Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Miaka ya nyuma nkitokea huko kwetu kaskazini kuja hapa mjini Dar'slam nilisema ntahamia huku kabisa ila baada ya kufika na kukutana na kero za mji nkapachukia na kuamua kubaki mgeni tu.
 
Miaka ya nyuma nkitokea huko kwetu kaskazini kuja hapa mjini Dar'slam nilisema ntahamia huku kabisa ila baada ya kufika na kukutana na kero za mji nkapachukia na kuamua kubaki mgeni tu.
 
Asalam wanajamvi?

Niende moja kwa moja kwenye mada! nini kilichopo nyuma ya hilo jina. Nini unakikumbuka ukajiita hilo jina! yapo majina mengi yanatoa tafakari na burudani!

Nikianza na mimi kindikinyer leborosier

Ni muunganiko wa vijiji vinne vilivyoandkwa kwa kifupi:

Kindi ni kijiji kimoja kipo kibosho kilimanjaro ambapo niliwahi kukaa kwa miaka minne nilijifunza uchaga na tamaduni zao zilinivutia na hua napakumbuka sana!

Kinyer (lendikinya) ni mtaa mmoja upo monduli umasaini niliwahi kwenda kusanya data nikajifunza mambo mengi ya kimasai.
Na tamaduni zao pia!

Leboro ni kijiji kingine kipo Manyara wilaya ya mbulu kata ya mama isara, ni chimbuko la wambulu (wairaki) niliwahi kwenda kukaa na kufanya shughuli zangu pale kwa muda pia, ni mahali pako vizur sana milima ile hali ya hewa ya ubaridi.. napakumbuka sana!

Na mwisho sier (esere) ni kijiji kipo wilaya ya ngorongoro mkoa wa Arusha kata ya enduleni, hapa kuna mambo mengi sana yalinifanya niishangae sana Tanzania, madini, mapango ya kale, na nyayo za mtu wa kale ambae zipo pembeni kidogo panaitwa laitolye, wanaishi wamasai nilijifunza mengi pia!!

Nini kinakukumbusha ukitazama jina lako la JamiiForums!!

Uzi tayari
Kindi ni kijiji kinafuga majambazi sana. Waliwahi kumuua Padre kwa ajili ya sadaka.
 
Jina langu MIIKU ni mzee kwa kichaga yaani napenda sana kusalimia watu Miiku hasa tukikutana wachagga.
 
Jina langu hili nilipewa na Bibi yangu.Jina la kabila langu.Wenye hilo kabila wanaelewa.Maana yake ata sikumbuki.
Haha lazima wewe ni mchagga kutoka kibosho, mkabasia, mkanoti, mkabengi, mkachanuo.
 
Mm asili ya jina langu Ni mwanamziki wa ki Kongo franco luambo makiadi nadhani haina haja ya kumuelezea huyu msanii maana alikuwa very popular hasa kwa nyimbo zake mamuu, Mario,pesa position , attention na sida, testament ya bouwe,azda,colonel Bangala nk
RIP FRANCO LUAMBO MAKIADI (1938_1989)
lucas mobutu
Hivi rombo mkoani Kilimanjaro hakuna sehemu inaitwa makiadi?
 
Unamfahamu vizuri Da Vinci? Nilisoma minovo yenye profile zake no "noma"
Nilikuwa napenda masomo ya biashara,katikati ya form three nikaumwa,nilivyopelekwa hospitali nikaulizwa kama nilikuwa tayari nimekula,sikujua kilichokuwa kinafuata,nilidungwa sindano moja Kali had I nikaanguka chini Akili ziliporudi nilimuuliza Dr.ni dawa gani nimedungwa,akajibu tu 5mega nikashindwa kuelewa ila nilichukua hatua zaidi nikabadili kwenda sayansi had I sasa ni Pharmacist
 
jina langu (la jf) ni buffet,,,,,,,,,,mwaka flani nikiwa depo ilifikia hatua nikakata tamaa na nikajawa na mawazo/fikra za kutoroka kwa ule msoto,,,,,siku moja tumetulia mesi nikachukua jarida kwa afande kimaro alikuwa anasoma,jarida hilo lilikuwa limechapisha habari iliyoandikwa na bilionea Warren buffet yenye title "economic intelligence",habari ile ilielezea sana mafanikio na harakati za kiuchumi lakin mm nilifanya kubadili context ya story,kutoka economic kuja militarily, ushuhuda aloelezea buffet na njia njia ngumu alopitia hadi anakuwa among the global billionaires ilifanya nijipe moyo na kuamini kuwa ninaweza pia na nitatoboa,asante Allah,I made it and am proud of this job,,,,Warren buffet is mine real model
Aaah aaah hongera ila wale motivation speaker sio wa kuwaamini saana wanatuchuuza saana... Kama yule buffet sijui kama kwel kapitia ugumu.

Kwa iyo vipi ndugu baada ya kuakaza mambo yanenda sawa mpaka sasa?
 
Aaah aaah hongera ila wale motivation speaker sio wa kuwaamini saana wanatuchuuza saana... Kama yule buffet sijui kama kwel kapitia ugumu.

Kwa iyo vipi ndugu baada ya kuakaza mambo yanenda sawa mpaka sasa?
mpaka sasa mambo yako sawia mkuu,karibu songea kikosi cha 411kj ruhuwiko
 
mpaka sasa mambo yako sawia mkuu,karibu songea kikosi cha 411kj ruhuwiko
Aaah aaah watata saana nyie tukiingia hanga zenu....

Tukaribishane makanisani na misikitini, bar na mitaani....

Ila huko kikosini msala mkuu
 
Daah ni story ya kusikitisha na kuhuzunisha that's why nalewa ili niwe nasahau sometimes nalala kabisa bar nanyanyuliwa napalekwa home ..nikipata wasaa naperuzi jamii forums nkiwa kwangu nimejifungia peke angu sina mda na jirani wala watu.

Kwanzaa nimeacha assets zangu nkatoweka sjulikan nilipo na rafki nikisema ndugu nadanganya maana Mimi mwenyewe siwajui ndo nina almost 3yrs nimekuja kuishi hili eneo as ordinary person hakuna anaejua background yangu wala jina baba mwenye nyumba ananijua jina tu kodi namlipa fresh japo ananidanganya mambo mengine na michango hapo home ili kunipiga pesa Mimi Nampa tu sihoji chochote hajui nafanya kazi gan pesa natoa wapi

japo kuna sister jiran anijui jina ananiita mlevi mmoja ndo nimelipenda natumia humu ndo akiona nimechelewa kurudi atanitafuta ataomba Msaada nisaidiwe kubebwa sometimes anakuja ananisaidia kufanya usafi sometimes ananikuta asubuhi na pombe zangu kazaa mezani anazichukua anazitupa ananifokea sana sometimes ananipikia

Mara nilale kweny baraza za watu hapo nimelewa wananisachi wananichukulia phone pesaa ila hyo hainiumizi kichwa.. Pesa kwangu hazina samani ni jambo dogo.. Makaratasi.. Pesa sio kila kitu nyie jidanganyeni tu

Nalewa nazidiwa na pombe mpaka nazima kwa kifafa napelekwa hospital huyu sister sijataka kujua jina Lake namuita Miss annoying maana naona ni msumbufu ananifuatilia life langu ..well anakuja kunicheki hospital ananiletea matunda tunapiga story na nikiwa sijalewa naongea point na mcheshi kwelikweli .

ila zle story zangu zakwenda ugaibun kpind hcho kutafuna papuchi siziingizi tukiongea [emoji23] mabaharia mnaelewa..tuachane na hlo hako kalikua kautani tu sitaki mtu hapa nlpo ajue Mimi na background ila yote tisa Mungu ambariki tu kwakweli

Tuachane na hayo sku nikipata mda ntaandika kwa nini niko hivi nadhani kuna somo watajifunza watu
Hapo peke yake nimeumia Sana sipendi kusikia au kuona mtu anaishi maisha hayo japo anakuwa ameamua
 
Feb mwaka huu ilizinduliwa muvi ya Captain Marvel iliyochezwa na Brie Larson..nampenda sana huyu mwanamke very wife material na yuko sexy. Kwakua ana jina la kike hvo sikuona kama ni vzuri kutumia jina la kike. Kwenye muvi hiyo katumia jina la Carol Denvers kwa kifupi wansmwita "Vers" Nimelipenda kabisa hilo jina ndio nikaona nibadili kutoka Da'Vinci to Denvers.
Usichanganye na Denver (bila s ) wa kwenye money heist. Denver ni sehemu iliyoko corolado huko usa
 
Back
Top Bottom