Asalam wanajamvi?
Niende moja kwa moja kwenye mada! nini kilichopo nyuma ya hilo jina. Nini unakikumbuka ukajiita hilo jina! yapo majina mengi yanatoa tafakari na burudani!
Nikianza na mimi kindikinyer leborosier
Ni muunganiko wa vijiji vinne vilivyoandkwa kwa kifupi:
Kindi ni kijiji kimoja kipo kibosho kilimanjaro ambapo niliwahi kukaa kwa miaka minne nilijifunza uchaga na tamaduni zao zilinivutia na hua napakumbuka sana!
Kinyer (lendikinya) ni mtaa mmoja upo monduli umasaini niliwahi kwenda kusanya data nikajifunza mambo mengi ya kimasai.
Na tamaduni zao pia!
Leboro ni kijiji kingine kipo Manyara wilaya ya mbulu kata ya mama isara, ni chimbuko la wambulu (wairaki) niliwahi kwenda kukaa na kufanya shughuli zangu pale kwa muda pia, ni mahali pako vizur sana milima ile hali ya hewa ya ubaridi.. napakumbuka sana!
Na mwisho sier (esere) ni kijiji kipo wilaya ya ngorongoro mkoa wa Arusha kata ya enduleni, hapa kuna mambo mengi sana yalinifanya niishangae sana Tanzania, madini, mapango ya kale, na nyayo za mtu wa kale ambae zipo pembeni kidogo panaitwa laitolye, wanaishi wamasai nilijifunza mengi pia!!
Nini kinakukumbusha ukitazama jina lako la JamiiForums!!
Uzi tayari