TOFAUTI YA DART NA UDART
DART ni taasisi ya serikali yenye hadhi ya wakala kama alivyo TANROADS, REA, TEMESA, nk na kirefu chake ni Dar es Salaam Rapid Transit Agency au Wakala wa Usafiri wa Haraka Dar es salaam.
Taasisi hii imeundwa kwa mujibu wa tangazo la serikali No. 120 la tarehe 25 Mei 2007 chini ya sheria No. 30 ya Wakala za Serikali ya mwaka 1997 na marekebisho yake. Jukumu kuu la DART ni kuanzisha na kuendesha mfumo wa Usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka kwa jiji la Dar es Salaam. Wakala inakusudia kufikia malengo yafuatayo:
a)Kuanzisha na kuendesha mfumo wa Mabasi Yaendayo Haraka kwaaajili ya Dar es Salaam, yatakayotumia jina la DART;
b)Kuhakikisha mtiririko bora wa usafiri kwenye mitaa na barabaraza mjini, na
c)Kuhakikisha usimamizi wa wakala wenye ufanisi.
Na Je, UDART ni nini?
UDART ni kampuni binafsi inayoendesha magari yaendayo haraka, kirefu chake ni USAFIRI DAR ES SALAAM RAPID TRANSIT. Huyu sasa ndio anatoa huduma na yale mabasi yake yanayoonekana barabarani. Na kama nilivyosema hapo juu, msimamizi mkuu wa usafiri wenyewe. Hivyo UDART hawezi kufanya lolote mule nje ya mkataba au maelekezo bila kupata idhini ya DART. Na hata ikitokea mkataba wa UDART umekwisha DART ndiyo anashughulika na kuandaa tenda ili kumpata mtoa huduma mwingine.
Nadhani kwa ufupi utakuwa umeelewa tofauti ya taasisi hizi mbili.