Je, jina la Yesu ni kweli lina nguvu na uwezo mkubwa katika kutenda miujiza hadi leo? Wewe limekutendea makubwa gani? Karibu ushuhudie

Je, jina la Yesu ni kweli lina nguvu na uwezo mkubwa katika kutenda miujiza hadi leo? Wewe limekutendea makubwa gani? Karibu ushuhudie

Nimemtolea mfano, mchungaji Mwamposa, jinsi anavyotumia Shuhuda za uongo kuibia wakristo wenzake.

Wewe umejibu wewe siyo Muumini wake.
Ndiyo nimekuuliza wewe ni muuni wa mtu.
Unachotakiwa kujua hizi ni nyakati za mwisho na Neno la Mungu lazima litimie,itakuwa katika nyakati za mwisho watainuka watumishi.................Jihadharini na mbwa mwitu waliovaa ngozi ya kondoo.......msiziamini kila roho bali zijaribuni kuona kama zinatoka kwa Bwana...Watu wangu wanaangamizwa kwa kusoma maarifa.Acha watapeliwe,Yesu akasema Neno la Mungu na lijae kwa wingi mioyoni mwenu,ukilijua Neno la Mungu huwezi kutapeliwa kirahisi.
 
  • Thanks
Reactions: _ly

Una Quote, ni vizuri kuanza mwanzo, mwanza ujue mpaka naandi hivyo tulianzis wapi.
Maana unadhani umejibu hoja yangu, kumbe jujanijibu bado.
 
Ndivyo älivyokuambia mchungaji wako?

Lugha ya Yohana ni ya namna ya peke yake.

Injili tatu za mwanzo, Mathayo, Marko na Luka zinamweleza Yesu ni binaadamu.

Lakini Yohana amepindukia mipaka hapa kwa kumweleza Yesu kuwa ni "Neno" kwa maana aliyoipata kutokana na waandishi wa Kigiriki, sio kutokana na maandishi ya Kiyahudi.

Kauli hii haikutajwa katika Injili hizo tatu za mwanzo wala katika vitabu vyote vya Agano la Kale.

Katika karne ya sita kabla ya Yesu kulizuka katika maifalasufi wa Kigiriki nadhariya ya kuwa uumbaji wa ulimwengu haukuzuka ovyo lakini kwa mpango wa kiakili, na ulimwengu wote unaendeshwa kwa kufuata sharia maalumu.

Sharia hii au akili hii au mpango huu waliuwita "Logos", maana yake ni "Neno".

Tunaona tamko hilo linatumika katika "Bio-logy" "Geo-logy" "Psycho-logy", kwa maana ya "ilimu".

Katika zile zile zama za Yesu alikuwako mwanachuoni wa Kiyahudi katika mji wa Iskandaria katika Misri ambaye alikuwa ni mwanachuoni katika ilimu za Kiyahudi na vile vile ni mtaalamu katika falsafa za Kigiriki.

Alijaribu kutaka kueleza mafunzo ya Kiyahudi kwa kutumia hoja za falsafa za Kigiriki. Yeye alitumia hii kauli ya Logos au "Neno"

kwa kueleza ile hekima na busara ya Mwenyezi Mungu katika kuumba. Myahudi huyu akiitwa Filo.

Yohana aliitumia lugha ya huyo Filo na kuingiza ndani yake mawazo ya kipagani akachanganya falsafa ya Kigiriki kwa kumuambatishia Yesu, na kumfanya yeye Yesu ndiye "Logos" au "Neno" na hilo "Neno" lilikuwapo tangu mwanzo, na hilo "Neno"lilikuwa pamoja na Mungu, bali ndilo khasa likawa ni Mungu.

Haya yote hayakusemwa kabisa na Injili zote zilizotangulia, wala Yesu mwenyewe hakuyadai, wala wanafunzi wake hawakupata kumdaia. Tena Yohana alizidi kusema:

Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Yohana 3.16

Tunaona kwa mara ya kwanza Yesu kuitwa Mwana wa Mungu wa pekee. Lakini hata kulitumia neno "Mwana wa Mungu" kuna maana gani khasa?

Tukiipitia Biblia na kufungua sahifa zake tutaona kuwa jina hilo limetumiliwa kwa watu wengi licha Yesu.

Katika Agano la Kale ambalo lote limeandikwa hata kabla ya Yesu hajazaliwa tunakuta mifano kama hii:

Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao,wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.
Mwanzo 6.1-2

Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani?
Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni,
Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja,
Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?
Ayubu 38.6-7

Tena itakuwa ya kwamba hesabu ya wana wa Israeli itafanana na mchanga wa bahari, usioweza kupimwa wala kuhesabiwa; tena itakuwa, badala ya kuambiwa, Ninyi si watu wangu, wataambiwa, Ninyi ndio wana wa Mungu aliye hai.
Hosea 1.10

Ni dhaahiri tunaona ilikuwa ni jambo la kawaida hata kwa waandishi wa Kiyahudi wanaoamini Mwenyezi Mungu mmoja kutumia maneno kama "wana wa Mungu" kwa kukusudia "vipenzi vya Mungu", au "waja wa Mungu", yaani watu wema.

Mwanachuoni wa Biblia wa Kitaliana, Marcello Craveri, aliyeandika kitabu chake, Maisha ya Yesu (The Life of Jesus), anaamini kuwa neno hilo "Mwana wa Mungu" limegeuka maana kwa kupitiwa na miaka ya makosa ya kufasiri. Ameandika:

"Kwa hakika, Agano la Kale limetumia neno ebed Yahweh, ambalo maana yake ni 'mtumishi wa Mungu', 'mtumwa wa Mungu', 'khaadimu wa Mungu'. Matini ya Kigiriki ya Septuagint imeipa tafsiri ambayo yaweza kuwa na maana mbili, (Pais Theou), hali ya kuwa pais, kama neno puer laweza kuwa maana ya 'mvulana mdogo' au 'mtumwa'.

Baada yake ilikuwa ni wepesi kuliondoa neno pais lenye maana ya 'mvulana' likatiwa neno (hyos)ambalo maana yake ni 'Mwana'."
Akipotea mmoja ,mnapotezana wote hakuna jipya msome na ndugu yako mwingine huyu mko na desa moja
 
Una Quote, ni vizuri kuanza mwanzo, mwanza ujue mpaka naandi hivyo tulianzis wapi.
Maana unadhani umejibu hoja yangu, kumbe jujanijibu bado.
Kama hoja yako nikiona kuna umuhimu wa kuijibu nitakujibu sijibu kila hoja ndugu yangu,hapo nimekujibu juu ya huyo uliyemtaja au hujaelewa nilichokiandika.Ungekuwa msomaji wa Biblia ungeelewa kwani mengin nimeandika ni kwa mujibu wa biblia.
 
🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Huu upumbavu wa kudhani imani yako ni bora kuliko kuliko ya mwingine, iliniganya ninunue bibilia nisome ili niwe najibu kwa mstari, humu tulikua na akina mgeni na wakristo wengine wenye majina fulani ya kishoga.

Lakini mwisho wa Siku tulikubaliana, Uwe Muislam uwe mkristo maisha ni yale yale Shida raha tunaziishi wote, bila kujali imani yako.

Hivyo kubisha hapa ni upumbavu tu, imani yako kama ndiyo bora kwanini ulalamikie kupanda kwa mafuta, kwanini Mungu wako asikurahishie eneo hilo, ili tabu muachie wasiamini kwenu.

Mtu anafunga Ramadhini yake kwa imani yake, alafu anatokea mjinga mmoja, anakosoa kupitia bibilia, huu si ujinga, yeye hafungi kupitia bibilia yako.

Kitabu chenu nimempa rafiki yangu John Ndongo, Ujinga uishie Mbali, Mungu hawezi kukuacha Salama ikiwa huheshimu wengine, Maana kwa mkosaji nini yeye mwenye uwezo wa kumuonyesha njia sahihi nae ndiye mwenye Kuhukumu.

Ila mkilianzisha sikai kimya.
 
Hili ni swali tu katika kujua uweza na uwezo wa nguvu za Jina la Yesu katika kutenda miujiza.

Yesu alipata kuishi yapata miaka 2019 iliyopita. Je inakuwaje jina lake leo lisemwe kwamba lina nguvu sana katika kutenda miujiza?

Kuna manabii wengi sana na mitume wengi wamepita, kina Krishna, Elisha , Elizabeth Mtishbi nk mbona hatusikii visa vya majina yao katika kutenda miujiza? Sanasana Wlisha ametajwa mara moja kwamba jamaaa walibeba maiti wakienda kuzika, walipofika katika kaburi la Elisha ikatokea vita, katika kujinusuru wakaibwaga maiti chini, maiti ikaangukia kaburi la Elisha, maiti ikafufuka, ikatoka nduki kichizi.

Ndugu mnaoelezea uweza wa jina la Yesu njooni hapa mshuhudie

Yesu ni Mungu

Kama ilivyotabiriwa na manabii. Na jina lake ndilo jina lipitalo majina yote

Isaya 9: 6-7
"Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepata mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.
Maongeo ya enzi yake na amani Hayatakuwa na mwisho kamwe, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa Bwana wa majeshi ndio utakaotenda hayo."

Luka 2: 10 - 11 ~ Aliyezaliwa ni Kristo, Jina Yesu lilishushwa na malaika. Yesu ni Mungu
"Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote; maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana."

Mathayo 1: 20 -21
"Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu"

Yohana 10: 17 - 18
"Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ili niutwae tena. Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. "
 
  • Thanks
Reactions: _ly
Unazidi kuprove nilichokisema juu yenu wapotoshaji wakubwa,mnatafuta maandiko mnayageuza mnavyotaka.Haya umesema Yesu alikuja kwa ajiliya ya wayahudi tu na hivyo ukristo haufai kufundishwa kwa watu wengine,wewe au huyo mwandishi wako una conclude haya ndiyo mawazo ya Yesu.Mtazamo wako au wa mwandishi unalazimisha yawe yalikuwa mawazo ya Yesu.Kwa hiyo Yesu baadaye alijipinga alivyowaambia wanafunzi wake" enendeni ulimwenguni kote mkaihubiri injili kwa watu wote?Hapo alisema kwa wayahudi peke yake?
Vipi Yohana 3:16?Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanae wa pekee ili kila mtu amwaminie asipotee...(Hapo aliposema Kila mtu amwaminie inamaanisha Wayahudi peke yao?).Kama nilivyokuambia mimi technique zenu nazijua,maandiko haya mnayajua ila mnajua yatawaaibisha lakini mnaendelea kupoteza watu ambao mnajua hawayajui maandiko na hao mmewapata.Mngekuwa mko fair mlitakiwa mjifunze na mngegundua ya kwamba mna mambo mengi ya kujifunza.
Unapojenga hoja katika biblia ni muhimu kuwa na mstari na ikiwezekana mistari mingi kutetea hoja yako.Labda nikusaidie kitu,mpango wa Mungu mwanzoni ilikuwa ni kulifikia taifa la Israel kisha taifa la Israel litumike kueneza habari njema duniani.Lakini walipomkataa Yesu,kazi hiyo walipewa baadhi yao walioamnini na wenhgine ambao hata hawakuwa Wayahudi.
Chakula cha watoto kuwapa mbwa ni msemo wa kutoa kitu cha thamani kwa mtu asiyekitambua thamani yaKe.
Kwa mfano hapa kuna muda natoa chakula cha watoto nawapa mbwa na nguruwe hapa ila hawajui thamani yake ndiyo sababu wanarudi na maswali yasiyo na hoja za msingi na hawako tayari kujifunza bali kufanya ubishi.
Kama unatakakujifunza na kuacha ushabiki tafuta kuna biblia ya King James Version ni ya Kiingereza maneno aliyoyasema Yesu wameyaandika kwa rangi nyekundu kutofautisha na mengine.Hapo utajua kipi kilitoka kinywani mwa Uesu na kipi walielezea wanafunzi wake.
Sielewi shida yenu ni nini wanafunzi wa Yesu wakiandika yale Yesu aliyoyatenda au kusema,naamini wewe unaweza ukawaelezea wazazi wako kwa kuwa umeishi nao inakuwa ngumu kwenu kuamini kile walichoandika wanafunzi wa Yesu kumhusu Yesu na wakati walikuwa naye wakifanya naye huduma huku na kule?
Mko tayari kuamini wanachoandika wapotoshaji ambao hata hawakuwepo na Yesu hicho mnakiamini,hii ni nini?
Hoja zenu hazina support ushahidi mwingine wa Yesu alikuja kwa ajili ya watu wote utaupata kwenye kitabu cha ufunuo?Labda nikupe shule itakusaidia siku moja ukimpokea Yesu,ufunuo unaweza ukawa wa mambo yaliyopita au mambo yajayo.Sasa katika kitabu cha ufunuo wa Yohana(hata hapa huwa mnamaswali yasiyio na msingi) haya niseme ni Ufuno wa Yesu aliompa Yohana ndiyo huwa mnapenda tuseme hivyo.

Ufunuo 21​

1.Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu(siyo na Wayahudi peke yao), naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao
Yohana 3:17-19
17.Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe (Siyo Wayahudi imesema ulimwengu)katika yeye.
18 Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu19 Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni(Yesu amekuja ulimwenguni), na watu(siyo Wayahudi imesema watu) wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.
Kwa hiyo ukizingatia hayo maandiko hapo juu Yesu alikuja kwa ajili ya watu wote,shida unachukua mstari mmoja unafanya conclusion bila kuangali amziungira au maneno hayo alikuwa anasema na nani na katika mazingira gani.Hapo tu mnapotea na tukiwaita mrudi hamtaki,taratibu tutaelewana.

Yesu alionya, lakini Paulo hakusikia:

"Katika njia ya Mataifa msiende, wala katika mji wo wote wa Wasamaria msiingie. Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa. Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na wakawararua."

Yaliyosemwa yamekuwa. Kwa kitendo cha Paulo kuwaingiza mapagani wa Kizungu katika dini ya Yesu sharia ya Mwenyezi Mungu ikaambiwa ni laana, ikatolewa ruhusa kula nyamafu, nguruwe na damu, na kila kiuzwacho sokoni bila ya kutia wasiwasi wo wote katika dhamiri.

Tohara aliyoamrishwa Ibrahimu na Mwenyezi Mungu na Manabii wote wakaifuata mpaka mwenyewe Yesu na wanafunzi wake, Paulo aliipuuza kuwaridhi makafiri. Imani za kipagani za mungu mwana na utatu zilizoenea katika mila za Mithra, Osiris, Attis n.k. zikaingizwa katika dini ya Kikristo.

Katika ufalme wa mbinguni Yesu ana yakini kuwa hatokuwa nao ila wana wa Israili tu. Injili ya Mathayo inasema:

Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.
Mathayo 19.28

Hata katika maombi yake inaonyesha kuwa Yesu alikuwa anajua mipaka yake na uwezo wake.

Madai ya kuwa yeye ni mwombezi, mbali kuwa ni mwokozi, wa ulimwengu mzima ni kumsingizia jambo ambalo mwenyewe hakulidhania.

Kumpa mtu cheo asichokuwa nacho ni kumtukana, ni kumvika kilemba cha ukoka, kama Mayahudi walivyotaka kumkejeli kwa kumvika taji la miba.

Cheo alicho nacho kwa hakika si kidogo. Kuwa ni Mtume wa Mwenyezi Mungu miongoni mwa Mitume na Manabii watukufu ni jambo kuu kweli kweli.

Kuwa mtumishi wa Mwenyezi Mungu mwenye kupendeza si utukufu mdogo.

Na Yesu alitafakhari nao, na alitafakhari kuwa yeye hakutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa Ki-Israili.

Na hayo si kwa upungufu wo wote kwa upande wake, ila ni kuutumikia ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa kuulinda usiharibiwe na washirikina mpaka ufike wakati wa kuja huyo atayekuwa kazi yake ni kuitangazia risala ya Mungu kwa ulimwengu mzima.
Katika Injili ya Yohana ananukuliwa Yesu kusema:

Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa.
Yohana 17.9

Ni jambo linalojuulikana katika historia - na hata ukisoma katika Biblia kitabu cha Matendo ya Mitume utaona - ya kuwa Ukristo kwanza haukuhubiriwa kwa mataifa mengine mpaka alipoingia Paulo.

Na yeye alipingwa vikali sana kwa kutoa shauri hiyo na wanafunzi wake Yesu waliomwona na wakawa naye siku zote na wakajifunza vilivyo mafunzo yake na makatazo yake ya kwenda kuwahubiria watu ambao bado ni makafiri.

Ukristo tuuonao na ulioenea ulimwenguni sio Ukristo aliofundisha Yesu. Wa Yesu ulitoweka na mwenyewe na wafuasi wake wa mwanzo wa kabila la Kiyahudi. Paulo kaufuja Ukristo.

Kauli zinazonukuliwa kwa kudai kuwa ni ushahidi kuwa Yesu mwenyewe alitaka mafunzo yake yakafundishwe kwa ulimwengu wote yamo katika Injili ya Mathayo 28.19-20, Injili ya Luka 24.46-49 na Marko 16.15. Mathayo inasema:

Basi, enendeni, mkwafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Mathayo 28.19-20

Luka anatwambia:

(Yesu) akwaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu. Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya. Na tazama, naweletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kueni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.
Luka 24.46-49

Na Injili ya Marko inasema:

(Yesu) akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
Marko 16.15

Je, imekuwaje?

Yesu ni kigeugeu?

Mbona huku anawakataza wanafunzi wake wasende kuwahubiria ila kabila kumi na mbili za Israili, na huku anawaambia nendeni kuwahubiria Injili ulimwengu mzima.

La, Yesu si mbabaishi, wala si kigeugeu.

Hebu natuziangalie vilivyo hizo amri mbili, moja ya kuwa mafunzo yake wasifunzwe ila wana wa Israili tu, na ya pili ni hii ya kuwa watu wote wafunzwe dini.

Vipande vyote vitatu tulivyonukulu mwishoni havitaji mambo ya Yesu alipokuwa na maisha yake ya uhai wa kidunia, lakini vyaeleza mambo yaliyotukia baada ya "kufufuka kutoka wafu" kama inavyosimuliwa na Injili zote tatu.

Yajuulikana kuwa Injili ya mwanzo kuandikwa ni Injili ya Marko. Hizo nyingine ziliandikwa baadae, na labda ujuzi wao ulitegemea hiyo hiyo Injili ya Marko.

Yajuulikana vile vile kuwa maneno yote yaliyohusu kufufuka Yesu kutokana na wafu, pamoja na hayo maamrisho ya kwenda kuihubiri Injili "kwa kila kiumbe", kinyume na maamrisho yake yote ya kuwa asihubiriwe ila Muisraeli tu - maneno hayo yote hayakuwamo katik Marko ya asli, bali yaliongezwa baadae.

Encyclopaedia Brittanica, nakla ya 11, jalada 17, sahifa 730, yasema ya kuwa kipande chote hicho kiliongezwa baadae, yamkini mwanzo mwanzo wa karne ya pili, kuchukua maneno yaliyopotea, au yaliyoonekana kuwa ni mapungufu.
 
Yesu ni Mungu

Kama ilivyotabiriwa na manabii. Na jina lake ndilo jina lipitalo majina yote

Isaya 9: 6-7
"Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepata mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.
Maongeo ya enzi yake na amani Hayatakuwa na mwisho kamwe, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa Bwana wa majeshi ndio utakaotenda hayo."

Luka 2: 10 - 11 ~ Aliyezaliwa ni Kristo, Jina Yesu lilishushwa na malaika. Yesu ni Mungu
"Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote; maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana."

Mathayo 1: 20 -21
"Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu"

Yohana 10: 17 - 18
"Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ili niutwae tena. Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. "

Yesu anasemaje katika Injili yake:

Yohana 17:3 imeandikwa hivi –

uzima wa milele ndiyo huu wakujue Mungu wa pekee na Yesu uliyemtuma.

Katika Aya hii Yesu anasema kwamba ili kupata uzima lazima tumjue kwanza Mungu wa pekee na umjue Yesu Kristo aliyetumwa na Mungu, hapa Yesu hasemi lolote kuhusu yeye kuwa nafasi ya pili ya Mungu ila anakiri wazi yeye ametumwa na Mungu mmoja wa pekee.

Luka 2:40 imeandikwa hivi: -

Yule mtoto akakua akaongezeka nguvu amejaa hekima na neema ya Mungu ilikua juu yake.

Katika Aya hii tunaambiwa kwamba Yesu alijaa hekima na neema ya Mungu.

Tahadhari ufikirie vizuri kwa makini sababu hapa inayonyesha kwamba bila ya Mungu kumpa neema Yesu asingelikuwa na hekima hii inaonyesha wazi Yesu ni kiumbe aliyeteuliwa na Mungu na hii ni kawaida yake Mwenyezi Mungu kwa Mitume na Manabii wake kuwapa neema na hekima.

Yohana 13:13 imeandikwa hivi: -

Nanyi mwaniita Mwalimu na Bwana nanyi mwasema vema maana ndivyo nilivyo. Maneno hayo yatueleza wazi kwamba alikuwa anajua wazi kwamba yeye ni Mwalimu na Bwana ndiyo maana anawasifu wanafunzi wake, NANYI MWASEMA VEMA.

Mathayo 23:9 imeandikwa: -

Wala msimwite mtu Baba maana Baba yenu ni mmoja wa Mbinguni wala msiitwe Kiongozi maana Kiongozi wenu ni mmoja naye ndiye Yesu Kristo. Hapa Yesu anaendelea kutuonyesha jinsi alivyo tofauti na Mungu, na yeye hayuko sawa na Mungu daima Mungu ni Baba lakini Yesu ni Kiongozi tu.

Ufunuo: 1:1-2 imeandikwa hivi: -

Ufunuo wa Yesu Kristo aliopewa na Mungu awaonyeshe watu wake…Naye akatuma Malaika akamuonyeshe Mtumwa wake Yohana… Wakati ufunuo unatolewa na Mungu na kupewa Yesu wakati huo Yesu ameshatoka Duniani yuko Mbinguni (kwa mujibu wa bible), lakini bado inaonyesha Mungu ndiye mkubwa Yesu bado ni wakutumwa ili awaonyeshe watumwa kuhusu mambo yao yatakayokuja kama tulivyosoma. Zipo Aya nyingi sana zinazoonyesha wazi kuwa Yesu alikuwa halijui kabisa fundisho la tatu na wala kuhusu kuwa yeye ni Mungu.

Wanafunzi wa kwanza walimuelewaje Yesu?

Matendo ya Mitume 3:13 imeandikwa hivi… Mungu wa Ibrahimu na wa Isaka na wa Yakobo, Mungu wa Baba zetu amemtukuza Mtumishi wake Yesu ambaye nyinyi mlimsaliti na kumkana mbele ya Pilato, alipokuwa ametoa hukumu yake ili afunguliwe.

Maneno ya wanafunzi yalikuwa wazi kuwa Yesu ni Mtumishi wa Mungu tu yaani Mtume pia ni Nabii.

Matendo ya Mitume 4:27 imeandikwa hivi…

maana ni kweli Herode na Pontio Pilato pamoja na Mataifa na watu wa Israel walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako Mtakatifu Yesu uliyemtia mafuta. Wanafunzi wanaendelea na msimamo wao kwamba Yesu ni Mtumishi wa Mungu aliyetumwa (Mtume) tu.

Luka 24:19 imeandikwa: -

Akawauliza mambo gani? Wakamwambia mambo ya Yesu Wanazareti aliyekuwa mtu nabii mwenye uwezo wa kutenda na kusema mbele za Mungu na Wanadamu.

Marko 6:2 imeandikwa: -

Na ilipokuwa Sabato aliingia katika Sinagogi, wengi waliposikia walishangaa wakasema huyu ameyapata wapi haya! Hekima gani hii? Aliyopewa huyu? Nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake? Huyu si ni yule Selemala mwana wa Mariamu na nduguyao Yakobo na Yosef na Yuda na Simoni na Maumbu wake hawapo hapa? (Maana ya Umbu ni dada)

Maneno haya yanathibitisha kwamba watu waliomfahamu Yesu walishangaa matendo makubwa anayoyatenda hata hivyo walijua kwamba yeye ni Selemala wa Mwana wa Mariamu tu. Na ni kiumbe mwenye ndugu zake na dada zake, kama watu wengine.

Marko 13:31 tunasoma hivi –

Mbingu na Nchi zitapita lakini maneno yangu hayatapita kamwe. Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna anaye ijua hata malaika wala Mwana (Yesu) ila Baba tu Mungu…

Hapa Yesu alikua anazungumza habari ya siku ya mwisho alikiri wazi kwamba yeye siku haijui hata Malaika hawajui ila Mungu peke yake.
 
Sema amina kubwa kubwa
 
Ukiweza kutofautisha Kristo na Yesu utapata majibu ya ulichoandika

Yohana 14: 8-9
"Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha. Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?"

Yesu ni Mungu
 
Back
Top Bottom