Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Kiungo bora kabisa kuwahi kutokea katika medani ya Soccer

"Xavi Hernandez Creus"
 
GENTAMYCINE ni Mghani ( Waswahili mnaita Rapa sijui Repa ) ila Wakongo ( Wazairwa ) wanaita ' Atalaku ' na Wafaransa wanaita ' Animateur '. Kama kuna Repa / Rapa ambaye Bendi ya Wenge Musica BCBG huwa ikienda Kupiga mahala popote pale iwe Afrika au Ulaya au Marekani halafu GENTAMYCINE majina yake halisi yakiwa ni Pitshou Lisimo hayupo basi kuna uwezekano mkubwa sana hiyo ' Show ' ama ikaboa au hata isijaze Watu kihivyo.

Baada ya Kuondoka kwa Marepa / Marapa wa mwanzoni wa Bendi ya Wenge Musica BCBG akina Roberto Wunda Enkokota ( ambaye sasa anaumwa Saratani ya Koo na yupo zake huko nchini Ufaransa ) na baadae Mwalimu wa Marepa / Marapa wengi Congo DR Tutu Caludgi majina yake kamili akiitwa Yombo Lumbu aliibuka huyu Rapa / Repa GENTAMYCINE au wengine humuita ANTIBIOUTIQUE ambaye ameweza kuiweka Bendi nzima ya Wenge Musica BCBG chini yake Rais mwenyewe Jean Bedele Tshituka Mpiana ( JB Mpiana ) hapo juu ilipo.

Rapa / Repa huyu GENTAMYCINE ni Mchangamfu, Mbunifu na ni Mjanja Mjanja mno bila kusahau pia kuwa ana Kiwango Kikubwa sana cha Elimu tena ya Chuo Kikuu ila hakupenda Kuitumia Elimu yake kwa kile alichosomea na badala yake akaamua aendeleze Kipaji chake cha Kuimba na hasa hasa Kughani huko na kwakweli amekuwa ni ' Kivutio ' kikubwa sana wa Wapenzi wa Muziki wengi wa Congo DR na ndiyo roho nzima ya Bendi kwani asipokuwepo Yeye basi hakuna starehe wala raha tena kutokana na kwamba ana Vitu ' adimu ' sana ambavyo huwezi Kuvikuta kwa Marepa wengine wa Kizazi chake kama Kerozene ( jina kamili ni Eyale Kalondji ) aliyekuwa Rapa / Repa wa Bendi ya Quarter Latin ya Koffi Olomide, Brigade Sabateur ( jina kamili Rwinga Keps ) aliyekuwa Rapa / Repa mahiri wa Wenge Musica Maison Mere yake ' Mtaalam ' wa Kung Fu na Mmiliki wa Black Belt Ngiama Makanda Werrason na Kila Mbongo ( jina kamili Mazikou Ghislain ) aliyekuwa Rapa / Repa wa Bendi ya Extra Musica Zangul chini yake Mpiga Solo hatari sana wa Kizazi cha Pili Roga Roga ( jina kamili ni Ibambi Ikombi )

Na huu ndiyo ' Uzao ' kamili wa hii ID yangu hapa Jamvini JamiiForums nikiamini ya kwamba matendo yangu mengi hapa na uwasiliwashi wangu wa mambo mbalimbali basi navivaa vizuri mno Viatu vya Rapa / Repa wangu Kipenzi kabisa wa Bendi ya Wenge Musica BCBG Pitshou Lisimo a.k.a GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE.

Kila la kheri,
Gentamycine pia ni dawa antibiotic
 
Mi nilichagua jina hili kwa kuwa professionary ni daktari wa binadamu na chichi ni jina langu la utani.kuhusu avatar huwaga napenda kuwekaga za nyani wakipiga ulabu coz mi mwenyewe nakunywa pombe
 
Gentamycine pia ni dawa antibiotic

Kwani uliambiwa kuwa sijui maana yake au Kiherehere tu? Nimejibu hoja ya jinsi nilivyolichukua hilo jina kwa Mtu mmoja na sijaelezea maana yake kwakuwa najua kila Mtu mwenye akili timamu angetaka kujua maana yake basi ange ' google ' na kuipata kama siyo na kuielewa pia.
 
Mzee wa liver mimi ni mnazi w liver miaka mingi mapenzi yangu kwa klabu hii ndio yakapelekea nitumie hilo jina hapa jamvini JF
 
Cc12 ni ujazo wa dawa kwenye sindano anayopigwa ng'ombe....
 
Back
Top Bottom