Je, jehanamu ziwa la moto na adhabu za huko ni za milele au sio za milele?

Je, jehanamu ziwa la moto na adhabu za huko ni za milele au sio za milele?

Mambo ya jahanamu ni ya kidini, hivyo mambo ya kidini yatamalizwa kwa kuzingatia maandiko ya vitabu vya kidini ambayo wewe mwenyewe unaifata, kwa mujibu wa maandiko ya kiislamu na maelezo kuhusu maisha ya jahanamu ni kubwa kuna makundi mawili ya wakazi wa jahanamu (majini na wanadamu)
Kundi la kwanza ni wale watakaokaa jahanamu kwa muda (temporary) kulingana na ufanyaji wao wa makosa hapa duniani kisha watatolewa.
Na kundi jingine ni wakazi wa kudumu wa jahanamu (permanent) ambao nao watakaa humo bila kufa wala kutolewa ni mwendo wa kuchemsha kuiva katika mfumo wa recycling.

Kwa maelezo zaidi kuhusu hilo nashauri ungemtafuta kiongozi wa imani yako akukupa maelezo zaidi ya haya.
 
Ni ya milele na milele. Mtu akishindwa kumwamini na kumkiri Yesu Kristo akiwa hai, maana yake hajaamini kuwa Yesu alishuka kumwokoa kwa kufa na kufufuka. Hajaamini wala kuthamini jambo hili muhimu kwa hiyo hawezi kwenda mbinguni. Kinyume ni jehanam ya milele na milele
Asante Sana,

Ila Kuna upande wanasema, watu watakufa huko JEHANAM ,hawata ishi Milele sababu hawana huo UZIMA wa Milele,

Ndio maana nimeomba tuhujadili huo ,UZIMA wa Milele ni Ahadi ya Mungu Kwa wenye dhambi pia ?
 
Wana theolojia, na wengine wote, karibuni kwenye MADA,

Naombeni mnisaidie hili swali,
Ni kama jepesi,Ila ni gumu,ni kutokana na mvutano uliopo,

Kuna wanaosema JEHANAM ya muda sio ya milele na wengine husema ya Milele,
Lipi jibu sahihi,

Je,jehanam ZIWA LA MOTO NA ADHABU ZAKE ni za Milele au za Muda tu sio za Milele,

Naomba Uzi huu ,utumike kumaliza utata huo,

Kwa Kila mtu humu kuchangia na haswa wanatheolojia ,

Naomba muwa-tag watu wote ambao unaona michango yao itakuwa inamanufaa humu,

Nawasilisha,
Karibuni,

Update

ENYI WATU NAOMBENI MCHANGO WA MAWAZO YENU ,

TAZAMA HII,

Mwilini = Start-End format
Rohoni=n.start-n.End format

Mwilini= Time
Rohoni= No Time

Mwilini= Kuna mwanzo na mwisho
Rohoni= Hakuna mwanzo Wala mwisho.

Mwilini = Kuna Muda
Rohoni= hakuna Muda

Hivyo ,jehanamu Haina muda, Haina mwisho ?

Na
Vipi kuhusu mateso ,tunaweza sema hayana muda, no end,

VIPI KUHUSU UZIMA WA MILELE,

HAPO NDIO KIINI CHA MADA ILIPO,

UZIMA WA MILELE JUU
UZIMA WA MILELE CHINI

UZIMA WA MILELE WA NURUNI
UZIMA WA MILELE WA GIZANI

UZIMA WA MILELE WA UHAI
UZIMA WA MILELE WA MAUTI,

UZIMA WA MILELE NA MUNGU
UZIMA WA MILELE NA SHETANI

UZIMA WA MILELE WA UTUKUFU
UZIMA WA MILELE WA DHAMBI

LABDA TUSEME, TUJIKITE KUCHAMBUA HUO UZIMA WA MILELE WA KIROHO ,NA WATU WA CHINI JEHANAM WATAKUWA NA UZIMA USIO NA MWISHO WA MILELE AU WATA KUFA MARA YA PILI KWA KUKOSA UZIMA WA MILELE,

TAGETI NI HUU UZIMA WA MILELE ,

JE, KUTOKUWA NAO HUO UZIMA NI KAMA HUKU DUNIANI MTU ANAKUFA MARA YA KWANZA ,

KULE JE MTU ATAKUFA MARA YA PILI AU KUWA KWENYE LILE ZIWA LA MOTO MILELE NDIO INAYOHESABIWA KUWA MULE ZIWANI NDIO KIFO CHENYEWE LAKINI ROHO YA MTU HAIFI ,

JE ZIWA NDIO MAUTI YA PILI , AU MAUTI HIO YA PILI NI WATU KUFA KABISA ZIWANI PA MOTO ,

KIMWILI MTU ALIEKOSA UZIMA TUNASEMA
ROHO IMETENGANA NA MWILI HIO KATIKA MWILI
NA

VIPI ROHONI TUTASEMA NAFSI IMETENGANA NA ROHO WA UZIMA (MUNGU) HIO NDIO KATIKA ROHO,NA HIO NDIO AWAMU YA PILI,

LAKINI KITU KINGINE TUNAONA KABLA HAWAJATUPWA JEHANAM WALE WATU WALIOPEWA MIILI YA DHAMBI ISIO NA UTUKUFU ILE MIILI YA KIFINYO CHA JEHANAM

NAOMBA Tuhujadili ,huu UZIMA wa Milele ,

UZIMA wa Milele wa Watakatifu juu

UZIMA wa Milele wa wenye Dhambi chini

UZIMA wa Milele ,ndio kiini Cha utata,

Watu Wana uhesabia ule UZIMA wa Milele na Mungu kama ndio UZIMA wa Milele unao kuja kichwani mwao,

Gumzo lipo Kwa wale funza,

Funza Wa JEHANAM wasio kufa Katika Lile Ziwa la moto Wana UZIMA wa Milele na kama Wana UZIMA wa Milele chakula Chao ni kifinyo Kwa watu ,je kama watu watapotea , Hao funza Huo UZIMA wa Milele wamepewa wa Nini Ndio gumzo lilipo,

Wale Funza ni kama wanatupa Siri ya upande wa pili ,kuwa hata chini Ziwa la moto JEHANAM Kuna UZIMA wa Milele sema huo ndio wa wenye Dhambi Ila ule wa juu mbinguni ni UZIMA wa watu wasio na Dhambi,

Funza hafi + moto hauzimiki = vipi wenye Dhambi nao ???

Karibuni ,Tujadili
let us assume kwamba waovu watakaa kwenye huo moto milele ,yaani wapo hai ila siku zote bila kukoma wanaungua
Then turudi kwenye kitabu cha mwanzo wakati wa Uumbaji
Adam na Hawa waliagizwa wasile tunda la mti wa kati na endapo wakila Watakufa
Shetani(nyoka) akawadanganya kwa kuwaambia Hawatakufa
Sasa tukikubali kuwa huo moto watu watangua bila kufa milele/bila kukoma, tutakuwa tunakubaliana na shetani kuwa hata mtu akila tunda hafi. si ndio jamani. maana yake ni kwamba mtu atakuwa kwenye moto akiteseka kwa moto lakini hafi
kwani ni nini maana ya milele?
Yuda1:7 Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele.

Conclusion ni kwamba matokeo ya huo moto yaani huko kuungua ni kwa milele
nitarudi
 
Mambo ya jahanamu ni ya kidini, hivyo mambo ya kidini yatamalizwa kwa kuzingatia maandiko ya vitabu vya kidini ambayo wewe mwenyewe unaifata, kwa mujibu wa maandiko ya kiislamu na maelezo kuhusu maisha ya jahanamu ni kubwa kuna makundi mawili ya wakazi wa jahanamu (majini na wanadamu)
Kundi la kwanza ni wale watakaokaa jahanamu kwa muda (temporary) kulingana na ufanyaji wao wa makosa hapa duniani kisha watatolewa.
Na kundi jingine ni wakazi wa kudumu wa jahanamu (permanent) ambao nao watakaa humo bila kufa wala kutolewa ni mwendo wa kuchemsha kuiva katika mfumo wa recycling.

Kwa maelezo zaidi kuhusu hilo nashauri ungemtafuta kiongozi wa imani yako akukupa maelezo zaidi ya haya.
Adam na Hawa waliagizwa wasile tunda la mti wa kati na endapo wakila Watakufa
Shetani(nyoka) akawadanganya kwa kuwaambia Hawatakufa
Waislam naona mmefuata msimamo wa shetani kwamba waovu hawafi bali wataishi kwenye moto milele
mkuu think twice
 
We umesoma hadi level gani ya elimu nadhani walimu wako walipata tabu sana katika kukufundisha.

Nimeweza Kuwa hilo ni suala la kidini hivyo maelezo yake yatategemea upande upi wa dini unaufuata.
Na ndio maana nikasema kwamba ili kupata maelezo zaidi kuhusu hilo ni lazima tuwaendee wenye ujuzi wa mambo haya kwa kuzingatia imani ya dini yako.

Wewe huwezi kutoa maelezo kuhusu maisha ya jahanamu kwa perspective ya kiislamu.

Samahani acha ujinga....
 
hakuna kitu kipya kwenye uislam, kwani uislam ni sub set ya ukristo. kama huamini basi
na ndio maana Adam na Hawa ni wale wale kwa dini zote mbili
Waislam wanaamini kuwa Yesu ndo mkombozi wa ulimwengu kama wanavyoamini Wakristo
tofauti ni katika maslahi tu ,ambayo yanasababisha tafsiri ziwe tofauti ili kuhalalisha uwepo wa hizo dini
 
Uislamu sio sun set ya ukristo kwa sababu, ukristo ni dini ya watu na uislamu ni dini ya Mungu na ndio maana uislamu unalazimisha kuamini manabii wote hadi yesu wakati ukristo upo tofauti na hivyo.

Tatizo ninyi ndugu zetu ni wavivu wa kusoma vitabu vyenu, take this serious as an assignment (wewe na wenzako) ukisoma biblia maeneo mengi yaliyotajwa na kuhusishwa yesu, wafuasi wake na mitume wenu kama petro, Yohana n.k yapo Uturuki, Misiri, Jodan, palestina, Yemen, na Syria ambapo majority yao ni waislamu mukitaka tuweke na Israel sawa tu yenyewe iko na wayahudi (ndugu wa Yuda eskariot) kwa wingi then wanafuata waislamu, huku kukiwa na chini ya 10% ya wakazi ambao ni wakristo, ninyi ukristo huo mmeutolea wapi ikiwa wanaotakiwa Kuwa wakristo kweli na kindaki Ndaki ni waislamu tena wenye imani thabiti,,,,.....!!!

Kwa mujibu wa mafundisho ya quran na biblia ni Kuwa wachache (ambao ni waislamu) ndio wataifuata njia sahihi na wengi kwa idadi (wakristo na wengineo) wataifuata njia ya upotevu kwa kudhania Kuwa wako sahihi na wengine (wachungaji na viongozi wa kikristo) wakifahamu kuhusu hilo ila watatumika kuwapoteza wengine ili wapate pesa na maisha mazuri ya duniani.

We tafuta kwenye biblia yako kama kuna hata kipande cha aya chenye kuthibitisha usahihi na ukweli wa dini ya kikristo halafu niletee hapa.

Ukweli wa mambo ni kuwa hamna mkristo katika dunia hii ambaye ataweza kuuchallenge uislamu kwa kutumia maandiko ya biblia na vitabu vingine vya kutungwa na binadamu na akafanikiwa. Ila mara nyingi mmekuwa ni watu wa kutumia mihemko na utashi wa nafsi zenu kuusema vibaya uislamu, tena kwa kauli zisizo na mantiki mara ugaidi, mara muunasibishe uislamu na majini na hamna hoja nyingine ukiachilia hizo.

Nilikuwa sipendi kuyasoma haya ila acha niseme You are totally wrong!!!!
 
MAUTI YA KWANZA.
Ni mtu anapokufa, mwili hubaki kaburini, Yeye hupelekwa kutunza Mahali temporary ( KUZIMU) ni Kwa wale watenda dhambi, wasiookoka, ambao Majina Yao hayapo kitabu Cha Uzima, ni wale wasio na ALAMA ya Mungu katika paji za nyuso zao.

MAUTI YA PILI.

Hii ni pale Yesu ataporudi mara ya pili na kuuhukumu Ulimwengu.

(Ufunuo 20:14-15)

MAUTI na kuzimu vitatupwa katika ziwa la Moto( JEHANUM). Hiyo ndiyo MAUTI ya pili, yaani MAUTI na kuzimu kutupwa katika ziwa la Moto Kwa watenda dhambi, wasioandikwa Majina Yao katika kitabu Cha Uzima.

Hadi tunavyoongea nw, Ziwa la Moto halijaumbwa Bado, Hadi muda ufike.

CONCLUSION.

Kuzimu ni temporary, gereza la muda.

JEHANUM ni gereza la milele.

Ubarikiwe.

Pia soma thread: Live Kutoka kuzimu - Rabbon, Kwa uelewa zaidi.
Hapo temporary (kuzimu)ni kwaajili ya wasiookoka!he wale waliookoka temporary yao IPO wapi!?
 
Kama huko motoni hatutakufa bali yatakua mateso ya milele then kifo cha milele hakipo.. labda igekua unachomwa then unakufa!! Au labda pengine Tutakufa ila huo moto utaendelea kuwaka milele

NB:
Dini ni Utapeli
 
MAUTI YA KWANZA.
Ni mtu anapokufa, mwili hubaki kaburini, Yeye hupelekwa kutunza Mahali temporary ( KUZIMU) ni Kwa wale watenda dhambi, wasiookoka, ambao Majina Yao hayapo kitabu Cha Uzima, ni wale wasio na ALAMA ya Mungu katika paji za nyuso zao.

MAUTI YA PILI.

Hii ni pale Yesu ataporudi mara ya pili na kuuhukumu Ulimwengu.

(Ufunuo 20:14-15)

MAUTI na kuzimu vitatupwa katika ziwa la Moto( JEHANUM). Hiyo ndiyo MAUTI ya pili, yaani MAUTI na kuzimu kutupwa katika ziwa la Moto Kwa watenda dhambi, wasioandikwa Majina Yao katika kitabu Cha Uzima.

Hadi tunavyoongea nw, Ziwa la Moto halijaumbwa Bado, Hadi muda ufike.

CONCLUSION.

Kuzimu ni temporary, gereza la muda.

JEHANUM ni gereza la milele.

Ubarikiwe.

Pia soma thread: Live Kutoka kuzimu - Rabbon, Kwa uelewa zaidi.
Kwanini ameifanya kua complex hivi . Kwanini tufe mara mbili .. Hadithi za Uongo
 
let us assume kwamba waovu watakaa kwenye huo moto milele ,yaani wapo hai ila siku zote bila kukoma wanaungua
Then turudi kwenye kitabu cha mwanzo wakati wa Uumbaji
Adam na Hawa waliagizwa wasile tunda la mti wa kati na endapo wakila Watakufa
Shetani(nyoka) akawadanganya kwa kuwaambia Hawatakufa
Sasa tukikubali kuwa huo moto watu watangua bila kufa milele/bila kukoma, tutakuwa tunakubaliana na shetani kuwa hata mtu akila tunda hafi. si ndio jamani. maana yake ni kwamba mtu atakuwa kwenye moto akiteseka kwa moto lakini hafi
kwani ni nini maana ya milele?
Yuda1:7 Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele.

Conclusion ni kwamba matokeo ya huo moto yaani huko kuungua ni kwa milele
nitarudi
Ndio maana ,tumeileta mada ,tuijadili mapema tutoke na jibu Moja,

Maana ni swala linalochanganya, watu,
 
Me naamini mungu yupo ila hakuna ziwa la moto maan mungu ni mwenye huruma hawez kubal ufe kwa maumivu makali
Je, una mwamini yesu,

Maana hata yesu alisema huo moto upo,
Na
Wewe unapinga ,Sisi tunachokijadili ni itakuwa Kwa Muda au ni Milele ,

Maana Dini zote ukristo na uislam zinaamini ipo huo moto wa Ziwa kubwa la moto,
 
Mambo ya jahanamu ni ya kidini, hivyo mambo ya kidini yatamalizwa kwa kuzingatia maandiko ya vitabu vya kidini ambayo wewe mwenyewe unaifata, kwa mujibu wa maandiko ya kiislamu na maelezo kuhusu maisha ya jahanamu ni kubwa kuna makundi mawili ya wakazi wa jahanamu (majini na wanadamu)
Kundi la kwanza ni wale watakaokaa jahanamu kwa muda (temporary) kulingana na ufanyaji wao wa makosa hapa duniani kisha watatolewa.
Na kundi jingine ni wakazi wa kudumu wa jahanamu (permanent) ambao nao watakaa humo bila kufa wala kutolewa ni mwendo wa kuchemsha kuiva katika mfumo wa recycling.

Kwa maelezo zaidi kuhusu hilo nashauri ungemtafuta kiongozi wa imani yako akukupa maelezo zaidi ya haya.
🔥🔥🔥
Fire,
Hiko kitu kiheshimiwe,
 
Ha

Hapa kaka nimekupata vyema hapa umemanisha dhambi za mtu zinatofautina na zitahukumiwa mtu na mtu huwez kuua leo ukafanana na mtu aliyetukan
Ni kweli kabisa,

Mungu ataukumu Kwa haki,

Wenye mafulushi makubwa watapewa adhabu itayo wastaili

Hivyo hivyo Kwa wenye dhambi chache watapewa kinacho lingana na wao
 
inawashwa sigara unaingia motoni ikiisha tu na kubaki kishungi ndipo adhabu yako imeisha👿
 
Back
Top Bottom