Tukundane
JF-Expert Member
- Apr 17, 2012
- 11,993
- 9,212
Iko hivi,kwanza binadamu mwenyewe ni roho inayoishi ndani ya mwili wa nyama,kwa hiyo binadamu mwenyewe ambaye ni roho huwa hafi,bali roho inatoka kwenye mwili huu wa duniani ambao unaoza na kuvalishwa mwili mpya ambao hauteketei kwa moto na haufi kwa mtu yule ambaye atakwenda motoni.milele kwa maana kwamba mtu anachomwa tu moto anaungu halafu hafi au?
Hivyohivyo na kwa mtu anayekwenda peponi naye anavalishwa mwili mwingine unaofanana na mazingira ya peponi kwa kuwa ni mwili mpya na ambao haujawahi kugusa dhambi.
Kwa ufupi ni kwamba kufa kwa binadamu ndio mwanzo wa maisha mapya ya milele na milele motoni au peponi,na hakuna kufa tena kwa kuwa hakuna kufa mara mbili na miili mipya haifi inafanana na malaika wa mbinguni.