Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Kujua maana ya jina langu unatakiwa uwe na imani

Imani thabiti

Wasio na imani wengi wamejikuta wakipata tafsiri mbaya yenye kuleta taswira ya mtu flani mshari, muhuni, nk

Niambie mpaka hapo imani yako imekuongoza na kukupa tafsiri gani?

Bila shaka huwezi kuwa miongoni mwa wapotofu wasio na imani
 
Jina langu maana yake ni ni ndinga moja luxury ya bei kaliii sana tokea pande za Italy 🇮🇹 huko
Wakati nikifanya jitihada za kuhakikisha usemi wako wa tafsiri wa hilo jina ikanibidi ni search google

Hiki ndicho walichoniletea

1648504248725.png
 
'Niliamua kujiita Carleen, baada ya kusoma ni mtu wa aina gani halafu najiona kabisa sifa zote hizo kiukhalisia ninazo, teh'..!!😂😂

Mimi bado napenda lile jingine hadi leo moyoni huwa nakuita vile
 
We kweli kiokote! Unadhani wote tunaona nyuzi zote? Unaweza kuta hata hili jibu ulilotoa hapa lilishawahi tolewa na mtu, je, tuseme hutaki kuumiza kichwa na kwamba umekopi tu??!
Basi Ngoja nimuulize Babu maana ya Hili Jina.
 
Mimi nikifafanua tu basi identity ya huyu kiumbe nyuma ya ID atajulikana na wengi...😉

Nipe siri ya ID yako kwanza Chakorii 😊
Nimelitoa kwenye movie ya kihindi inayoitwa udaan (Kama sijakosea)alikuwa ni main character wa hiyo movie.ni mtoto mchangamfu sana na mcheshi muda wote(mwanzoni mwa movie)hata ukimkosea anapoteza furaha baada ya muda baada ya hapo anarudi kwenye maisha Yake ya uchangamfu,furaha/ucheahi na upendo

Ni movie ndefu sana utafikiri treni ya kwenda mbinguni.
Sikuwahi kufifikia katikati wala kuimaliza

Anaitwa Chakor lakini nikaongeza ii Kwa lafudhi ya watu wa kaskazini.
0E1E35F9-5DD8-404E-8839-30C3A0DD83E5.jpeg
Huyu ndie Chakor
Watu8
 
Back
Top Bottom