Unazidi kuprove nilichokisema juu yenu wapotoshaji wakubwa,mnatafuta maandiko mnayageuza mnavyotaka.Haya umesema Yesu alikuja kwa ajiliya ya wayahudi tu na hivyo ukristo haufai kufundishwa kwa watu wengine,wewe au huyo mwandishi wako una conclude haya ndiyo mawazo ya Yesu.Mtazamo wako au wa mwandishi unalazimisha yawe yalikuwa mawazo ya Yesu.Kwa hiyo Yesu baadaye alijipinga alivyowaambia wanafunzi wake" enendeni ulimwenguni kote mkaihubiri injili kwa watu wote?Hapo alisema kwa wayahudi peke yake?
Vipi Yohana 3:16?Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanae wa pekee ili kila mtu amwaminie asipotee...(Hapo aliposema Kila mtu amwaminie inamaanisha Wayahudi peke yao?).Kama nilivyokuambia mimi technique zenu nazijua,maandiko haya mnayajua ila mnajua yatawaaibisha lakini mnaendelea kupoteza watu ambao mnajua hawayajui maandiko na hao mmewapata.Mngekuwa mko fair mlitakiwa mjifunze na mngegundua ya kwamba mna mambo mengi ya kujifunza.
Unapojenga hoja katika biblia ni muhimu kuwa na mstari na ikiwezekana mistari mingi kutetea hoja yako.Labda nikusaidie kitu,mpango wa Mungu mwanzoni ilikuwa ni kulifikia taifa la Israel kisha taifa la Israel litumike kueneza habari njema duniani.Lakini walipomkataa Yesu,kazi hiyo walipewa baadhi yao walioamnini na wenhgine ambao hata hawakuwa Wayahudi.
Chakula cha watoto kuwapa mbwa ni msemo wa kutoa kitu cha thamani kwa mtu asiyekitambua thamani yaKe.
Kwa mfano hapa kuna muda natoa chakula cha watoto nawapa mbwa na nguruwe hapa ila hawajui thamani yake ndiyo sababu wanarudi na maswali yasiyo na hoja za msingi na hawako tayari kujifunza bali kufanya ubishi.
Kama unatakakujifunza na kuacha ushabiki tafuta kuna biblia ya King James Version ni ya Kiingereza maneno aliyoyasema Yesu wameyaandika kwa rangi nyekundu kutofautisha na mengine.Hapo utajua kipi kilitoka kinywani mwa Uesu na kipi walielezea wanafunzi wake.
Sielewi shida yenu ni nini wanafunzi wa Yesu wakiandika yale Yesu aliyoyatenda au kusema,naamini wewe unaweza ukawaelezea wazazi wako kwa kuwa umeishi nao inakuwa ngumu kwenu kuamini kile walichoandika wanafunzi wa Yesu kumhusu Yesu na wakati walikuwa naye wakifanya naye huduma huku na kule?
Mko tayari kuamini wanachoandika wapotoshaji ambao hata hawakuwepo na Yesu hicho mnakiamini,hii ni nini?
Hoja zenu hazina support ushahidi mwingine wa Yesu alikuja kwa ajili ya watu wote utaupata kwenye kitabu cha ufunuo?Labda nikupe shule itakusaidia siku moja ukimpokea Yesu,ufunuo unaweza ukawa wa mambo yaliyopita au mambo yajayo.Sasa katika kitabu cha ufunuo wa Yohana(hata hapa huwa mnamaswali yasiyio na msingi) haya niseme ni Ufuno wa Yesu aliompa Yohana ndiyo huwa mnapenda tuseme hivyo.
Ufunuo 21
1.Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu(siyo na Wayahudi peke yao), naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao
Yohana 3:17-19
17.Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe (Siyo Wayahudi imesema ulimwengu)katika yeye.
18 Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu19 Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni(Yesu amekuja ulimwenguni), na watu(siyo Wayahudi imesema watu) wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.
Kwa hiyo ukizingatia hayo maandiko hapo juu Yesu alikuja kwa ajili ya watu wote,shida unachukua mstari mmoja unafanya conclusion bila kuangali amziungira au maneno hayo alikuwa anasema na nani na katika mazingira gani.Hapo tu mnapotea na tukiwaita mrudi hamtaki,taratibu tutaelewana.
Yesu alionya, lakini Paulo hakusikia:
"Katika njia ya Mataifa msiende, wala katika mji wo wote wa Wasamaria msiingie. Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa. Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na wakawararua."
Yaliyosemwa yamekuwa. Kwa kitendo cha Paulo kuwaingiza mapagani wa Kizungu katika dini ya Yesu sharia ya Mwenyezi Mungu ikaambiwa ni laana, ikatolewa ruhusa kula nyamafu, nguruwe na damu, na kila kiuzwacho sokoni bila ya kutia wasiwasi wo wote katika dhamiri.
Tohara aliyoamrishwa Ibrahimu na Mwenyezi Mungu na Manabii wote wakaifuata mpaka mwenyewe Yesu na wanafunzi wake, Paulo aliipuuza kuwaridhi makafiri. Imani za kipagani za mungu mwana na utatu zilizoenea katika mila za Mithra, Osiris, Attis n.k. zikaingizwa katika dini ya Kikristo.
Katika ufalme wa mbinguni Yesu ana yakini kuwa hatokuwa nao ila wana wa Israili tu. Injili ya Mathayo inasema:
Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.
Mathayo 19.28
Hata katika maombi yake inaonyesha kuwa Yesu alikuwa anajua mipaka yake na uwezo wake.
Madai ya kuwa yeye ni mwombezi, mbali kuwa ni mwokozi, wa ulimwengu mzima ni kumsingizia jambo ambalo mwenyewe hakulidhania.
Kumpa mtu cheo asichokuwa nacho ni kumtukana, ni kumvika kilemba cha ukoka, kama Mayahudi walivyotaka kumkejeli kwa kumvika taji la miba.
Cheo alicho nacho kwa hakika si kidogo. Kuwa ni Mtume wa Mwenyezi Mungu miongoni mwa Mitume na Manabii watukufu ni jambo kuu kweli kweli.
Kuwa mtumishi wa Mwenyezi Mungu mwenye kupendeza si utukufu mdogo.
Na Yesu alitafakhari nao, na alitafakhari kuwa yeye hakutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa Ki-Israili.
Na hayo si kwa upungufu wo wote kwa upande wake, ila ni kuutumikia ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa kuulinda usiharibiwe na washirikina mpaka ufike wakati wa kuja huyo atayekuwa kazi yake ni kuitangazia risala ya Mungu kwa ulimwengu mzima.
Katika Injili ya Yohana ananukuliwa Yesu kusema:
Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa.
Yohana 17.9
Ni jambo linalojuulikana katika historia - na hata ukisoma katika Biblia kitabu cha Matendo ya Mitume utaona - ya kuwa Ukristo kwanza haukuhubiriwa kwa mataifa mengine mpaka alipoingia Paulo.
Na yeye alipingwa vikali sana kwa kutoa shauri hiyo na wanafunzi wake Yesu waliomwona na wakawa naye siku zote na wakajifunza vilivyo mafunzo yake na makatazo yake ya kwenda kuwahubiria watu ambao bado ni makafiri.
Ukristo tuuonao na ulioenea ulimwenguni sio Ukristo aliofundisha Yesu. Wa Yesu ulitoweka na mwenyewe na wafuasi wake wa mwanzo wa kabila la Kiyahudi. Paulo kaufuja Ukristo.
Kauli zinazonukuliwa kwa kudai kuwa ni ushahidi kuwa Yesu mwenyewe alitaka mafunzo yake yakafundishwe kwa ulimwengu wote yamo katika Injili ya
Mathayo 28.19-20, Injili ya
Luka 24.46-49 na
Marko 16.15. Mathayo inasema:
Basi, enendeni, mkwafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Mathayo 28.19-20
Luka anatwambia:
(Yesu) akwaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu. Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya. Na tazama, naweletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kueni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.
Luka 24.46-49
Na Injili ya Marko inasema:
(Yesu) akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
Marko 16.15
Je, imekuwaje?
Yesu ni kigeugeu?
Mbona huku anawakataza wanafunzi wake wasende kuwahubiria ila kabila kumi na mbili za Israili, na huku anawaambia nendeni kuwahubiria Injili ulimwengu mzima.
La, Yesu si mbabaishi, wala si kigeugeu.
Hebu natuziangalie vilivyo hizo amri mbili, moja ya kuwa mafunzo yake wasifunzwe ila wana wa Israili tu, na ya pili ni hii ya kuwa watu wote wafunzwe dini.
Vipande vyote vitatu tulivyonukulu mwishoni havitaji mambo ya Yesu alipokuwa na maisha yake ya uhai wa kidunia, lakini vyaeleza mambo yaliyotukia baada ya "kufufuka kutoka wafu" kama inavyosimuliwa na Injili zote tatu.
Yajuulikana kuwa Injili ya mwanzo kuandikwa ni Injili ya Marko. Hizo nyingine ziliandikwa baadae, na labda ujuzi wao ulitegemea hiyo hiyo Injili ya Marko.
Yajuulikana vile vile kuwa maneno yote yaliyohusu kufufuka Yesu kutokana na wafu, pamoja na hayo maamrisho ya kwenda kuihubiri Injili "kwa kila kiumbe", kinyume na maamrisho yake yote ya kuwa asihubiriwe ila Muisraeli tu - maneno hayo yote hayakuwamo katik Marko ya asli, bali yaliongezwa baadae.
Encyclopaedia Brittanica, nakla ya 11, jalada 17, sahifa 730, yasema ya kuwa kipande chote hicho kiliongezwa baadae, yamkini mwanzo mwanzo wa karne ya pili, kuchukua maneno yaliyopotea, au yaliyoonekana kuwa ni mapungufu.