Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Kuna binti nilimpenda sana bahati mbaya Mungu akampenda zaidi anaitwa malula,so kwa ajili ya kumbukumbu nikaligeuza na kuwa lamalu
 
Shimba ya Buyenze what the meaning ya hilo jina kuna muda huwa linapop kichwan kwangu 🀣🀣🀣
Shimba (Simba)
ya (lenye)
Buyenze (Manyoya)

Manyoya ya simba dume (mane) ndiyo humtambulisha jinsia yake na pia hutumika kama kivutio kwa masimba jike ambayo huchukulia urefu, uzuri wa rangi na density ya manyoya hayo kama kiashiria cha DNA nzuri. Hivyo ili simba dume liweze kutawala na kumiliki majike kadhaa ni lazima liwe na manyoya marefu, yenye afya na yenye kuvutia (kama alivyokuwa Bob Junior). Na likiunguruma kwa sauti yake ya kimamlaka huku likiyatikisa manyoya yake kila memba wa himaya yake inabidi atilie maanani na kuzingatia ujumbe uliokusudiwa maana akipuuzia anaweza hata kuuliwa.

By the way, jina hili SYB linapo-pop kichwani mwako huwa lina-pop kwa mema au mabaya? Furaha au huzuni? Upendo au chuki? πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ™πŸΏ



Huyo Shimba ya Buyenze atakuwa kakuingia moyoni tayari amekaa zake huko ndani kwako tulii, we hujui,haiwezekani awe anapop kichwani mwako😁😁😁

Joannah pulizi kaa mbali na jibu hili 😁😁
 
mzee una swaga sanaπŸ˜‚
 
Kuna kitabu chaitwa "The stars shine down" by Sidney Sheldon kinahusu a lady , successfully real estate developer in New York City....am a real estate expert too,there are some resemblance with that character (the IronbutterflyπŸ™kitafute usome,it's a nice book.
 
Mie nikiona hii I'd yako, namkumbuka character m1 ktk Korea Drama inayoitwa "Endless Love" alikua mke wa waziri mkuu, ila hustles zake humo ni balaaa, ndo alikua anatumia hili name "ironbutterfly"
 
Mie nikiona hii I'd yako, namkumbuka character m1 ktk Korea Drama inayoitwa "Endless Love" alikua mke wa waziri mkuu, ila hustles zake humo ni balaaa, ndo alikua anatumia hili name "ironbutterfly"
Yap,hili jina ni la mwanamke mwenye harakat kabambe ktk utafutaji rizki,iwe kwenye kazi,uongozi,biashara yani ni hustlers
 
Ngoja tusubiri jibu lake.😁😁
 
Nilikuwa na jina langu la Riyan nikafutiwa akaunti.

Nikabadilisha na kuitwa liyan.

Nalipenda jina la Riyan kiasi cha kupangilia majina ya watoto wangu kuwa

1.Ian
2.Ivan
3Riyan
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…