Ishu sio mchungaji kwa mujibu wa maandiko na elimu ya jumla katika ulimwengu usioonekana.
Hata waliokuwa level ya mwisho ya uchawi wakiwemo wenye phd ya uchawi wanathibitisha hilo.
Hebu tuiache Biblia itueleze:
Yesu akaondoka huko, akaenda kando pande za Tiro na Sidoni. Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo. Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu. Akajibu, akisema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. Naye akaja akamsujudia, akisema, Bwana, unisaidie. akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa. Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani za bwana zao. Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, Mama, imani yako ni kubwa; na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile.
Mathayo 15.21-28
Kwa maneno yasiotatanisha Yesu Kristo anasema kuwa yeye hakutumwa ila kwa "kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli." Hakuwajia Waarabu, wala Wazungu, wala Wahindi, wala Waafrika, wala Machina.
Kama hayo hayakutosha kuonyesha kuwa yeye hakuwajia wasio Mayahudi anazidi kufahamisha kwa mfano wa kumkata mtu kiu: Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa."
Ikiwa ipo shaka yo yote katika akili ya mtu kuwa maana ya maneno hayo ni kuwa Yesu anasema kuwa hakutumwa kwa kabila nyengine zo zote ila Waisiraili tu na atazame mwenye shaka tafsiri kubwa kabisa ya Wakristo inayoeleza maana wazi maneno ya Biblia
, The Interpreter's Bible, sahifa 441 jalada VII ambamo imeandikwa hivi: "Yaonekana wazi kuwa Yesu hakika aliamini kuwa ujumbe wake kwanza na khasa ni kwa watu wake mwenyewe." Ndio maana alisema:
Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua.
Mathayo 7.6
Mbwa na nguruwe ni watu wa mataifa yasiyokuwa wana wa Israili. Ukristo haufai kufundishwa watu wo wote isipokuwa Mayahudi. Hayo ndiyo mawazo ya Yesu, au ya hao walioandika Injili na wakatia maneno hayo kinywani mwa Yesu. Kama asemavyo Isaac Asimov katika kitabu chake Guide to the Bible (Uwongozi kwa Biblia):
"Suala liliopo ni nani hao mbwa na nguruwe wnaokusudiwa katika mstari huu?
Yaweza kuwa maana ya mstari huu ni kuwa haifai kufunza ukweli wa dini kwa wale wasiotubu katika kejeli zao, au wale waliozama katika madhambi, lakini hayo hayaelekei kabisa.
Basi mtu amfundishe nani? Wale waliokwisha amini? Yesu mwenyewe anakanya hayo, kwani aliposhutumiwa kuwa anachanganyika na wenye dhambi ananukuliwa kusema:
Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi.
Mathayo 9.12
"Upande mwengine, huku kutaja mbwa na nguruwe huweza kuwa ni maneno aliyoyachagua Mathayo kulipa nguvu wazo lake kuwa isifanywe juhudi kubwa kueneza mafunzo ya Yesu miongoni mwa Mataifa mengine.
Labda ni nadhari ya Mathayo kuwa ipo khatari kubwa ya hayo Mataifa kuudhika na juhudi za kutaka kuwatanasarisha na kwa hivyo wakawatesa Wakristo; itakuwa ndio 'watageuka na kuwararua'
.Na hayo kwa hakika waliwahi kuyafanya. Yaweza kuwa aliona kuwa yale Mataifa yaliyoukubali Ukristo bila ya kuijua Sharia ya Musa yangeweza kuyavuruga mafunzo ya Yesu: 'na kuyakanyaga chini ya miguu yao.'"
Na juu ya kauli ya Yesu : "Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa," Asimov anasema:
"Hapa Mathayo kwa uwazi anatuletea Yesu ambaye kazi yake ni ndani ya mipaka ya uwananchi wa Kiyahudi tu."