Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Wakuu, basi hapa jf kuna kila aina ya majina kulingana na hizi ID zetu feki zinazotumiwa humu!

Kikubwa zaidi kuna id nyingine ukiiona unaanza kucheka huku ukijiliuza hii ina maana gani?

Leo naomba tujadili sababu iliyokufanya uchague hiyo id unayoitumia na ina maana gani. Mm kwa upande wangu bwana.,nakumbuka nilikuwa na id yangu moja hivi ikapigwa ban, niaona usinitanie nikaingia usajili mwingine.

Kilicho fanya nitumie jina la "Crimea" ni kwamba wakati flani nchi ya Urusi na nchi siikumbuki jinabwalikuwa katika ugomvi mkali wakigimbea jimbo la Crimea, ule mgogoro hadi ulizusha hofu ya vita ya tatu ya dunia. Hii crimea ikawa maarufu sana midomoni mwa watu na vyombo vya habari, baai na mie nikaona nijinyakulie niifanye iwe nsio id yangu hapa jf.

Twambie wewe nn kilipelekea kuchagua hii id yako?

GENTAMYCINE ni Mghani ( Waswahili mnaita Rapa sijui Repa ) ila Wakongo ( Wazairwa ) wanaita ' Atalaku ' na Wafaransa wanaita ' Animateur '. Kama kuna Repa / Rapa ambaye Bendi ya Wenge Musica BCBG huwa ikienda Kupiga mahala popote pale iwe Afrika au Ulaya au Marekani halafu GENTAMYCINE majina yake halisi yakiwa ni Pitshou Lisimo hayupo basi kuna uwezekano mkubwa sana hiyo ' Show ' ama ikaboa au hata isijaze Watu kihivyo.

Baada ya Kuondoka kwa Marepa / Marapa wa mwanzoni wa Bendi ya Wenge Musica BCBG akina Roberto Wunda Enkokota ( ambaye sasa anaumwa Saratani ya Koo na yupo zake huko nchini Ufaransa ) na baadae Mwalimu wa Marepa / Marapa wengi Congo DR Tutu Caludgi majina yake kamili akiitwa Yombo Lumbu aliibuka huyu Rapa / Repa GENTAMYCINE au wengine humuita ANTIBIOUTIQUE ambaye ameweza kuiweka Bendi nzima ya Wenge Musica BCBG chini yake Rais mwenyewe Jean Bedele Tshituka Mpiana ( JB Mpiana ) hapo juu ilipo.

Rapa / Repa huyu GENTAMYCINE ni Mchangamfu, Mbunifu na ni Mjanja Mjanja mno bila kusahau pia kuwa ana Kiwango Kikubwa sana cha Elimu tena ya Chuo Kikuu ila hakupenda Kuitumia Elimu yake kwa kile alichosomea na badala yake akaamua aendeleze Kipaji chake cha Kuimba na hasa hasa Kughani huko na kwakweli amekuwa ni ' Kivutio ' kikubwa sana wa Wapenzi wa Muziki wengi wa Congo DR na ndiyo roho nzima ya Bendi kwani asipokuwepo Yeye basi hakuna starehe wala raha tena kutokana na kwamba ana Vitu ' adimu ' sana ambavyo huwezi Kuvikuta kwa Marepa wengine wa Kizazi chake kama Kerozene ( jina kamili ni Eyale Kalondji ) aliyekuwa Rapa / Repa wa Bendi ya Quarter Latin ya Koffi Olomide, Brigade Sabateur ( jina kamili Rwinga Keps ) aliyekuwa Rapa / Repa mahiri wa Wenge Musica Maison Mere yake ' Mtaalam ' wa Kung Fu na Mmiliki wa Black Belt Ngiama Makanda Werrason na Kila Mbongo ( jina kamili Mazikou Ghislain ) aliyekuwa Rapa / Repa wa Bendi ya Extra Musica Zangul chini yake Mpiga Solo hatari sana wa Kizazi cha Pili Roga Roga ( jina kamili ni Ibambi Ikombi )

Na huu ndiyo ' Uzao ' kamili wa hii ID yangu hapa Jamvini JamiiForums nikiamini ya kwamba matendo yangu mengi hapa na uwasiliwashi wangu wa mambo mbalimbali basi navivaa vizuri mno Viatu vya Rapa / Repa wangu Kipenzi kabisa wa Bendi ya Wenge Musica BCBG Pitshou Lisimo a.k.a GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE.

Kila la kheri,
 
Mwanzoni nilikuwa natumia ID moja, ikikuwa maarufu sanaa humu hasa kipindi cha uchaguzi, baada ya sekeseke la lowassa na vijana wa IT, nikabadili ID nikajiita Id nyingine ile nayo nikaona miyeyusho,

Hii sasa ni baada ya Bibi yangu kuniambia utakuja kuwa Mangi kweli,
Kama si juwa na mapesa mingimingi basi hata Rais.

Kwasasa naona pesa ndo zinakuja taratibu na wosia kutimiaa.
Nikifika 35s nitakuwa tajiri mkubwa tz.
 
Back
Top Bottom