Je, Kanisa Katoliki ndiye mnyama wa nne duniani wa Unabii wa Daniel na Ufunuo?

hizo siku za mwisho[nje kidogo ya mada]
'' hutaweza kuuza wa kununua bila chapa ya huyo myama 666'' Huu wakati hatujaufikia au ulipita? je unaamini papa atakujafanya hivyo? je nabii wa uongo atakua nani au ni nani? nieleweshe hapa

Bora umekuja vzr tujadili tueleweshane bila fujo,


Unabii mwingi wa siku za mwisho ule wa mathayo 24, UFUNUO na Daniel kwa 80-90% umekamilika


Halafu tunaposema mpinga kristo sio papa Bali Ni mfumo wa Upapa

Papa anaweza kubadilika akatubu ,Ila Upapa haubadiliki ndio hawa wanaohimiza ushoga ,na Mambo mengine ya Upagani ndani ya Kanisa na nje

Nabii wa uongo au sanamu ya mnyama Ni uprotestant ulioasi hawa Ni makanisa au madhehebu yanajiita ya kikristo lakini yanafata mafundisho ya Roman Catholic


Kabla hujajua kutimilika kwa kutonunua au kuuza inabidi ujue chapa ya 666 Ni Nini


Huu wakati umeshaanza na kwingine haujafika , nitakuja na evidence


Pia kuhusu unabii note kitu kimoja , unabii sio lazima utimie dunia nzima ,unaweza kutimia sehemu fulani Basi na usijue


Chapa ya 666 nitakuja kuelezea baadae baada ya mechi ya Yanga
 
Walokole ,Wasabato na ndugu zenu wa Yehova mnashida Sana...
Walokole Ni ndugu zetu mmewapotosha


Mmewalisha mafundisho ya uongo na Upagani


IBADA YA JUMAPILI

IBADA ZA EASTER(mungu Ashrorethi)

JUMATANO YA MAJIVU

ALAMA ZA MISALABA

ULAJI NAJISI


N.K


Roman ndio mmewafundisha Upagani hao jamaa,


Muulize tapeli mwamposa nani kamfundisha afanye Ibada jumapili, ale kenge, nguruwe ,ashiriki X mass paganism,Easter paganisma, Valentine paganism, n.k
 
Nasubiri ili ni-note kitu. kila neno yatupasa kulipima, yawezekana kuna asilimia flan za ukweli, hizo ndio nazitafuta
 
Unafahamu KARAMU YA MWISHO YA YESU KRISTO!! ALISEMA NINI !!

19 Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, [Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.

20 Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.]
Luka 22:20

FANYENI HIVI KILA MNYWAPO KWA UKUMBUSHO WANGU.
 
Mnafanya hivyo enyi Wasabato na walokole !!?
 
Hiyo Tafsiri ya kwamba:-

-Mwanamke ni Kanisa

-Kahaba ni Kanisa Katoliki

-Bahari ni Idadi kubwa ya watu /Umma

Umepata wapi hizo tafsiri? Zimetafsiriwa wapi katika Biblia?
 
Walokole wote wanafanya hivyo, yaani wanashiriki hii Sakramenti
Nashukuru kutambua hilo.... Lakini Bado huyu hajanijibu Bado Ili nikuulize kingine ..Tena hichi alikisema msalabani kabla ya kukata Robo ... Au niulize tu atalikut swali eti... Waliobaki Mitume wangapi na nani YESU alimkabidhi mtume huyo kwa mamayee !!?!
 
Hiyo Tafsiri ya kwamba:-

-Mwanamke ni Kanisa

-Kahaba ni Kanisa Katoliki

-Bahari ni Idadi kubwa ya watu /Umma

Umepata wapi hizo tafsiri? Zimetafsiriwa wapi katika Biblia?

BIBLIA MBONA INAJIELEZA YENYEWE DADA.!!!
HAKIKA TUNAPOTEA KWASABABU HATUJUI MAANDIKO.

VITABU VYA UNABII vimeandikwa kwa picha Hiyo Ili isiwe Rahisi kwa watu KUJARIBU nakala.


Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko.
Luka 24:45

Yesu akajibu, akawaambia, Je! Hampotei kwa sababu hii, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu?

Marko 12:24


Lakini msipoyaamini maandiko yake, mtayaamini wapi maneno yangu?

Yohana 5:47

MUOMBE ROHO MTAKATIFU ATAKUFUNULIA UTAELEWA TU
 
Wewe Mtoto wa nzi ujibiwe mara ngapi ndipo uelewe.

Mbona unakua na fuvu gumu sana?
 
UKUMBI WA PAPA NA UTAMBULISHO WA SHETANI. (JOKA)
Pope Audiance Hall


 
Ukweli mchungu ni kwamba DINI ZOTE, MADHEHEBU YOTE...... YANA MCHURUZU WA UPAGANI...... HUTAKI.... NI UMEAMUA KUWA MBISHI TU. SHETANI Alishacheza hii kete mapema sana kupitia waanzilishi Wahenga. Na ndio maana Ile dini Moja itakayokuja itaonganisha hizo zote zilizopo na MADHEHEBU yake kwa urahisi coz wale WA kule juu wanajua ukweli ila Nyumbu WA huku chini more than 5bilions wanaenda kwa HISIA na mihemko ya dini. Yesu atawaambia siwajui mimi.
Yeye abadili na makabila yake 12 na watu wote waliohusika kuwa peleka Utumwani na kuwatesa. Wote mataifa yote yaliyohusika Hakuna rangi wataacha kuona. But huu ubishi WA Sabato vs catholic vs Lutheran vs others.... Shetani anacheka tu maana kote huko ameshakumbatia huku anapiga miluzi.
 

KANISA LA MUNGU LITASIMAMA MUNGU NI AMINI NA KWELI.

Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.

KANISA LA MUNGU LIPO MOJA TU.


Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu;
UFUNUO 12.17.

KANISA LA MUNGU NI MOJA NA SI MUUNGANIKO.
 
Sasa mkuu ipi dini au dhehebu la haki ambalo tunapaswa kuabudu maana hayo makanisa yote yamefata mpaka siku ya sabato Kwa waroma na huku tena inadaiwa hta uislam ni wao waanzilishi kimbilio la mwanadamu ni wapi
 
Kuna kanisa limeuwa watakatifu wake kasome ufunuo. Hao ndio watakuwa namba Moja kula jiramba LA hasira za Mungu
 
Sasa mkuu ipi dini au dhehebu la haki ambalo tunapaswa kuabudu maana hayo makanisa yote yamefata mpaka siku ya sabato Kwa waroma na huku tena inadaiwa hta uislam ni wao waanzilishi kimbilio la mwanadamu ni wapi
Hakuna kanisa lililo sahihi yote yana mambo ya kipagani. MUNGU atamhurumia Jacob tu.... Na ataingia AGANO tena na uzao wake tu... Na wote waliohusika ANADili nao sambamba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…