Je, Israel ya sasa ni Taifa teule la Mungu au ni propaganda tu za kanisa?

Mkuu huu mstari wa Roman 11: nilioutumia hapo juu umetoa majibu yote,,kwamba ndio wayahudi walimkataa Yesu..Ila kwa ule ufalme kuondoka kwao sio moja kwa moja....hebu upitie tena mwenyewe utaona point yangu.
Ila kwa Sasa unakubaliana umeondolewa kwa mda Hadi pale watakapo tubu na kutambua Yesu kristo waliomkataa ndiye Masihi waliyekuwa wanasubiri? Na ukiona ilo limetokea basi ujue Mwisho wa ulimwengu umefikia.
 
Israel ni taifa lililoko pale mashariki ya kati,,wakristo waliomwamini Yesu wote ni kanisa/mwili wa Kristo na sio waisrael.
Shida yangu sio waitwe waisrael point yangu ni kwamba warithi halali wa hizo ahadi za waisrael ni nani je ni kina netanyahu au wakristo??? Hio Israel ya mashariki ya kati ni ya kimwili tu haina impact yeyote kwa ufalme wa Mungu.

Jikite kwenye hiyo mistari ya petro nilioweka je petro alimaanisha nini kuwaita wakristo taifa teule
 

'Israeli', kama 'taifa teule la Mungu' haina maana ya nchi ya Israeli, bali wale ambao kwa mafundisho ya Yesu na mitume wake wamekuja kuamini na kuishi maneno ya habari njema. Hawa ndio kanisa huwa linasema, familia ya Mungu, taifa la Mungu etc.
 


Kanisa la kristo , Hivi kristo gani mwenye kanisa ??
 
Hivi Taifa teule la Mungu ndo ili la Benjamin Netanyahu au kwakuwa Biblia ina mafumbo mengi labda Taifa Teule la Mungu ni watenda mema wote haijalishi ni Mtanzania, Mpakistan, Mnyarwanda au Mkenya,

Je Taifa teule la Mungu ni lipi? Ndo Israel hii??
 
Hivi Taifa teule la Mungu ndo ili la Benjamin Netanyahu au kwakuwa Biblia ina mafumbo mengi labda Taifa Teule la Mungu ni watenda mema wote haijalishi ni Mtanzania, Mpakistan, Mnyarwanda au Mkenya,

Je Taifa teule la Mungu ni lipi? Ndo Israel hii??
Israel walijiita hivyo kwa vile waliwahi kustaarabika, na kwa uzalendo waliokuwa nayo kwa nchi ya na miji yao eg Jerusalem wakayaita maeneo matakatifu. Lakini ukiniuliza mimi hakuna bustani nzuri ya Eden kama Serengeti & Ngorongoro ambako viumbe wote wa Mungu wanapatikana, na Tanganyika yangu ikiwa ndiyo taifa teule. Sema sisi technology duni, umasikini, uongozi mbovu usiothamini raia wake nk
 
mkuu, talk about land not people...............


ardhi ya lile taifa ndio imebarikiwa na Mungu, so automatically linakua taifa teule/barikiwa la Jehovah Mungu!!!!.......

kuhusu zile kabila 12 za Israel, who knows? wengi hatuna uhakika kama ndio hao kina Netanyahu au wenyewe wapo mahali kwingine...........


ila ukifika wkt wa Bwana, hao watarudi (kama kweli hawapo Israel hivi leo), si unajua MASHAURI YA BWANA mwanadamu hawezi kuyazuia!
 
Hivi Taifa teule la Mungu ndo ili la Benjamin Netanyahu au kwakuwa Biblia ina mafumbo mengi labda Taifa Teule la Mungu ni watenda mema wote haijalishi ni Mtanzania, Mpakistan, Mnyarwanda au Mkenya,

Je Taifa teule la Mungu ni lipi? Ndo Israel hii??
kuna tofauti pia kati ya KANISA, na taifa la Israeli.........


KANISA ni wale wote wamwaminio KRISTO kama BWANA, MASIHI, MKOMBOZI NA MFALME.............


ISRAELI ni ile ardhi ambayo BABA MUNGU alimwapia IBRAHIMU, ISAKA NA YAKOBO kuwapa wazao wao!.............


N.B/ kitabu cha Danieli ndio kimeongelea kwa mapana na marefu destiny ya Israeli
 
Wayahudi walitumia maandiko ya Mwenyezi Mungu vibaya sana kujipa "superiority"...hata hivyo hali ya sasa inawaumbua mbele ya macho ya Watu duniani kote kwani hawana tofauti na Congo (DR), Syria au Afghanistan. Kwanza kisheria na kiutaratibu ni Wadhulumat wa ardhi ya Wapalestina japo wanatumia hayohayo maandiko kujisafishia njia ya kuwanyanyasa Wapalestina. Kwa kiburi walimkataa hata Yesu (Nabii Issa A.S).
 
Hivi ndio ambavyo mimi huwa natambua pia.. Kongole mkuu
 
Taifa la Israel liliundwa na watoto 12 wa Yakobo ambaye baadaye allitwa Israel. Na hao watoto walitengeneza kabila 12 za waisrael. Hii familia katika mazingira Fulani walijikuta wako Misri kama watumwa ,baadaye wakaondolewa kwa nguvu za Mungu akimtumia Musa hadi katika nchi alyowaahidi.Inaamini ndio hao hao akina Natanyahu kwa kuwa kuna baadhi ya tamaduni na mila za waisrael wale wailoelezwa kwenye biblia na akina Natanyahu wanazifuata.Kimsingi Mungu aliyokuwa akiwaeleza Waisrael ilitakiwa wayaeneze kwa mataifa mengine yote ulimwenguni. Hata hivyo baada ya Yesu kuja ,wale wote wanaomwamini nao ni waisrael wa Kiroho.Hata milango ambayo ipo kwenye mji wa mbinguni kuna milango kumi na mbili na kila mlango umeandikwa jina la kabila la Israel.
Ufunuo 21:9-15
Akaja mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na vile vitasa saba vilivyojaa yale mapigo saba ya mwisho, naye akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo.
10 Akanichukua katika Roho mpaka mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu;

11 wenye utukufu wa Mungu, na mwangaza wake ulikuwa mfano wa kito chenye thamani nyingi kama kito cha yaspi, safi kama bilauri;

12 ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu, wenye milango kumi na miwili, na katika ile milango malaika kumi na wawili; na majina yameandikwa ambayo ni majina ya kabila kumi na mbili za Waisraeli.

13 Upande wa mashariki milango mitatu; na upande wa kaskazini milango mitatu; na upande wa kusini milango mitatu; na upande wa magharibi milango mitatu.

14 Na ukuta wa mji ulikuwa na misingi kumi na miwili, na katika ile misingi majina kumi na mawili ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo.

15 Na yeye aliyesema nami alikuwa na mwanzi wa dhahabu, apate kuupima huo mji, na milango yake, na ukuta wake.
 
Waislam wachache wahovyo kweli wakiongozwa na media zinazojiita zina misingi ya kiislam.
.
Nenda kawakomboe sasa hao wapalestina wanaodhurumiwa anzisheni jihad dhidi ya Israel mwasubiri mini miongo yote hiyo?
 
Waislam wachache wahovyo kweli wakiongozwa na media zinazojiita zina misingi ya kiislam.
.
Nenda kawakomboe sasa hao wapalestina wanaodhurumiwa anzisheni jihad dhidi ya Israel mwasubiri mini miongo yote hiyo?
Uislamu umetokea wapi wewe pimbi? Kwanza unajua kuwa wayahudi siyo Wakristu na walishamkataa Yesu? Acheni kudanganyana huko vijiweni mkahisi hao wayahudi ni ndugu zenu...you are a very poor minded creature i ever met here. Soma vitabu vya kihistoria utaujua ukweli.
 
Hakuna taifa ambalo halina ardhi yake, wanatumia maandiko kuunda upya lile taifa lao, baada ya kuzaliwa kwa red haife, muda si mrefu ule msikiti watabomoa ili wajenge hekalu na hivyo kukamilisha unabii wa nabii Ezekiel!
 
Tofautisha kati ya waisrael na wayahudi, uyahudi ni dini ambayo wanavikubali vitabu vya torati ila bado wanamsubiria masihi, waisrael ni taifa kwa ujumla, ndani yake kukiwa na wayahudi, wakristu, waislam, na hata ambao hawana dini. Mada inazungumzia Waisrael na siyo wayahudi.
 
Ahsante mimi pimbi wewe nyumbu.
.
Wayahudi au Judaism sio dini ni dhehebu haiko kama unavyopotoshwa au ulivyopotoshwa na mama yako.
.
Wayahudi wanatumia biblia kuabudu japo wana baadhi ya taratibu ambazo madhehebu mengine hayazifuati, wasabato nao ni wakristo japo nao kuna baadhi ya mambo yanayofanywa na madhehebu mengine hawayafuati, PENTECOSTAL n.k nao wanataratibu zao.
.
Kwa jinsi ulivyo tahira wewe mtoto haujui hata mabohora nao ni waislam Ila wana namna zao za kuabudu.
.
Pumbavu sana ujielewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…