Je, katiba inasemaje kuhusu ukomo wa Raisi kuongoza kwa hali ya sasa, je raisi tuliyenae atakuwa madarakani kwa miaka mingapi?

Je, katiba inasemaje kuhusu ukomo wa Raisi kuongoza kwa hali ya sasa, je raisi tuliyenae atakuwa madarakani kwa miaka mingapi?

Kuna aliyetaka kutawala maisha , leo yuko wapi ? Mtangulize Mungu kwanza
Ukimtanguliza Mungu ndio hufi?Alishatamka mara nyingi kwa kinywa chake kuwa hakuwa tayari kuongeza muda kutawala,wacheni kuzua na kumlisha maneno mzee wa watu.
Waliokuwa wakitoa hayo matamko ya kutaka kuongezewa muda ni haki yao kikatiba kutoa maoni.
 
Hili lilishatolewa majibu.
Akishamaliza muda wake 2025 ,ana haki ya kugombea kipindi kimoja tu,yaani 2025-2030 kama akitaka .

Ila kama kwa mfano Rais angekuwa amekufa 2024 au 2025 kabla ya mchakato wa kusimamisha wagombea ,Makamu wa Rais anakuwa Rais kwa kipindi kilichobaki ambacho ni chini ya miaka miwili na ana haki ya kugombea vipindi viwili yaani 2025-2030,2030-2035 kama akitaka.
 
Nina hakika CCM itashinda chaguzi zote zijazo, swali langu je katiba inasemaje kwa raisi aliyeshika madaraka kutokana na kifo cha raisi aliyekuwa madarakani,kwani katiba inasema atashika madaraka mfululizo kwa miaka kumi itawapo atachaguliwa,kwa hivyo basi je raisi tuliyenae sasa anaweza kutuongoza kwa miaka 14 iwapo atachaguliwa katika chaguzi mbili zijazo au atatuongoza kwa miaka hii minne na miaka 5 ijayo kwa hiyo kuwa raisi kwa miaka 9? Naona kwa sasa hili hakuna anayelizungumzia sote tumebaki kushangilia tu.Je katiba inasemaje kutokana na hali tuliyonayo sasa?
Apewe mi5×5 tena , apende asipende
 
Ningekutukana tusi ila wewe ni mpuuzi tu. Hakuna siku JPM alisema ataongeza muda! Muogope maulana au wewe ni kafiri
Ila kuna kipindi alidokeza kuwa akiondoka madarkani hakuna mtu atakayeweza kumalizia miradi mikubwa aliyoanzisha. Vilevile Spika wa Bunge Mr. Job Ndugai alisema watapitisha bungeni sheria ya kumruhusu Hayati JPM ili aendelee kutawala kwa vipindi vingine.
 
Ingekuwa wewe ungeweza kufanya uho uzuzu,, yaani 2025 asigombee ili kupisha wasukuma au??
Yaan katiba inamruhusu kugombea nafasi kubwa ya urais kwa mara ya tatu mfululizo, eti asigombee ili kuwafurahisha nyinyi wasukuma wenye uchu wa madaraka,

Nadhani unafahamu jopo la watu wa karibu wanaomzunguka, ambao waliteswa wakati wa utawala wa mwendazake, kwaiyo watamchukulia fomu kwa lazima ili agombee kuanza rasmi awamu yake ya sita kwa vipindi viwili vya 2025 had 2035
Wewe na mwendazake,mwendazake na wewe,una uwezo wa kukalili kama mbwa,lkn huna uwezo wa kujifunza,
 
Ila kuna kipindi alidokeza kuwa akiondoka madarkani hakuna mtu atakayeweza kumalizia miradi mikubwa aliyoanzisha. Vilevile Spika wa Bunge Mr. Job Ndugai alisema watapitisha bungeni sheria ya kumruhusu Hayati JPM ili aendelee kutawala kwa vipindi vingine.
Unakumbuka alimjibu vipi mzee ruksa ? Acheni upopoma kwa Marehemu
 
Kuna aliyetaka kutawala maisha , leo yuko wapi ? Mtangulize Mungu kwanza
"Aliyetaka kutawala maisha" Hii ulimsikia mwenyewe kuwa akitaka kutawala maisha au unamwekea maneno mdomoni? Mwenyewe si alishasema kuwa hatoobgeza ata dakika 1 kwenye utawala wake?
 
Kwa katiba ipi?! Katiba iliyopo ni ukomo wa mihula miwili, na yeye mwenyewe alinukuliwa mara kadhaa akisema ataheshimu katiba dhidi ya kujiongezea muda.

Hayupo kwasasa, tujadili yaliyopo.

Kuna walio simamisha mishipa ya shingo kwa kupiga mayowe "... akikataa alazimishweee ..."

Usitupangie ya kujadili, tunajadili yaliyopo kwa kuangalia yaliyopita ili tujue tunaelekea wapi. Haya kumlazimisheni arudi kuwa hai sasa

Mungu mkubwa huenda raisi ajaye 2025 akawa HASHIM RUNGWE hujui nini MUNGU kapanga hamjifunzi tu
 
Hili alilisema mwenyewe siku anaapisha kuhusu wanaopita pita kujiandaa Na urais 2025 watulie muda bado Na chama kinawaangalia closely!
Mnachekesha wasukuma, mbona anasema ye na Magufuli ni kitu kimoja" lakini Bado anafanya overall kwenye engine,
Mama ashajua acheze vipi na akili zenu, mkuu" take it from me, SAMIA tunae hadi #2035__ hutaki jiue
 
Back
Top Bottom