Yesu hakuwa nabiii bali akuwa Mesiya!! tuanzia hapo kwanza ili tuendelee na mengine.
Ujio wa Yesu kristo kama Mesiya ulitabiliwa na manabii wengi tu akiwemo Zakaria, Isaya na wengine kuonyesha ukuu wake.
Isaya 7:14: "Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli”
Isaya 9:6: "Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume, na uweza wa kifalme utakuwa juu ya mabegani mwake. Naye ataitwa jina lake Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani."
Mika 5:2: "Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katiaka Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.”
Utabiri kuhusu kifo chake pia kilishuhudiwa na manabii wa kale
Zakaria 9:9: " Furahi sana, Ee binti Sayuni; piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazam, mflame wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwana-punda, motto wa Punda” ( Neno hili lilitimia wakati Yesu akiingia Yerusalem huku akiwa amempanda wanapunda)
Zaburi 22:16-18: "Kwa maana mbwa wamenizunguka; kusanyiko la waovu wamenisonga; wamenizua mikono na miguu. Naweza kuihesabu mifupa yangu yote; wao wannitazama na kunikodolea macho. Wanagawanya nguo zangu, na vazi langu wanlipigia kura.” ( Hapa neno hili lilitimia akiwa msalabani na wakati walipoipigia kura Kanzu ya Yesu)