Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Hahaha mkuu umenikumbusha...
Id yangu ilikua hivi,...

Ni kipindi natoka Rwanda nikiwa na wenzangu wanne sasa tuliondoka mda sio Kigali tukafika boda mida ya usiku na hapakua na usafiri wa kutuchukua kwa upande wa Tz. Sasa akatokea mchaga mmoja ana semiteller akatuambia atuchukue kwa elfu mbili mbili kwa kila mmoja mpaka mbele mbele. Sasa tukapanda kwenye kontena mulikua na magunia kama saba ya karoti, hakika siku hiyo nilitafuna kama za kwangu. Na hapo ndo jina hilo likapatikana.
 
Che - ni kiambishi awali cha sifa ya hadhi.
Yaani kama unaitwa Sombi basi ukishatoka jandoni unaitwa
Che Sombi.
Ni kama makabila mengine yanatumia viambishi awali kama
She - Lukindo
Mwa - Kipesile
Se - Kalinga
Se - Ntongo, nk.
Wazungu utasikia wanaitwa
Allex, Mc - Neell
Perez, De - Quere, nk

Mittoga ni jina la hadhi ya ukoo.
Kumbuka ile "Che" ni kiambishi awali cha sifa ya hadhi, na sio jina.
Kwa mfano ukimsaidia mtu ktk tatizo kubwa anakuja kukushukuru hata kama unaitwa Ally hatamki Ally.
Bali anasema
"Usengwile Mittoga" kama ni mwanamume asiye pitia jandoni, kama kapitia jandoni utaunganisha Kiambishi awali cha sifa ya hadhi na jina la hadhi ya ukoo na utatamka
Che mittoga
Kwa maana ya " Asante Ally "
Hapo inamaana wanaume wa ukoo wa "Chapanjila" wote kama yeyote atafanya jambo zuri hivyo kutakiwa kushukuriwa au kuombwa radhi basi jina litakalotumika ni " mittoga "
Asante Che mittoga
Samahani Che mittoga.
Ndio maana nikatumia hiyo
Avatal.
Usengwile makamanda.
Kunjani


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiongozi mi ID yangu ilikuja baada ya kuwa na demu mkali hatare, ananipenda kuliko chochote kile.
Namimi nikaamini na midevu yangu kama Sultan kumbe chaka....... Et "She loves me" hovyooooo

[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38] dume zima hovyoo!!!!!! Halaf nikiitwa shoga nalalamika
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwaiyo hata tukikuita shoga ni fresh tuu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…