Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Ahaa! Ni vyema nami mkaelewa maana ya jina langu MONGOIWE; MONGO inamaanisha Supu na IWE ni jiwe hivyo linamaana ya supu ya Jiwe, jina hili asili yake ni kanda ya Ziwa na linatokana na kabila ya KISUKUMA.
Jina hili mimi kwangu nilipachikwa na babu yangu kotokana na yeye kupenda kunitania lakini pia tabia yangu ya kupenda kukimbilia mlimani kilamara kupanda mawe na majabari ya Mwanza.


Ahsanteni sana Supu ya jiwe, Mauzauza, Gold digger na Zebaki 😉
 
Fundi Mchundo ni fundi mchundo kweli kitaaluma. Kweli kabisa, ingawa nashukuru kuwa kuna baadhi wanaotaka kunipandisha kufikia uhandisi! Huko sikuwezi.

Amandla......
 
Fundi Utumbo, Fundi uwiano usio maalum! Ili mradi tu. Fundi Utumbo nilipewa na mtu mmoja makini sana!

Amandla......

Mkuu siku zote kwangu mimi wewe ni Mhandisi Mkuu...huyo aliyekuita hivyo alikuwa na lake jambo.
 
The great prophet of the land, Mugo wa Kibiro had in his prophecy fore seen this happening. He prophesized the white man invading the ridges. Mugo prophesized that "…there shall come a people with clothes like butterflies…" The people did not believe what he prophesized and instead poured scorn on him, laughed at him and even went to the extreme of suggesting he was not "well". He was rejected by his own people in is own land; "The seer was rejected by the people of the ridges".
Mugo's last words on earth before he died were whispered to his son's ear, he said "salvation shall come from the hills. From the blood that flows in me, I say from the same tree, a son shall rise. And his duty shall be to lead and save the people!"

Hii ni copy and paste kutoka kwenye review ya The River Between by Ngugi wa Thiong'o.

Nilimpenda Mugo kwa sababu utabiri wake una-extend hata Tanzania ya leo, Nchi kuuzwa(Shamba la Bibi), ufisadi kushika kasi, tamaduni kuharibika, watu kuamini kuwa CCM haiwezi kuanguka na wala mafisadi hawawezi kushindwa, na vilevile jinsi watoto/wajukuu zetu watakavyotafuta ukombozi kwa mara ya pili. AMANI IWE KWENU.
 
Nyumbu- kwa sababu wengi hudhani nyumbu ni myama mjinga kumbe ni kinyume kabisa. Nyumbu hawezi kukubali shida hata kama mafanikio yake yatagharimu maisha yake. Ndio maana wakati wa njaa kule Kenya huvuka kuja Tanzania. Njiani hukutana na vikwazo kadhaa, yaani mafuriko, kuliwa na mamba na wanyama wengi wakali. Lakini anakuwa determined kufika anakoenda. Hivyo hujitosa , mbio mbio , mbio mtindo mmoja mpaka afikie Green Pastures alizozitaka. Na kwa kujua kwamba uwepo wake hutegemea zaidi wingi kuliko nguvu, basi huwazidi kete maadui wake kwa kuzaa sana mpaka wenyewe inafika mahali wanabaki wameshiba wala hawahitaji kuwala nyumbu. That way, nyumbu ndo amekuwa gumzo la Serengeti na Masai mara.
HIVYO, TUKIUNGANA KWA WINGI WETU, TUKAAMUA MOJA LA KUPIGANA NA HAWA MAMRUKI WA wazungu na wote watuibiao, tutashinda. they will try to kill us, but we got to keep moving, running, getting more members etc. Mwisho watasema du, hawa watu hawashindwi na hawaishi! Ukimuua Amina Chicfupa, 10 more Aminas will come...and at last we will conqure back our land, na kusihi kama ndugu ndani ya nchi yetu , tuliyoachiwa na mtakatifu Nyerere .......
 
prosperity ni kufanikiwa kwa kile ambacho una amini.niliamua kuchagua jina hili kutokana na mimi kuamini kuwa mafanikio yangu yatakuja sio kwa kumtegemea mtu ila badiliko la kwanza kupata mafanikio lazima lianze na mimi mwenyewe. na katika shida na tabu zote za maisha naamini kuwa kufanikiwa kupo sana regardless of your tribe, elimu, ukoo, rangi, umbo to mention a few.
naweza toa ushauri zaidi kwa watu walio kata tamaa za maisha wanaweza PM mimi kwa mawasiliano zaidi.
tumaini bado lipo usikate tamaa
 
Muda wote napenda sana kuwaona binadamu wenzangu wakiwa na amani. Hii ndo maana naitwa AmaniKwenu.
 
Muda wote napenda sana kuwaona binadamu wenzangu wakiwa na amani. Hii ndo maana naitwa AmaniKwenu.


Amani iwe nawe pia 😉

Have a great weekend 🙂
 
Linatokana na simu niliyokua natumia ukitaka kupokea ilikua inabidi uifyatue na inatoa mlio kama mtu anakoki silaha ndio watu wakanipachika mzee wa AK-47


LOL! Ahsante sana Mzee wa AK-47 🙂
 
Wakati niko school A level nilikuwa napenda sana mambo ya diplomasia na nilikuwa na dream kwamba siku moja nami niwe balozi wa Tanzania katika nchi yoyote. Wenzangu walinipachika jina la Ambassador na wakanishauri nisome International Relations. Matokeo yake? Sikuwa hata balozi wa nyumba kumi! I still treasure and honor my friends, and ofcourse my dream...... With due respect....


Basi kuanzia leo Board of Directors ya JF imekuteua rasmi kama Balozi wa JF popote pale utakapokuwa duniani na cheo hichi ni cha milele. Hongera sana kwa uteuzi huo 🙂
 
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=sQgd6MccwZc[/ame]
 
Oh yeah ... .... Wacha. You need to know the meaning of Wacha unless yuo are not a Chelsick fan.
 
jina langu kama unavyolijuwa kama ujuavyo dawa za kienyeji hutokana na Mizizi Mibichi lakini mimi nikatumia jina la hilo Mzizi mkavu hauchimbwi dawa kama jina langu ulionavyo
 
Kinyamana,hili ni jina lililotokana na lugha ya kinyakyusa likiwa na maana ya Mnayama/Mdudu hatari. Mara nyingi huwa inatumika kama sifa kwa mtu jasiri.Na huo ndiyo ujasiri nilionao.

umenikumbusha "kinyamana, akalele fijo..."
 
Back
Top Bottom