Je, jina la Yesu ni kweli lina nguvu na uwezo mkubwa katika kutenda miujiza hadi leo? Wewe limekutendea makubwa gani? Karibu ushuhudie

There is a power in the name of Jesus

YESU MWENYEWE ANASEMA hawezi kufanya chochote


John 5:30


By myself I can do nothing; I judge only as I hear, and my judgment is just, for I seek not to please myself but him who sent me.
 

MIZANI YA IMANI YA WAKRISTO

Bwana Yesu Kristo alieleza mizani na alama za imani kama ifuatavyo:

1. Mkiwa na imani ya punje ya haridali, mtauambia mlima huu, ondoka hapa nenda kule, nao utaondoka; wala halitakuwapo neno lisilowezekana kwenu. (Mathayo17:20; 21:21; Marko 11:22-23, 9:23, Luka 17:6, 12, 13).

2. Bwana akasema: “Kama mngekua na imani kiasi cha chembe ya haridali mngeuambia mkuyu huu, ng'oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii.” (Luka 17:7).

3. Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia mkiwa na imani , msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, ngo'ka ukatupwe baharini, litatendeka. na yoyote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea. (Mathayo 21:21-22)

4. Amin, Amin, nawaambieni, yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwani mimi naenda kwa Baba. (Yohana 14:12-13).

5. Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lolote nanyi mtatendewa. (Yohana 15:7).

6. Tena nawaambia, wawili wenu mtakapopatana duniani katika jambo lolote watakalo liomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. (Mathayo 7:3-12).

7. Ombeni nanyi mtapewa.... (Mathayo 7:3-12).


Katika mizani hii ya imani ya Wakristo, tumejua kwamba Mkristo atatambulika kwa alama zilizotajwa hapo juu.

Tena hizi ni alama za imani ndogo sana ya chembe ya haridali. Lakini kama Mkristo atakuwa na imani kubwa ataweza kuonesha miujiza mikubwa zaidi.

Vilevile Mkristo mwenye imani ni yule ambaye ataweza kuonesha miujiza na hasa sawa na ya Bwana Yesu bali mikubwa zaidi kuliko yake.

Sasa kwanza tutafute miujiza ya Bwana Yesu katika Biblia, tumeona baadhi yao kama ifuatavyo:

1. Kuponya wagonjwa (Mathayo 8:16, 9:22, na 15:21).

2. Kuponya walemavu (Mathayo 8:1-3).

3. Kuponya mabubu. (Mathayo 9:3-7; 12-22).

4. Kuponya mwenye kupooza upande mmoja (kiarusi) (Mathayo 8:5-13. 9:1-7, 12:22).

5. Kumponya mwenye kifafa. (Mathayo 17:14-19).

6. Kuponya mkono wenye ukoma. (Mathayo 12:15).

7. Kuponya mgongo uliopinda (Kibyongo) (Luka 13:10).

8. Kuwafufua wafu. (Mathayo 9:24).

9. Kugeuza maji kuwa pombe. (Yohana 2:1-9).

10. Chakula kidogo kitoshe watu elfu tano.(Mathayo 14:13-21).

11. Kutembea juu ya maji. (Mathayo 14:22-23).

12. Kuzuia tufani . ( Mathayo 8:23-33).

Hapa nimetoa baadhi ya mifano tu ya miujiza ya Bwana Yesu.

Kama Wakristo hamuwezi kuonesha miujiza ya aina hii au alama ya imani yao sawa na Biblia, basi
mambo mawili yanathibitika.

A. Bwana Yesu pia hakuonesha mujiza wowote bali ni hadithi za kutungwa tu zisizo na ukweli ndani yake.

B. Siku hizi Mkristo yeyote hana imani sawa na chembe ya haridali, bali wote mumeshapotea tayari na hamna alama au dalili yoyote ya imani.

Hali hizi zote mbili ni mbaya sana na za kutisha.

Na dawa yake ni moja tu kwamba muingie katika dini ya Mwenyezi Mungu, ISLAM, baada ya kutambua umoja wa Mungu na Mtume Muhammad s.a.w. bila hivyo mtaendelea kufedheheka siku hadi siku.


TAMBIO:

Ninawapa Wakristo tambio (challenge) kwamba kama wanayo imani sawa na chembe ya haridali, watuoneshe miujiza iliyotajwa hapo juu. Mkristo mmoja au wawili au wajumuike wote, tunataka kuona miujiza tu ya imani yao, hata Pope au wachungaji wenu wajitokeze.
 
🤣🤣
Eti kiti anataka maji, dhahabu
Sie hatuna muda, tunayafukuza Ili kae Roho Mtakatifu ndani ya mtu sio majini

Mathew 24


Jesus answered: “Watch out that no one deceives you.

5 For many will come in my name, claiming, ‘I am the Messiah,’ and will deceive many.
 

Mbona unatuletea ya Musa , lete ya Yesu
 

Yesu alihubiri kwa upendo ??

Hivi ndivyo watu wanavyohubiri kwa upendo ??



LUGHA YA YESU

Kila mti hutambulika kwa matunda yake (Luka 6:44) na vile vile mtu anatambulika kwa ulimi na lugha yake kwamba anazo tabia za aina gani?

Maana lugha ya mtu inaonesha masomo yake, tabia na vitendo vyake.

Hapa tunampima Bwana Yesu Kristo sawa na maandiko ya Biblia.

Bila ya kupoteza muda , ningependa kukuletea baadhi ya maneno na lugha ya Bwana Yesu aliyotumia katika uhai wake.

1. Wasioamini (wasio Waisraeli) wameitwa mbwa na nguruwe. (Mathayo 7:6).

2. Aliwaita watu wabaya: ”Enyi wazao wa nyoka” (Mathayo 12:34).

3. Mayahudi waliitwa: “Kizazi cha zinaa.” (Mathayo 12:40,, 16:4).

4. Mayahudi waliitwa “Wazinifu na wakosefu.” (Marko 8:38).

5. “Ole wenu waandishi na wafarisayo, wanafiki,” (Mathayo 23:16).

6. “Ole wenu viongozi vipofu.” (Mathayo 23:16).

7. “Enyi nyoka, wana wa majoka” (Mathayo 23:33).

8. “Watu wengine waliitwa mbwa.” (Mathayo 15:27).

9. Aliwaita manabii wenzake: “wote walionitangulia ni wevi na wanyang'anyi.” (Yohana 10:8).

10. Aliwaita wanafunzi wake: ”Enyi kizazi kisicho amini, kilichopotoka.” (Mathayo 17:17).

11. Akamwambia Petro “Nenda nyuma yangu Shetani.” (Mathayo 16:23).

12. Akamwambia mama yake: “Ewe mwanamke nina nini nawe? (Yohana 2:4).

13. Akasema mama yangu ni nani na ndugu zangu ni akina nani? (Mathayo 12:48).

14. Siku ya Kiyama atawaita wahubiri Wakristo: “Nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi mtendao maovu.”

(Mathayo 7:23).
 
Na dawa yake ni moja tu kwamba muingie katika dini ya Mwenyezi Mungu, ISLAM, baada ya kutambua umoja wa Mungu na Mtume Muhammad s.a.w. bila hivyo mtaendelea kufedheheka siku hadi siku.
Hahahaha,umenichekesha sana kwa hiyo line hapo kwenye bold

First of all sidhani kama nipo tayari kupokea wanawake bikra 70 na kunywa pombe peponi sijui ahera,also duniani sipo tayari kusimama kupigana vita kwa ajili ya Mungu ninaemini anaweza kila kitu nyie mliofanikiwa kuyaelewa hayo mnatosha
 
Katika uumbaji wote wa Mungu kwa uzao wa Adamu hakuna hata mmoja aliyewahi kufa na kufufuka na kupaa mbinguni bila kuuacha mwili wa nyama na damu ila Yesu peke yake.
Ndio maana anatajwa kuwa aliye hai milele.
Huu ndio muujiza uliozidi miujiza yote wa Yesu mfufuka.
Wengine wote wapo makaburini wakisubiri kiama ya wafu wafufuliwe na wachache sana wawili au watatu walitwaliwa bila kifo hivyo hawana sifa ya kukishinda kifo na mauti bali walipewa neema ya kutokugusa huo mfupa mgumu uliowashinda wengine wote.
 

Kama unaendelea na ukristo utakuwa hata imani ndogo ya chembe ya hardali huna maana hata kuiambia kalamu ianguke kutoka kwenye meza huwezi

Mbona biblia inasema vyengine kuhusu huyo mungu unayemuabudu wewe ??


Kuna vifungu vingi katika Agano Jipya vinavyokana uungu wa Yesu.

Kwa mfano, katika Mathayo 19:17, Yesu alimjibu yule aliyemtambulisha yeye kama ni “Mwalimu mwema” kwa kusema “Akawaambia, Kwani kuniuliza habari ya wema? Aliye mwema ni mmoja…”

Kama Yesu amekataa kuitwa “mwema”, na ameeleza kuwa ni mungu pekee ndiye aliyemwema wa kweli, naye kwa uwazi kabisa ameashiria kuwa yeye si Mungu.

Katika Yohana 14:28, yesu alikuwa anasema:

“Mlisikia ya kwamba mimi niliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahia kwa sababu naenda kwa Baba; kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi.” Kwa kusema “Baba” ni mkuu kuliko yeye, Yesu amejitenganisha na Mungu.

Pia katika Yohana 20:17, Yesu alimwambia Mariam Magdalene awaambie wafuasi zake:

"Yesu akawaambia, Usinishike, kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.

” Yesu amemwashiria Mungu kuwa ni “Baba yangu na Baba yenu” amesisitiza zaidi, tofauti yake na Mungu.

Zaidi ya hayo, Yesu amemwashiria Mungu kuwa ni “Mungu wake”, hakutoa nafasi kwa yoyote kudai kiujanja ujanja kuwa Yeye Yesu ndiye Mungu.

Ingawa katika baadhi ya maandiko ya Paulo, yaliyochukuliwa na kanisa kuwa ni matakatifu,

Yesu anaonyeshwa kuwa ni “mtu” ametofautiana na kutengana na Mungu.

Katika 1 Timotheo 2:5, Paulo anaandika

“Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu.”
 
Msingi wa Ukristo siku hizi ni kifo cha msalaba cha bwana Yesu a.s. Mayahudi na Wakristo wanadhani kwamba Bwana Yesu alifariki juu ya msalaba, kifo cha laana.

A. Mayahudi walidhani hivi kwa sababu ya kupata nafasi ya kumkataa Bwana Yesu, kuwa wa kweli, maana Torati inasema kwamba “Aliyetundikwa amelaaniwa na Mungu, (Kumbukumbu la Torati 21:23).

Kwahiyo Mayahudi walitaka sana kumfisha Yesu msalabani ili athibitike kuwa mlaaniwa na mlaaniwa hawezi kuwa Nabii wa Mungu.

B. Wakristo walikubali kwamba Yesu alikufa msalabani kwa sababu waliambiwa kwamba Yesu amebeba dhambi za watu kwa kufa msalabani.
Hivi wavivu wote ambao hawataki kufuata sheria ya Mungu, mara moja walikubali kwamba damu ya Yesu imetuokoa. (Wagalatia 3:13).
 
Yesu alipofufuka, makaburi yakapasuka, wafu wakafufuka. Baada ya kukufuka wakafa tena au waliyeyuka hamna ajuaye walienda wapi?
 
Mathew 24


Jesus answered: “Watch out that no one deceives you.

5 For many will come in my name, claiming, ‘I am the Messiah,’ and will deceive many.
Hapo uliponi quote inahusiana nn na huu mstari?

Hao fake wako wengi tu na biblia imesema
 
Naona umetoka nje ya mada
Ulichojibu na nilichosrema vitu viwili tofauti
Sina muda wa kupoteza
 
YESU MWENYEWE ANASEMA hawezi kufanya chochote


John 5:30


By myself I can do nothing; I judge only as I hear, and my judgment is just, for I seek not to please myself but him who sent me.
Whatever you ask in my name........John 16:23
 
Whatever you ask in my name........John 16:23

Sasa unaamini yapi maneno ya kweli ?? John 16 :23 au John 5:30 ??

halafu imeanzia John 16 : 19 imeandikwa

Jesus saw that they wanted to ask him about this, so he said to them ....

Hapo anayetupa habari za Yesu ni nani ??
 
Sasa unaamini yapi maneno ya kweli ?? John 16 :23 au John 5:30 ??

halafu imeanzia John 16 : 19 imeandikwa

Jesus saw that they wanted to ask him about this, so he said to them ....

Hapo anayetupa habari za Yesu ni nani ??
Mie nakupa POLE
 
Warumi 10:17
Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.
 
Mie nakupa POLE
Nimeipokea pole yako sasa jibu hoja

Sasa unaamini yapi maneno ya kweli ?? John 16 :23 au John 5:30 ??

halafu imeanzia John 16 : 19 imeandikwa

Jesus saw that they wanted to ask him about this, so he said to them ....

Hapo anayetupa habari za Yesu ni nani ??
 
Warumi 10:17
Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.

Anayesema maneno hayo anaendelea kusema

Warumi 7

14. Tunafahamu kwamba sheria ni ya kiroho. Lakini mimi si wa kiroho; mimi nimeuzwa utumwani, ni mtumwa wa dhambi.

15 Sielewi nitendalo: kwa maana lile ninalotaka kulifanya, sifanyi; badala yake, ninafanya lile ambalo nachukia kulifanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…