Je Kindamba ni mtu sahihi UDART? Ana exposure yoyote kuhusu sekta ya usafirishaji?

Je Kindamba ni mtu sahihi UDART? Ana exposure yoyote kuhusu sekta ya usafirishaji?

Mkuu Kindamba kabla ya kuwa mkuu wamkoa nadhani aliwahi kuwa director kwenye private sector sikumbuki ni wapi Ila naamini ni MTU sahihi ingawa dart ni janga it's a sinking ship
Alikuwa Boss wa TTCL
 
Matukio ya ajali nyingi za mwendokasi zinazosababisha hasara kubwa. Pia serikali ya mkoa iweke sheria kali za bodaboda, bajaj wasiwe sababu nyingine ya ziada kuchelewesha malengo ya CEO Waziri Waziri Kindamba

View: https://m.youtube.com/shorts/bQxcULYHr5Q

Moja ya majukumu ya CEO nikuhakikisha safe operation, kutimiza hilo ni pamoja na kuhakikisha safe passage kwenye hiyo njia ya mwendokasi, nini afanye? ( Yeye ndio CEO sasa, akae chini na watu wake watoe alternatives).
Skills za hao madereva ziwe reviewed ni kama wengi ni kamlete.
Operation manager wake awe anafanya risk assessment za hizo barabara mara Kwa mara na kushare na hao madereva ikiwepo daily briefing Kwa Kila shift mpya.

Mambo ni mengi, Mr CEO anapaswa kuonyesha umahili wake Sasa, ndio maana tunazungumzia exposure kwenye hizi positions tena iwe international exposure.
 
Waziri Kindamba ni total failure. Yule ni kada tu wa CCM hakuna anachoweza. Hiyo kazi ni mzigo mkubwa kwake, kiufupi ndiya anakwenda kuitumbukiza kaburini mazima.
 
Mnawaweka wanasiasa kuongoza mashirika ya kibiashara 😄
Nchi hii inachekesha kwerikweri

Ova
 
Tatizo la mamlaka za uteuzi zimekaa kisanii sana!
Huyu mtu hana exposure yoyote ktk fani ya usafiri lkn teuzi zinafanyika kisiasa badala ya kuweka mbele taaluma ili tuweze kutoka hapa tulipo.
Aliyeondolewa ana taaluma ila ni msanii na huwa hawezi ku-deliver kitu kabisa zaidi kuishi kwa vitisho na kutishia walio chini yake!

Hakuna jipya UDART litakalotokea chini ya kindamba , nimekaa pale
 
Katika kipindi cha uongozi wake ndio kipindi kilichoongoza kwa wataalamu mbali mbali kuondoka TTCL baada ya kuona shirika limegeuka kuwa brothel (danguro) ambapo binti ukiwa mrembo unateuliwa kuwa manager, huku wataalamu wakiwekwa pembeni bila ya kusikilizwa na utaalamu wao
Nchi ya vutuko sana hii mkuu! 🤣 🤣
Anyway, ndio sera pendwa za ccm
 
Mradi wa DART umepewa mkurugenzi mpya ambaye ni Kindammba. Kwa utendaji wa Kindammba kama mkuu wa mkoa sidhani kama huyu ni kiongozi wa nafasi za kitaalamu kama makampuni.

Najiuliza baraza la mawaziri lililokaa wiki hii na kumpitisha lilijishauri vyema au lilitumia influence ya kiongozi mkuu kumpitisha?

Kwanini Tanzania tunaogopa kuzishindanisha hizi nafasi watu waombe? Nakumbuka Nehemia Mchechu aliwahi kushauri nafasi za wakuu wa mashirika ziwe zinaombwa badala ya kuwa na nafasi za uteuzi ila mfumo ulimpinga vikali.

Huyu Kindammba siyo mtu wakupewa shirika lililokufa kwasababu yeye mwenyewe ni tegemezi wa fikra na hajawahi kuwa mtu wakuchukua hatua pale anapoona ubadhirifu.
Ndo upuuzi wa hii nchi! Aisee inakasirisha..
 
Kuna Dart na Udart,Kindamba ni mkurugenzi wa Udart mkurugenzi wa Dart ni Athuman Kihamia.
Kindamba amechukua nafasi ya Gilliard Ngewe na Athuman Kihamia aliteuliwa Januari 11,2024 kuchukua nafasi ya Dk. Edwin Mhede.
UDART ni Kampuni ya mabasi yaendayo haraka na DART ni Wakala wa mabasi yaendayo haraka.
Nb: Sijajua kiundani tofauti na mipaka ya shughuli zao au nani anawajibika kwa mwenzake.
DART wanamiliki njia na miundombinu yake kama vituo na ofisi UDART wanamiliki magari na wafanyakazi wake, kimsingi DART anamkodisha UDART njia.
 
DKT. ATHUMAN KIHAMIA
Athuman Kihamia photo

Dkt. Athuman Kihamia​

Mtendaji Mkuu DART (UDART)
DART na UDART ni taasisi mbili tofauti na kila moja ina Mtendaji mkuu wake,sijui kwanini zilifanywa tofauti wakati zote ni za serikali!
 
Kuna Dart na Udart,Kindamba ni mkurugenzi wa Udart mkurugenzi wa Dart ni Athuman Kihamia.
Kindamba amechukua nafasi ya Gilliard Ngewe na Athuman Kihamia aliteuliwa Januari 11,2024 kuchukua nafasi ya Dk. Edwin Mhede.
UDART ni Kampuni ya mabasi yaendayo haraka na DART ni Wakala wa mabasi yaendayo haraka.
Nb: Sijajua kiundani tofauti na mipaka ya shughuli zao au nani anawajibika kwa mwenzake.
Ulichosemw ni kweli kabisa. Lakini mambo yanachanganya haya.
 
Kutoka kuwa Rc mpaka kuwa mkurugenzi Udart hii ni demotion bila shaka. Anywa Kindamba atapaweza Udart.
 
Ukiona mtu ameenda nje ya nchi ukubwani akaishi huko miaka kadhaa baada ya kurudi anapewa kazi serikalini kwenye taasisi yao akiboronga anarudishwa serikalini kama mkuu wa mkoa elewa huyo mtu wao.

Kuna tofauti kati ya Kindamba na watu kama Mhongo, Matindi na Mataragio. Hao watatu walirudishwa kwa sababu ya utaalamu wao ukitolewa kwenye majukumu waliyoikutia, serikali aina shughuli na wewe tena.

Kindamba system so tegemea kumuona popote serikalini kwa miaka mingi sana either ana skills za hiyo nafasi wanayompa au la.
 
Kuna Dart na Udart,Kindamba ni mkurugenzi wa Udart mkurugenzi wa Dart ni Athuman Kihamia.
Kindamba amechukua nafasi ya Gilliard Ngewe na Athuman Kihamia aliteuliwa Januari 11,2024 kuchukua nafasi ya Dk. Edwin Mhede.
UDART ni Kampuni ya mabasi yaendayo haraka na DART ni Wakala wa mabasi yaendayo haraka.
Nb: Sijajua kiundani tofauti na mipaka ya shughuli zao au nani anawajibika kwa mwenzake.
TOFAUTI YA DART NA UDART
DART ni taasisi ya serikali yenye hadhi ya wakala kama alivyo TANROADS, REA, TEMESA, nk na kirefu chake ni Dar es Salaam Rapid Transit Agency au Wakala wa Usafiri wa Haraka Dar es salaam.
Taasisi hii imeundwa kwa mujibu wa tangazo la serikali No. 120 la tarehe 25 Mei 2007 chini ya sheria No. 30 ya Wakala za Serikali ya mwaka 1997 na marekebisho yake. Jukumu kuu la DART ni kuanzisha na kuendesha mfumo wa Usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka kwa jiji la Dar es Salaam. Wakala inakusudia kufikia malengo yafuatayo:
a)Kuanzisha na kuendesha mfumo wa Mabasi Yaendayo Haraka kwaaajili ya Dar es Salaam, yatakayotumia jina la DART;
b)Kuhakikisha mtiririko bora wa usafiri kwenye mitaa na barabaraza mjini, na
c)Kuhakikisha usimamizi wa wakala wenye ufanisi.
Na Je, UDART ni nini?
UDART ni kampuni binafsi inayoendesha magari yaendayo haraka, kirefu chake ni USAFIRI DAR ES SALAAM RAPID TRANSIT. Huyu sasa ndio anatoa huduma na yale mabasi yake yanayoonekana barabarani. Na kama nilivyosema hapo juu, msimamizi mkuu wa usafiri wenyewe. Hivyo UDART hawezi kufanya lolote mule nje ya mkataba au maelekezo bila kupata idhini ya DART. Na hata ikitokea mkataba wa UDART umekwisha DART ndiyo anashughulika na kuandaa tenda ili kumpata mtoa huduma mwingine.
Nadhani kwa ufupi utakuwa umeelewa tofauti ya taasisi hizi mbili.
 
Ukiona mtu ameenda nje ya nchi ukubwani akaishi huko miaka kadhaa baada ya kurudi anapewa kazi serikalini kwenye taasisi yao akiboronga anarudishwa serikalini kama mkuu wa mkoa elewa huyo mtu wao.

Kuna tofauti kati ya Kindamba na watu kama Mhongo, Matindi na Mataragio. Hao watatu walirudishwa kwa sababu ya utaalamu wao ukitolewa kwenye majukumu waliyoikutia, serikali aina shughuli na wewe tena.

Kindamba system so tegemea kumuona popote serikalini kwa miaka mingi sana either ana skills za hiyo nafasi wanayompa au la.
Kindamba hana skills zozote tusidanganyane hapa. Sema ana mtu wake kwenye mfumo tu ambaye anamsemea kwa wateuzi. Kindamba kabla ya kwenda TTCL alikuwa bank officer DTB TRUST Bank.

He is nothing but a lucky mediocre performer
 
Tatizo la mamlaka za uteuzi zimekaa kisanii sana!
Huyu mtu hana exposure yoyote ktk fani ya usafiri lkn teuzi zinafanyika kisiasa badala ya kuweka mbele taaluma ili tuweze kutoka hapa tulipo.
Aliyeondolewa ana taaluma ila ni msanii na huwa hawezi ku-deliver kitu kabisa zaidi kuishi kwa vitisho na kutishia walio chini yake!

Hakuna jipya UDART litakalotokea chini ya kindamba , nimekaa pale
Kuweka Wanasiasa kwenye nafasi za kiutendaji ni utamaduni wa CCM wa tangu enzi na enzi, hata kwenye Mashirika ya Umma au viwandani miaka ya nyuma kulikuwa na watu walioitwa Political Commissar ambao ndio walikuwa mabosi kwenye viwanda badala ya kuweka Wahandisi wa Mitambo. Ndio maana viwanda vyote vilikufa kibudu
 
Ukiona mtu ameenda nje ya nchi ukubwani akaishi huko miaka kadhaa baada ya kurudi anapewa kazi serikalini kwenye taasisi yao akiboronga anarudishwa serikalini kama mkuu wa mkoa elewa huyo mtu wao.

Kuna tofauti kati ya Kindamba na watu kama Mhongo, Matindi na Mataragio. Hao watatu walirudishwa kwa sababu ya utaalamu wao ukitolewa kwenye majukumu waliyoikutia, serikali aina shughuli na wewe tena.

Kindamba system so tegemea kumuona popote serikalini kwa miaka mingi sana either ana skills za hiyo nafasi wanayompa au la.
Kazi Maalumu yule jamaa kama Athuman Kihamia pia maana jamaa alitumika sana pale NEC kuvuruga matokeo ya uchaguzi!
 
Back
Top Bottom