Je, kitu gani ni hatari lakini watu wengi wanakichukulia poa?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
Kuna vitu vingi katika maisha yetu ambavyo vina hatari kubwa, lakini tunavichukulia poa tu na maisha yanasonga bila kufikiria athari zake. Ukija kushtuka huwezi kurudi kunyuma, na ukibahatika kunyanyuka basi unakuwa umepoteza pakubwa.

Mfano kula vitu ovyo ovyo, tunajua tunajaza sumu kibao mwilini, na tunajitafutia magonjwa kwa shangwe zote, lakini hatujali wala nini, mpaka yatufike! Eti tunajipa moyo mbinguni tutapata mili mipya😂😅😅.

Kwenu Wakuu, kitu gani ni hatari lakini kila mtu anachukulia poa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…