And that is civil war
 
Hujanielewa, kuna wakristo/wayahudi weusi tanzania, wenye chuki na waislamu, wana chuki na waarabu, hivyo wemefurahia sana namna mateso na mauwaji wanayopitia ndugu zetu wapalestina.

Religion in Israel (2016)[1]

JudaismHiloni (33.1%)
Judaism–Masorti (24.3%)
Judaism–Dati (8.8%)
Judaism–Haredi (7.3%)
Islam (18.1%)
Christianity (1.9%)
Druze (1.6%)
Others and unclassified (4.8%)
 
Mzee Israel co wakristo! Nenda wikipidia cheki dini zilizopo Israel
1 Judaism
2 Islamic
Ndoo zinafuata taka nyingine.... Kwa kifupi wale ni ndugu wanapigana. And that is civil war

Hawana undugu wowote, wale ni makafiri na Wapalestina ni waislamu. So hawawezi kuwa ndugu, laanatullah alayhim
 
Israel is ahead of Iran kwenye izo anga. Juzi amezuiwa tu na Marekani kwasababu marekani aliogopa iran itafunga mlango wake wa bahari na uchumi ungeenda kuwa shida. walichofanya ni kupiga rada za kinu chao cha Nukes pekee ili asiweze kabisa kuwarushia makombora ya nuclear. Ndege zilizoenda kupiga huko unaambiwa hazikuonekana hata iran ilikiri kwamba hawajajua ni nani kapiga hadi sasaivi, manake radar za iran hazikuiona. kama ukiwa na uwezo huo manake unaweza kuamua kupiga mtu bila yeye kukujua.

Pia, marekani ana uwezo mkubwa sana kiteknolojia kumzidi hata urusi. kama unakumbuka siku mrusi anaenda kupiga ukraine, marekani alishatangaza kuwa siku fulani ndio imepangwa kwenda kupiga, na siku iran anapiga marekani ilishatangaza kua siku fulani iran atapiga. tuseme urusi aliitaarifu marekani siku anayoanza vita ukraine? tuseme iran aliitaarifu marekani? ni wanakusoma hapohapo ulipo

kuna siri kubwa sana, aidha kuogopa vita vya baridi kuanza upya kwa urusi na china kuungana na iran ili kuishambulia marekani, au kuna kitu cha siri, kwasababu kwa tulivyozoea na tunavyoijua marekani, haiwezi kushambuliwa na nchi kama iran ikanyamaza kimya, lazima kuna mchezo waliusoma wa urusi na china. Unakumbuka Iran aliishambulia marekani kwenye kambi zake za iran siku ile alipoua kamanda wao suleiman? hivyo hata juzi wamemzuia Israel asifanye kitu kitakachoamsha vita mpya ambayo nadhani kwa ustawi wa dunia marekani hataki kabisa ije kwasababu ameshawasoma hao wenzake china na urusi wanachomuwazia.

Na iran naye nadhani ana busara, kambi zake iraq na syria zimechakazwa, na radar yake ya nukes imechakazwa, akaona hapa naweza kula hasara akasema mapema kabisa kwamba hata kama tumepigwa hatutarudisha kisasi. tuseme Iran ameogopa nini? ati Iran aseme hata kama Israel amerusha chochote sisi hatutarudisha kisasi? tuseme walikubaliana na marekani israel naye arushe kitu ili ionekane israel hajashindwa? na iran akakubali? tangu lini marekani na iran ni marafiki? since revolution iran na marekani hawapendani, nini kiliwafanya wanyamaze juzi, walipigwa mkwara gani hadi wakaamua kuufyata? waliambiwa ukirudishia tutaingia na tutakufumua. possibly.

all in all, Marekani inasemekana ni taifa la kifreemason, kuna wakati naamini kwasababu ushoga na dhambi za ajabuajabu zimezidi mno marekani, shetan asingewaacha lazima angekaa kwenye kiti cha ili arun dunia.
Israel walilenga kulipua kinu cha nuclear Isfahan ila walifeli.
Iraq hakuna kambi za Iran bali kuna kambi za wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran,ni sawa ulipue kambi za Hizbollah Lebanon.
Syria kambi zilizopigwa ni za Al Quds fighters wanaosapotiwa na Iran sio za Iran.
Angekua kaguswa Iran pasingekalika kimya.
Shambulio la Israel drone 3 na kombora moja vimedunguliwa utasemaje havikuonekana!?
Walichodai Iran hawakujua wapi shambulio linatoka ila interception wamefanya.
 
Vipi Putin nae kashindwa maana miaka inayeyuka sasa au mnasemaje watumwa?
Unajitoa ufahamu kuwa Ukraine anasaidiwa na NATO kifedha,kisilaha na kijeshi!?
Au ushasahau kuwa Russia anapigana na NATO pale Ukraine!?
 
Back
Top Bottom