Je, Kila Mwanasiasa Tajiri ni Fisadi?

Yaani umeongea kitu kikubwa sana ambacho tokea uzi umeshushwa hakuna mtu amegusia

Navutiwa na watu like you hawachukulii mambo juu juu

Nimechukua hapo mwenye nacho anaongezewa
 
Kwa muktadha wa mazingira ya kwetu siasa ni ajira wengi wanaogombea ubunge, udiwani, nk hufanya hivyo kama kutafuta kazi na siyo uzalendo wa kulitumikia taifa,

Narudi kwenye swali kuu, mara nyingi kwa kuwa siasa ndiyo inayoendesha kila kitu kuanzia uchumi, afya, elimu nk, wengi hutumia siasa kama ngao ya kufanikisha harakati zao au biashara zao, hapa wengi ndiyo tunaposema kila mwanasiasa tajiri ni fisadi kwa sababu hata kama kabla ya kuwa mwanasiasa labda alikuwa na biashara nzuri tu na zilikuwa zikimpa pesa nzuri tu lazima akiingia kwenye siasa atatafuta favorable climate kwa ajili ya biashara yake ku prosper either kwa kukwepa Kodi, kuweza kupata mikataba minono kwa kutumia nafasi yake ya kisiasa, kupitisha bidhaa zake kinyemela kwa kutumia cheo chake nk, kwa mtazamo wangu mdogo hata kama alikuwa tajiri kabla ya kuingia kwenye siasa lazima utajiri wake utaongezeka maradufu kwa kutumia mgongo wa cheo chake Cha kisiasa na hapa ndipo tunaposema kila mwanasiasa tajiri ni fisadi, tukirudi kwa wanasiasa wengine ambao huingia kwenye siasa na ghafla wanageuka kuwa matajiri wakubwa ni wazi kuwa ukiacha marupurupu wayapatayo ambayo ni makubwa kuliko kawaida pia wengi hununulika na wafanyabiashara kupitisha ajenda zao au kuwapa upendeleo fulani bila kusahau makandokando mengine mengi.
 
Hapa hata mimi najadili tu mada ila sio siasa,
Hua sipo interested sana na mambo hayo,

Mimi nikiingia JF hua naingia kwenye Trending na kuanza kusoma nyuzi bila hata kujua nipo jukwaa gani.
usinifokee bwana kwan mi nimesema unajadili siasa?,, maana yangu ilikua kwamba kuhusu siasa mi sifuatiliagi ila kuhusu habari zako ninazo nyingi mpka ambazo wew hauzifahamu ayu zea🤨😏
 
Umesema hata walimu wa vyuo wameamua kujiingiza huko siasani

Hii inamaanisha kila mtu angependa kupata hiyo nafasi

Isipokua kwa kua hatuwezi kupata hizo nafasi tunaishia kulalamika?
 
Aisee una hoja
Lakini sasa tufanyeni ili ahuweni kwa wale wanaolalamika kila siku

Ambao mi nadhani hata wao wakipata hizo nafasi watafanya hivyo hivyo
 
Ikiwa waccm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…