Je, Kila Mwanasiasa Tajiri ni Fisadi?

Ni kweli wanasiasa wengi matajiri ni mafisadi,

Nature ya biashara hata bila siasa ni unyonyaji, Mfanyabiashara akiwa mwanasiasa ni sawa na kuchimba mfereji wa maji in a steep slope, yatashuka kwa kasi kufata mkondo hayawezi kupanda. Ni kwamba umeirahisishia ile nature ya exploitation.

Hii ni topic mtambuka sana na iko relevant sio kwa tz pekee ni world wide iko hivyo. Fikiria raisi wa Taifa kubwa kama Ufaransa waliostarabika amefungwa kwa ufisadi kutoka kwa Gaddafi, raisi wa Israel anatuhumiwa kwa ufisadi. Ndo ije kwetu huku madongo kuinama tuwe na wanasiasa wasafi?

Topic yako ya leo imekuzidi uwezo.
 
Hili la katiba umeshakua wimbo uliokosa kiitikio
Sababu ni hata vyama vya upinzani Tanzania vinakosea step sana ndiyo maana katiba inashindikana ...kwanza hata wakiandika katiba, awana uwezo wa kujua katiba sahihi inatakiwa kuwa vipi na kuwa na nini ...mfano katiba mpya ya Kenya ni mbovu kwa asilimia 70% japo ni bora kuliko yetu ..sasa hiyo 70% iliyo lose kosekana ndani ya katiba ya Kenya ni ngumu watu kuitambua ..isipokuwa watu wenye akili kubwa sana...
 
SAFI umenyookaπŸ˜€
 
Aisee una hoja
Lakini sasa tufanyeni ili ahuweni kwa wale wanaolalamika kila siku

Ambao mi nadhani hata wao wakipata hizo nafasi watafanya hivyo hivyo
Kumaliza hili tatizo moja kwa moja ni ngumu, Cha kufanya ni kutunga sheria zitakazosimamiwa ipasavyo zitakazowabana wanasiasa na kuwaondolea baadhi ya privilege walizonazo, kuhakikisha biashara zote zinazosimamiwa au kuhusishwa na wafanyabiashara zinafuatiliwa kwa umakini kuhakikisha hakuna favorite yoyote kuanzia tax evasion nk, na kuundwa mahakama maalumu ya kushughulikia wanasiasa wanaotumia vyeo au nyadhifa zao kwa maslahi yao binafsi, pia kuwe na mfumo ambao utawapa nguvu wananchi kuanzia kwenye boksi la kura na uwezo wa kuwawajibisha wote waliowachagua kuanzia mbunge hadi rais kwa kuwa na vote of no confidence ambayo inaweza kumuondoa mbunge au rais madarakani ili wanasiasa wasiwe miungu watu bali watumishi wa watu.

NB: inaweza kupunguza kwa kiasi chake kujinufaisha kwa mgongo wa siasa hapa katiba bora ni muhimu
 
Mkuu,
Sikupingi lakini lolote linawezekana kama alikuwa na biashara, mashamba, hisa au uwekezaji mwingine kabla ya kuingia kwenye uongozi, si jambo la kushangaza kuona mali zake zikiongezeka kadiri muda unavyokwenda.

Si kila utajiri wa kiongozi ni wa rushwa, lakini pia si kila utajiri wa kiongozi unapaswa kukubaliwa bila kuulizwa maswali.

Kinachopaswa kuangaliwa ni uwiano kati ya mapato yake halali, muda aliokuwa madarakani na ongezeko la mali zake.
Kwa hiyo, si kosa kwa kiongozi kutajirika akiwa madarakani ikiwa utajiri huo unatokana na shughuli halali na unaweza kuelezwa kwa uwazi. Lakini ni jambo la msingi kwa jamii kuendelea kuhoji na kudai uwajibikaji pale ambapo ongezeko la utajiri linaonekana kutolingana na vyanzo vinavyojulikana vya mapato. Huo nao ni sehemu ya uwajibikaji katika utumishi wa umma.
 
Kwanza inafaa ujue ni mwanasiasa kwa muda gani. Aghalabu kwa yule anayeingia siasani kwa mara ya kwanza huwa ni wa kawaida tuu kwani hajausoma mchezo. huyu mawazo na akili zake hujikita kwenye mshahara na marupurupu mengine halali.
Lakini akiwa ni mwanasiasa anayeendelea i.e. amekuwa mwanasiasa kwa muda mrefu, huyo ameshajua "game" linachezwaje. Atajitahidi kuingia kwenye kamati mbalimbali, kujihusisha na misafara ya wakubwa, kufanya lobbying na wakuu wa Idara, kuibua hoja za ufuatiliaji miradi ya maendeleo n.k. n.k.
Ikitokea/zikibainika hoja za kero ya matumizi mabaya ya Fedha yy anajua mhusika na anajitokeza "kumsaidia" ila Asante ni muhimu.
 
Topic yangu haijanizidi uwezo
Ila Topic yangu imekuzidi uwezo wewe πŸ“Œ

Wewe kukosa cha kuchangia chenye mantiki hainamana Topic yangu imenizidi
Unachekesha mkuuπŸ˜…πŸ˜…
 
Ahaa asante sana mkuu
 
Hata sheria zikitungwa namna gani, hakuna mahali tutafika kwa mentality ya watanzania wa kizazi hiki. Niambie nani mzalendo anaweza kusimama kwa ajili ya nchi yake sasa hivi, binafsi simuoni. Leo hii ukipewa nasafi fulani, hata ukurugenzi tu au ukuu wa wilaya, utataka kujineemesha wewe na watu wako, na hiyo ni kwa mtanzania yoyote wa kizazi hiki.
 
Mapendekezo yako mazuri asante kwa maoni yako mkuu
 
Hili nalo ni tatizo kwa kweli, Leo unawezekana kuwa shujaa nje ya mfumo ila ukiingia ndipo imani na misimamo yako inapojaribiwa
 
Kwahiyo hapa unataka kusema kila mwanasiasa ni fisadi si ndio?
 
Hili nalo ni tatizo kwa kweli, Leo unawezekana kuwa shujaa nje ya mfumo ila ukiingia ndipo imani na misimamo yako inapojaribiwa
Yes, wengi tunaongea kwa vile tupo nje ya mfumo. Tukiingia midomo inajaa mafuta tu dadeq! Halafu tunanyamaza kama hatujui vile, hii nchi uzalendo ni somo la kufundishwa from grassroots.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…