Je, jehanamu ziwa la moto na adhabu za huko ni za milele au sio za milele?

Mambo ya jahanamu ni ya kidini, hivyo mambo ya kidini yatamalizwa kwa kuzingatia maandiko ya vitabu vya kidini ambayo wewe mwenyewe unaifata, kwa mujibu wa maandiko ya kiislamu na maelezo kuhusu maisha ya jahanamu ni kubwa kuna makundi mawili ya wakazi wa jahanamu (majini na wanadamu)
Kundi la kwanza ni wale watakaokaa jahanamu kwa muda (temporary) kulingana na ufanyaji wao wa makosa hapa duniani kisha watatolewa.
Na kundi jingine ni wakazi wa kudumu wa jahanamu (permanent) ambao nao watakaa humo bila kufa wala kutolewa ni mwendo wa kuchemsha kuiva katika mfumo wa recycling.

Kwa maelezo zaidi kuhusu hilo nashauri ungemtafuta kiongozi wa imani yako akukupa maelezo zaidi ya haya.
 
Asante Sana,

Ila Kuna upande wanasema, watu watakufa huko JEHANAM ,hawata ishi Milele sababu hawana huo UZIMA wa Milele,

Ndio maana nimeomba tuhujadili huo ,UZIMA wa Milele ni Ahadi ya Mungu Kwa wenye dhambi pia ?
 
let us assume kwamba waovu watakaa kwenye huo moto milele ,yaani wapo hai ila siku zote bila kukoma wanaungua
Then turudi kwenye kitabu cha mwanzo wakati wa Uumbaji
Adam na Hawa waliagizwa wasile tunda la mti wa kati na endapo wakila Watakufa
Shetani(nyoka) akawadanganya kwa kuwaambia Hawatakufa
Sasa tukikubali kuwa huo moto watu watangua bila kufa milele/bila kukoma, tutakuwa tunakubaliana na shetani kuwa hata mtu akila tunda hafi. si ndio jamani. maana yake ni kwamba mtu atakuwa kwenye moto akiteseka kwa moto lakini hafi
kwani ni nini maana ya milele?
Yuda1:7 Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele.

Conclusion ni kwamba matokeo ya huo moto yaani huko kuungua ni kwa milele
nitarudi
 
Adam na Hawa waliagizwa wasile tunda la mti wa kati na endapo wakila Watakufa
Shetani(nyoka) akawadanganya kwa kuwaambia Hawatakufa
Waislam naona mmefuata msimamo wa shetani kwamba waovu hawafi bali wataishi kwenye moto milele
mkuu think twice
 
Adam na Hawa waliagizwa wasile tunda la mti wa kati na endapo wakila Watakufa
Shetani(nyoka) akawadanganya kwa kuwaambia Hawatakufa
Waislam naona mmefuata msimamo wa shetani kwamba waovu hawafi bali wataishi kwenye moto milele
mkuu think twice
We umesoma hadi level gani ya elimu nadhani walimu wako walipata tabu sana katika kukufundisha.

Nimeweza Kuwa hilo ni suala la kidini hivyo maelezo yake yatategemea upande upi wa dini unaufuata.
Na ndio maana nikasema kwamba ili kupata maelezo zaidi kuhusu hilo ni lazima tuwaendee wenye ujuzi wa mambo haya kwa kuzingatia imani ya dini yako.

Wewe huwezi kutoa maelezo kuhusu maisha ya jahanamu kwa perspective ya kiislamu.

Samahani acha ujinga....
 
hakuna kitu kipya kwenye uislam, kwani uislam ni sub set ya ukristo. kama huamini basi
na ndio maana Adam na Hawa ni wale wale kwa dini zote mbili
Waislam wanaamini kuwa Yesu ndo mkombozi wa ulimwengu kama wanavyoamini Wakristo
tofauti ni katika maslahi tu ,ambayo yanasababisha tafsiri ziwe tofauti ili kuhalalisha uwepo wa hizo dini
 
Uislamu sio sun set ya ukristo kwa sababu, ukristo ni dini ya watu na uislamu ni dini ya Mungu na ndio maana uislamu unalazimisha kuamini manabii wote hadi yesu wakati ukristo upo tofauti na hivyo.

Tatizo ninyi ndugu zetu ni wavivu wa kusoma vitabu vyenu, take this serious as an assignment (wewe na wenzako) ukisoma biblia maeneo mengi yaliyotajwa na kuhusishwa yesu, wafuasi wake na mitume wenu kama petro, Yohana n.k yapo Uturuki, Misiri, Jodan, palestina, Yemen, na Syria ambapo majority yao ni waislamu mukitaka tuweke na Israel sawa tu yenyewe iko na wayahudi (ndugu wa Yuda eskariot) kwa wingi then wanafuata waislamu, huku kukiwa na chini ya 10% ya wakazi ambao ni wakristo, ninyi ukristo huo mmeutolea wapi ikiwa wanaotakiwa Kuwa wakristo kweli na kindaki Ndaki ni waislamu tena wenye imani thabiti,,,,.....!!!

Kwa mujibu wa mafundisho ya quran na biblia ni Kuwa wachache (ambao ni waislamu) ndio wataifuata njia sahihi na wengi kwa idadi (wakristo na wengineo) wataifuata njia ya upotevu kwa kudhania Kuwa wako sahihi na wengine (wachungaji na viongozi wa kikristo) wakifahamu kuhusu hilo ila watatumika kuwapoteza wengine ili wapate pesa na maisha mazuri ya duniani.

We tafuta kwenye biblia yako kama kuna hata kipande cha aya chenye kuthibitisha usahihi na ukweli wa dini ya kikristo halafu niletee hapa.

Ukweli wa mambo ni kuwa hamna mkristo katika dunia hii ambaye ataweza kuuchallenge uislamu kwa kutumia maandiko ya biblia na vitabu vingine vya kutungwa na binadamu na akafanikiwa. Ila mara nyingi mmekuwa ni watu wa kutumia mihemko na utashi wa nafsi zenu kuusema vibaya uislamu, tena kwa kauli zisizo na mantiki mara ugaidi, mara muunasibishe uislamu na majini na hamna hoja nyingine ukiachilia hizo.

Nilikuwa sipendi kuyasoma haya ila acha niseme You are totally wrong!!!!
 
Hapo temporary (kuzimu)ni kwaajili ya wasiookoka!he wale waliookoka temporary yao IPO wapi!?
 
Kama huko motoni hatutakufa bali yatakua mateso ya milele then kifo cha milele hakipo.. labda igekua unachomwa then unakufa!! Au labda pengine Tutakufa ila huo moto utaendelea kuwaka milele

NB:
Dini ni Utapeli
 
Kwanini ameifanya kua complex hivi . Kwanini tufe mara mbili .. Hadithi za Uongo
 
Hakuna moto wala nini, ukifa habari yako imeisha
 
Ndio maana ,tumeileta mada ,tuijadili mapema tutoke na jibu Moja,


Maana ni swala linalochanganya, watu,
 
Me naamini mungu yupo ila hakuna ziwa la moto maan mungu ni mwenye huruma hawez kubal ufe kwa maumivu makali
Je, una mwamini yesu,

Maana hata yesu alisema huo moto upo,
Na
Wewe unapinga ,Sisi tunachokijadili ni itakuwa Kwa Muda au ni Milele ,

Maana Dini zote ukristo na uislam zinaamini ipo huo moto wa Ziwa kubwa la moto,
 
🔥🔥🔥
Fire,
Hiko kitu kiheshimiwe,
 
Ha

Hapa kaka nimekupata vyema hapa umemanisha dhambi za mtu zinatofautina na zitahukumiwa mtu na mtu huwez kuua leo ukafanana na mtu aliyetukan
Ni kweli kabisa,

Mungu ataukumu Kwa haki,

Wenye mafulushi makubwa watapewa adhabu itayo wastaili

Hivyo hivyo Kwa wenye dhambi chache watapewa kinacho lingana na wao
 
inawashwa sigara unaingia motoni ikiisha tu na kubaki kishungi ndipo adhabu yako imeisha👿
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…