Sawa we jifananishe na Mungu, kuna mwenzio mmoja alikuwa akiishi kule Misri alikuwa anajifananisha na Mungu na alifika pahala akakufuru kabisa kwa kujiita yeye ni Mungu, Mungu alimpa pigo moja tu kisha baada ya kufariki kwenye maji bahari ilimkataa na kumtema na kila akizikwa baada ya muda watu wanaukuta mwili wake juu yani na ardhi pia ilimkataa na mwili wake hauozi mpaka leo hii amebaki historia vizazi na vizazi na Mungu amefanya ivo makusudi ili tupate kujua ukuu wake na iwe fundisho kwa wote tuliobaki.
Hivyo ni vitisho vya kizamani, Leo huwezi kunidanganya hivyo.
Mummification Tecnology ya Ancient Egypt, mkaitengenezea hadithi zinazowapendeza.
Lakini pia hakuna nilichokitoa nje ya maandiko katika hoja yangu ya kufanana.
Mungu ana Upendo, na wewe unao.
Mungu ana huruma, hata wewe unayo.
Mungu anachukia, hata wewe kuna unavyochukia.
Mungu anasamehe, hata wewe anasamehe.
Mungu ana hili na lile kama Mimi na wewe tu. Hoja ya kusema hafanani na chochote ni Uongo.
Mungu ana wasaidizi sawa na viongozi wa dunia.
Mungu ana subira sawa na Mimi.
Mungu ana jeshi sawa na USA NATO.
Mungu ana Kiti, sawa na baba nyumbani.
Usisahau kuwa wapo walioona kichogo chake, isijekuwa kinafanana na changu au chako pia.
Na kama kichogo kipo, mengine yaliyokosa nakuachia wewe.
Kama mnachotofautisha ni kiwango cha Upendo, basi hata binadamu wanatofautiana pia. Wako wewe ni tofauti na ule wangu.
Kama Kufuru ingekuwepo kweli basi hakika ninyi watu wa dini ndio muongozao Kufuru, maana mpaka sasa mmejiumbia lidubwana LA kufikirika vichwani mwenu, Kuuubwaa na kulijajaza sifa nyiiingi na mkaamua kuliita Mungu. Kimsingi hilo lidude halipo na halitawahi kuwepo.