Je, Kila Mwanasiasa Tajiri ni Fisadi?

Je, Kila Mwanasiasa Tajiri ni Fisadi?

Anaweza kupata utajiri akiwa kwenye uongozi kwa njia halali. Kwa mfano, anaweza kuwa na biashara iliyokuwepo kabla ya kuingia madarakani ambayo inaendelea kukua, kufanya uwekezaji halali, au kupata mapato yanayoruhusiwa kisheria kutokana na kazi na mali zake.
Kwa uchumi wa bongo kupata utajiri ni mchakato mrefu na mara nyingi inakua urithi wa kizazi yaani kama Mo si ajabu kukuta utajiri ulianzia kwa bibi wa baba yake.

Bado hatujapiga hatua kwenye teknolojia ambapo unaweza kulala masikini kuamka tajiri. Sisi tupo huku kwenye kilimo, usafirishaji, uchuuzi n.k ambapo kutajirika ni mchakato unaohitaji muda mrefu.
 
Shehe huwezi kuwa mwanasiasa afu ukawa tajiri bila kuwa fisadi never..
Na wafanya biashara wengi wanajaribu kuingia kwenye siasa au hata kudhamini wanasiasa wakati wa kampeni zao ili waweze kupiga pesa bila kuhojiwa wala kufuatiliwa.
 
Kila mtu timamu anapenda siasa
Siasa ni maisha na maisha ni siasa
KWA KUONGEZEA MWAMBIE SIASA NI KAMA MAJI
KAMA AMBAVYO MAJI HUWA YANATUMIKA AIDHA KWA KUPENDWA AU KUTOPENDWA
HATA SIASA HAIHITAJI KUPENDWA.
UKILA UTAKUTANA NA SIASA
UKINYWA UTAKUTANA NA SIASA
UKIENDA KAZINI UTAKUtaNA NA SIASA
UKIWA KANISANI AU MSIKITINI UTAKUtaNA NA SIASA
UKIWA KWENYE CHOMBO CHA USAFIRI.

SEHEMU ISIYO NA SIASA LABDA NI MAKABURINI AMBAKO NAKO SHERIA ZINAZOTOKANA NA WANASIASA ZINAWEZA KUAMUA HAYA MAKABURI YAHAMISHWE
 
KWA MUJIBU WA SHERIA, KUNA LEVEL YA UONGOZI MTU AKIIFIKIA ANATAKIWA KUJAZA FOMU FULANI ZINAZOONESHA KIPATO CHAKE, UWEKEZAJI WAKE NA MALI ALIZONAZO. LAKINI KATIKA KUKWEPA HILO TAKWA LA KISHERIA BAADHI YA VIONGOZI WASIO WAAMINIFU KAMA KUNA MALI WALIZIPATA ISIVYO HALALI HUWA WANAZISAJILI KUWA ZINAMILIKIWA NA NDUGU ZAO.
NAWAFAHAMU WATU KADHAA WALIOWAHI KUFANYA HUO MCHEZO, MMOJAWAO NI HOMEBOY WANGU.
Kumbe okay
But mimi sijata wa kunipa nimiliki kwa hewa ukijaliwa ni check 😎
 
Sawa nimeelewa kwamba mwanasiasa ana haki ya kumiliki mali na kua na maisha mazuri kwa sababu mbali na uanasiasa wake yeye ni mtumishi kama watumishi wengine

So kama kuna sntofahamu vyombo vya uchunguzi na sheria ndivyo vinapaswa kufanya kazi na sio dhana ambazo wakati mwingine sio halisi

Asante kwa maoni karibu tena
SAWA AUNTIE
NAKUPENDA
 
Siyo kudokoa kidogo au kikubwa sifa ya mdokozi mzalendo hata akidokoa kikubwa basi icho alicho dokoa nacho anakenda kufanyia mambo ya manufaa kwa taifa tofauti na asiye mzalendo..mfano tajiri mzalendo atumii utajiri wake kuujumu nchi yake bali anatumia utajiri wake kwa manufaa ya nchi yake pia ..hivyo UFISADI WA KIZALENDO BADO UPO KUNUFAISHA TAIFA TOFAUTI NA UFISADI USIO WA KIZALENDO
Ahaa asante sana mkuu nimekuelewa sasa nini kifanye ili tupate mafisadi wazalendo kwa faida ya Taifa letu
 
Shehe huwezi kuwa mwanasiasa afu ukawa tajiri bila kuwa fisadi never..
Na wafanya biashara wengi wanajaribu kuingia kwenye siasa au hata kudhamini wanasiasa wakati wa kampeni zao ili waweze kupiga pesa bila kuhojiwa wala kufuatiliwa.
Kumbe ndivyo mambo yalivyo aisee asante kwa maoni Maalimu
 
Ukiwa huna utanyang’anywa hata hicho kidogo ulichonacho (Biblia)

Watu wote wanaogomea nafasi yeyote na kupewa ridhaa na vyama vyao hasa CCM amini wana kitu kwanza (kiuchumi). Ile huwa ni kazi kama kazi zingine anagombea udiwani, anawekeza kisi flani baada ta miaka mitano atapata zaidi ya hicho. Hivyohivyo kwenye ngazi zingine.

Wanaogombea ngazi kubwa zaidi wanakua na nguvu kubwa zaidi ya uchumi na connection. Wakiingia wanatoka wakiwa wamepata zaidi.

Siri iko hapa, unahitaji kitu mkononi ili upate zaidi. Mwenyenacho atazidishiwa, na kinyume chake.
 
KWA KUONGEZEA MWAMBIE SIASA NI KAMA MAJI
KAMA AMBAVYO MAJI HUWA YANATUMIKA AIDHA KWA KUPENDWA AU KUTOPENDWA
HATA SIASA HAIHITAJI KUPENDWA.
UKILA UTAKUTANA NA SIASA
UKINYWA UTAKUTANA NA SIASA
UKIENDA KAZINI UTAKUNA NA SIASA
UKIWA KANISANI AU MSIKITINI UTAKUNA NA SIASA
UKIWA KWENYE CHOMBO CHA USAFIRI.

SEHEMU ISIYO NA SIASA LABDA NI MAKABURINI AMBAKO NAKO SHERIA ZINAZOTOKANA NA WANASIASA ZINAWEZA KUAMUA HAYA MAKABURI YAHAMISHWE
Hakika 📌
 
Ahaa kumbe tatizo wao sio kua wamiliki ila uhalali wake ni upi okay

Sasa tufanye je ?
On equal grounds za kufanya biashara, huyu anakwepa kodi na huyu analipa kodi, unadhani nani atatajirika haraka?

Angalia lecturers wengi wameachana na vyuo wameingia kwenye siasa, ukiachana na stahiki kuwa kubwa ambazo ni haki yao kimsingi, wanakuwa na privileges nyingi, deals zao kupita kwa vimemo tu.

Ndio maana hakuna tajiri yoyote kupitia siasa anakuwa listed huko forces coz wengi pesa zao ni chafu.

We're not jealous, ila kinachosemwa ni ukweli tu, wengi pesa yao ni chafu.
 
Back
Top Bottom