Je, Kila Mwanasiasa Tajiri ni Fisadi?

Facts
 
Issue ni kuwa ukweli sisi waafrika ni wajinga sana

We don't do things for the sake of helping others we do it for our own gains.

Mfanya biashara atakwepa kodi, Mwana siasa atavmchukua rushwa ya mkwepa kodi na hata yeye mwenyewe kuikwepa

Utajiri wa waafrika wengi ni wa kuchukua advantage kwa wanyonge
 
Okay
 
Liliundwa azimio la arusha 1967 kuepusha conflict of interests, mzee mwinyi 1994 akaunda azimio la zanzibar lililofuta yale yote azimio la arusha lililokataza ikiwepo wafanyabiasha kuwa viongozi na viongozi kuwa wafanyabiashara
Asante sana mkuu nilikua sijazaliwa aisee
 
Iko hivi -: Zile Enzi za Mwalimu Nyerere mwanasiasa akipata uteuzi anatakiwa ajaze fomu ya kuelezea mali zake na jinsi alivyozipata na baadaye baada ya muda wake wa uongozi ukiisha kama mali zake zimezidi kupita maelezo hapo itabidi ajieleze alipatapataje !
 
Umesema enzi za Nyerere
Je kwa sasa hali ipo je?
Utaratibu umebadilika?
 
kwanza si kweli kwamba,
kila mwanasiasa tajiri ni fisadi.

Lakini nikiri tu kwamba kuna hiyo dhana ambayo sitaki kusema ni potofu miongoni mwa jamii mbalimbali ulimwenguni, hususani hapa Tanzania.

Kiujumla siasa ni maisha na maisha ni siasa. Ndio maana mapioneer wa falsafa hii ya siasa walisema, human beings are political animals. Na kwamba hayupo mwanadamu mwenye uwezo wa kuikwepa siasa maishani mwake ispokua labda awe manafiki tu. Unaweza kudhani umekwepa siasa za vyama vyama vya siasa majukwaani, badala yake lazima utakutana na siasa za kwenye familia yako, kwenye dhehebu lako la dini, zaidi sana utakutana na siasa kwenye michezo uipendayo, utakutana na siasa kwenye biashara, kwenye kilimo, mahusiano na chochote kile kinachohusisha jamii fulani inayochangamana na kuahidiana mambo mbalimbali n.k.

hii ikimaanisha kwamba,
ukiamu kujizatiti kwenye aina fulani ya siasa kikamilifu, mathalani kwenye siasa ya biashara, vyama, kilimo au ufugaji kadiri nilivyoelezea hapo juu unaweza kutajirika vizuri sana na jamii ikaibua dhana mbalimbali dhidi ya utajiri wako. Wengine watadhani, watasema au kudai kwamba utajiri wako ni kutokana na kutoa kafara ndugu zako, freemanson, ujambazi, ufisadi n.k, dhana ambazo zinaweza kua hazina uthibitisho kabisa.

Sote ni mashahidi jinsi ambavyo waTanzania hujenga dhana mbalimbali dhidi ya utajiri wa wa kutupwa wa viongozi mbalimbali wanaofanya siasa za kidini kama vile mitume, manabii na makuhani humu nchini.

So,
mi nadhani mtu yeyote yule hapa Tanzania ana haki ya kuchagua aina ya siasa aipendayo na kuifanya. Lakini pia ana haki ya kutajirika kadiri awezavyo kulingana na bidii na maariafa yale akonayo. Na mtu yeyote yule anayefanya aina yoyote ya siasa na akatajirika kiudanganyifu au kinyume na sheria atawajibishwa kwa mujibu wa sheria za nchi ikiwa itathibitishwa na vyombo husika vya kutoa haki. Natamani kueleza zaidi but kwasababu ya muda naomba kuishia hapo.

Otherwise,
nakupongeza sana ndugu madau,
kwa namna ambavyo uanabuni hoja zako, unajenga hoja, unatetea hoja zako na kuibua falsafa zenye concepts muhimu na nzito sana jukwaani. Una uwezo mkubwa mno wa kudevelop theories za kutafakarisha na kuibua hisia mseto za kusisimua sana ubongo.
well done and,

God bless you
 
kwanza si kweli kwamba,
kila mwanasiasa tajiri ni fisadi.
Hapa unasema si kweli inabidi utoe na mfano kwa nini si kweli usipite juu juu mdau
Je si kweli
si kweli ki vipi?
Lakini nikiri tu kwamba kuna hiyo dhana ambayo sitaki kusema ni potofu miongoni mwa jamii mbalimbali ulimwenguni, hususani hapa Tanzania.
Inaweza kua potofu au isiwe potofu
Ni kweli maisha asilimia kubwa ni siasa tupu
Kwa leo ndugu mdau tunazungumzia siasa ya nchi kwa ujumla wake
Sio siasa ya kilimo wala siasa ya biashara
Sote ni mashahidi jinsi ambavyo waTanzania hujenga dhana mbalimbali dhidi ya utajiri wa wa kutupwa wa viongozi mbalimbali wanaofanya siasa za kidini kama vile mitume, manabii na makuhani humu nchini.
Hawa sasa kwa leo tuwaache
Tutawaongelea next time
Ndugu mdau asante kwa maoni yako ambayo kimsingi ni ya jumla jumla
Nikiwa na maana hujajikita kwenye swali langu la msingi
Asante kwa pongezi nazipokea 😊
 
ndugu mdau,
kwakua hiyo ni dhana tu miongoni mwa jamii,
uthibitisho wa juu ya ukweli au si kweli unawezakua wa kinadharia zaidi na usio na hitimisho. Dhana hiyo kwa maoni yangu ni darasa au shule tu ya kuongeza uelewa na ufahamu kuhusu mseto wa dhana yenyewe
 
Ahaa sawa asante kwa maoni yako mdau karibu tena
 
Hujamtaja HECHE du hii ni maajabu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…