Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

JamiiForums mnakwama wapi? Ebu ungeni behewa hapo.

Nimefafanua ID kwenye huo uzi post namba 1021
 
Iblis Bin Shetan nilijiita jina hili kuwa prove wrong watu kuwa iblis au shetan hawana uhusiano na kuleta maovu au mabaya duniani
Bali maovu na mabaya yanasababishwa na akili za watu wenye chuki roho mbaya kulipiza kisasi halafu wanasema shetani kanipitia
Mimi ni Iblis lakini ni mtu mwema sina ubaya na mtu
 
Wakati najiunga rasmi JF kulikua na malalamiko makubwa sana hasa kutoka kwa wanachama wakongwe kwamba JF imevamiwa na vijana 'weupe kichwani' na 'vilaza' hivyo kuifanya JF kutokuwa 'konki kama zamani'.
Sasa nikajitathmini, nikajipima na kujitafakari na nikafikia muafaka kwamba mimi ni.nani na hata nisiwe kundi lile lalamikiwa.
Basi nikajitunuku nomino mujarab ya ''Ndio walewale''
and here we are....
keeping it rolling....
 
Nilikuwa napenda sana somo la econometrics ambalo 3/4 ya wanafunzi darasani walikuwa hawalipendi ila kwangu ndilo nilikuwa nafaulu kuliko Masomo yote.
 
Reactions: BAK
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…