Je, jina la Yesu ni kweli lina nguvu na uwezo mkubwa katika kutenda miujiza hadi leo? Wewe limekutendea makubwa gani? Karibu ushuhudie

Shetani hajawahi liogopa. Ndio manaa Kila Siku anaingia Kanisani. Na Kuwavuruga Humo. Sasa Hivi Ni Jina La Maigizo Zaidi kuliko Uhalisia
Kuingia kanisani sio tatizo,kulishinda kanisa ndio tatizo.
Shetani ajawahi shinda jina hilo
 
Kuingia kanisani sio tatizo,kulishinda kanisa ndio tatizo.
Shetani ajawahi shinda jina hilo
Kama Unaona Kuingia Kanisani Si Tatizo Sasa Wewe Unamuepukaje Huyo Shetani Wakati Kwenye Nyumba Ya Mungu Anaweza Kuingia Na Akawadondosha Watu na Kuwafanya Atakavyo yeye. Leo akitoka Kwa Huyu anaingia Kwa Huyu bila Shida Yeyote.

Hapo Keshashinda maana Kaweza Kuingia Mpaka Sehemu anayoabudiwa Mungu. Sehemu mnayosema ni Takatifu
 
Sio wote wanaenda kanisani wanamfata Yesu.
Kwenda kanisani na kumjua Mungu ni vitu viwili tofauti kabisa
 
Ambo ni mengi sana ambayo nimeyaahuhudia kwangu binafsi na kwa wengine. Nilitupiwaga Pepo la Mauti, niliumwa na jamaa mmoja ofisi mate wangu tena wa chini yangu naye alikuwa anaumwa na tukalazwa hospitali moja na chumba kimoja wodini. Jamaa aliumwa sana usiku. Mimi nikaenda muita dr aje amsaidie. Jamaa alikunywa gongo akaanguka akawa mgonjwa. Mimi tumbo tu lilikuwa linaniuma.
Jamaa usiku akaumwa sana nikajua anakufa. Alikuwa akichomwa sindano au kuwekewa drip anaichomoa. Asubuhi kukakucha, ndugu na jamaa wakaja kututumbelea kutuletea chai na Juice pale na jamaa akawa fresh.

Ikafika jioni Ilikuwa 6/6/..... Jamaa alikuwa nje mimi nilikuwa ndani na dereva wa Ofisi. Nikashangaa namwambia dereva neno ambalo tuliongeza zaidi ya miezi 6 "kuwa mimi nikifa, maiti yangu mkiiweka kwenye jeneza na kulifunga juu ya land cruiser nitakunja miguu" tukacheka pale na ghafla naona kitu kimenikumba na mawenge. Jamaa yule mgonjwa alikuwa nje na akaingia ndani akasema" Ndetefyose ulikuwa unajua jana usiku nakufa, sasa wewe ndio utakufa sasa" pale pale Pressure Juu 240 na sukari ikashuka 3 au 2. Moyo unapiga pah pah tena kwa nguvu. Nikawa naweweseka jamaa zangu wamekuja wananishangaa na mke wangu analia nje.

Wakati huo nilikuwa malaya na msela tu ila sijui nilipata Neema gani nikajikuta nasema" Kwa Jina la Yesu, Sifi nitaishi na kutangaza matendo makuu ya Mungu"

Ghafla nikawa sawa, dr akaitwa na kuja kuniwekea drip na nichoma sindano. Toka hapo nimeona mengi sana kupitia Jina Hilo.
 
Brother nafuatailiaga nyuzi zako, ni against God tu. Mimi nakushuhudia leo, Mungu ni kweli na Halisi. Nami nilikuwa kama wewe ila baada ya kupita kwenye jaribu nikaona mkono wake na sasa nakiri uzima katika Yeye.

Bro, shetani hana nguvu kwa muamini. Shetani hana nguvu kwa Yesu. Shetani hana uadui na Mungu na ndio maana wakati wa Ayubu alijihudhurisha mbele za Mungu. Wakati wa Nabii Mikaya Mapepo yalijihushurisha mbele za Mungu. Hizo ni Roho na zina changamanaga, Shetani ana uadui na mwanadamu akipambana kumzuia kuwa na uhusiano na Mungu wake na kumzuia kuingia mbinguni. Nifahamuvyo, shetani ni kiumbe na hapatikani mahali pote kwa wakati mmoja. Nifahamuvyo, mapepo ni roho zinazotangatanga duniani na kama mtu mchafu ndio humuingia ila ukisimama sawa katika utakatifu hawakugusi. Kanisani huwa tunayakemea na kuwatoka watu na kama u mchafu watakuingia sababu na wao ni wachafu. Hivyo ni viumbe dhaifu kama utasimama kweli na Mungu wako.
 
Kikongwe lengo la kuweka hii mistari ni nini? Ulipotea sana humu Faiza kipindi cha JPM naona umerudi sasa kipindi cha Mama.
 
Leo umeandika kitu kizuri sana bro. Mimi nimeona mengi kwani huwa naombea watu huku kijijini kwetu. Nimeona viwete wanatembea, vipofu wanaona, magonjwa yanaponywa, mapepo yanakimbia. Hakika hakuna Jina jingine wanadamu wanapaswa okolewa nalo zaidi ya Jina la Yesu.

Lengo la uzi wako ni mzuri japo changamoto ya kizazi hiki wataanza tukanana wenye dini tofauti. Yataanza mashindano muda si mrefu na uzi kuharibika na si kuelimishana.
 
Bila kusahau shetani ndiye aliyesababisha huyo Yesu auwawe msalabani ili msamehewe dhambi.

LUKA 22​

3 Shetani akamwingia Yuda, aitwaye Iskarioti, naye ni mmoja wa wale Kumi na Wawili. 4Akaondoka, akaenda akasema na wakuu wa makuhani na majemadari, jinsi atakavyoweza kumtia mikononi mwao.


Hapo kwenye Mathayo shetani akamuweka juu ya mnara la hekalu. Naona hapa alisahau kwa jina langu shetani toka.

MATHAYO 4​

5 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu, mji mtakatifu, akamweka juu ya mnara wa hekalu
 
[emoji28][emoji28][emoji28] asa waislam wataangukaje mapepo wakat mapepo yanaishi katika miili ya waisalam(sio wote) na msikitin hakuna nguvu ya kuyachomoa.
 
[emoji28][emoji28][emoji28] asa waislam wataangukaje mapepo wakat mapepo yanaishi katika miili ya waisalam(sio wote) na msikitin hakuna nguvu ya kuyachomoa.
Wao huyapunga. Niliona mkutano mmoja wa Mashehe Morogoro. Wanayapunga tu kwani Shetani hawezi mtoa shetani mwenzake.
 
Swadakta😇
 
mjomba shusha nondo hizi kuna watu watapona kwa ushuhuda wako...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…