Je, kufanya mapenzi na kukojoa nje kwa Wanaume hupunguza nguvu za Kiume?

Je, kufanya mapenzi na kukojoa nje kwa Wanaume hupunguza nguvu za Kiume?

Mimi nilikuwa na wasiwasi labda inaweza kuwa ni sehemu ya punyeto kumbe haina madhara.
Haina tatizo watakuja wataalam hapa wakuambie sio salama ili umlishe ile midawa yao apate kansa au aanze kuvimba tumbo ndo raha yao hiyo
 
MziziMkavu,
Mkuu
Hebu rudia upya swali la mleta mada,
Kifupi anauliza kama kukojoa nje kuna athiri nguvu za kiume,
Hilo ndo swali la msingi,
Hayo mengine ni mbwembwe tu za kukoleza swali,
 
Maisha yangu yooote nimeishi kwa kukwepa kudungisha mimba kwa njia hii, Nnachofanya nikikojoa nje Naenda maliwato nakojoa mkojo wa kawaida kuflush mabaki ya shahawa na nnajua mkojo huharibu mbegu zinazoweza kuwa kwenye njia,halafu narudi kuendekeza kazi,
Na sijawahi pungukiwa nguvu kabisa,

Sijui labda ni maumbile
 
alexmahone,
Ulichoongea ni mtazamo wako binafsi siyo ukweli wa mambo,kuna muda wa mbegu kutoka na kuna ute lainishi,ni vitu tofauti,sema baada ya kukojoa mabaki ya shahawa yanaweza baki kwenye njia Na ili kuziondoa kabla ya kurudia nenda kakojoe mkoja kuua mabaki ya shahawa
 
Zaidi ya alichosema Alexmahone ukikojoa nje duct ya penis hubaki na mbegu hivyo unaporudia tendo mbegu mabaki huingia moja kwa moja nakutunga mimba. Kukojoa nje haisaidii kabisa . In fact umekuwa ukifanya on safe days.
Baada ya kukojoa nje usiichomeke kabla ya kwenda kukojoa mkojo huua mabaki ya mbegu katika njia,
 
Wakuu shukrani kwa kuchangia japo najua kuna utata bado wa nguvu za kiume unapokojoa nje. Najua wataalam wengine nao watakuja kutujuza vizuri maana wengi twatumia style huenda kwa kutojua chochote.
Mimi naomba nijibu kwa uzoefu, ni kweli kukojoa nje kunapunguza nguvu za kiume kwa sababu, unatoa nje uume wenye nguvu na kwa kasi inayokuwa nayo unalazimika kuukandamiza mapajani au juu ya kinena cha mwanamke.

Kitendo hiki kinalazimisha uume kujikunja kwa nguvu na hivyo kuikunja mishipa ya uume ambayo inatakiwa kuwa imenyooka wakati wote Wa tendo. Kujikunja huku kwa kulazimishwa kunaathiri nguvu ya kukunjuka na hivyo taratibu na baada ya muda kusimama kwa uume kunashuka kiwango.
 
Maisha yangu yooote nimeishi kwa kukwepa kudungisha mimba kwa njia hii,
Nnachofanya nikikojoa nje Naenda maliwato nakojoa mkojo wa kawaida kuflush mabaki ya shahawa na nnajua mkojo huharibu mbegu zinazoweza kuwa kwenye njia,halafu narudi kuendekeza kazi,
Na sijawahi pungukiwa nguvu kabisa,
Sijui labda ni maumbile
Hio ni contraceptive method kwa kumbukumbu zangu hafifu katika somo la biology tuliita ni withdrawal method. Nadhani ndio njia sahihi na salama zaidi ya kuepuka matatizo ya mimba zosizotarajiwa.
 
mmmh wewe jasiri sana kijana wengine wakiingia tu ni kumwaga
utadhani ametumwa kuja kumwaga huko hata dakika moja hamalizi ...sijui watu wengine wapoje ningekupata ungenifaa sana
kama ndivyo ulivyoumbika hivo hata sekunde 15 ni nyingi mno
 
Hakuna ukweli wowote ktk hili maana kuna couple nyingi sana zinatumia njia hii kupanga uzazi maana ni salama zaidi kuliko masindano, kitanza au vidonge.
 
Kumwaga nje? Sitaki kusikia huo mchezo. Bora nitumie condom.
ha ha ha ha ha ha
hiyo siku huyo mwanamke atajuta nikimvalia mpira maana bao la kwanza ni mpaka dakika 90 ziishe na extra time ndio tunahesabu la kwanza
nikirudia la pili nasi nazimiwa simu hata wiki mbili
acha tujinafasi bana😀😀😀😀
 
Mimi naomba nijibu kwa uzoefu, ni kweli kukojoa nje kunapunguza nguvu za kiume kwa sababu, unatoa nje uume wenye nguvu na kwa kasi inayokuwa nayo unalazimika kuukandamiza mapajani au juu ya kinena cha mwanamke. Kitendo hiki kinalazimisha uume kujikunja kwa nguvu na hivyo kuikunja mishipa ya uume ambayo inatakiwa kuwa imenyooka wakati wote Wa tendo. Kujikunja huku kwa kulazimishwa kunaathiri nguvu ya kukunjuka na hivyo taratibu na baada ya muda kusimama kwa uume kunashuka kiwango.


Noted
Ama Tuzae Tu Elimu Bure Sasa Hivi
Mkuu Unaweza Kujikuta Unazaa Watoto Wengi Sana Kwa Muda Mfupi
 
Kennedy, Huwezi kuizuia mimba kwa kukojolea nje unajidanganya. Kama wewe ni mwanaume unayezalisha hata tone moja tu la manii linamvimbisha mtu wakati ukishakojoa na kuendelea na mapenzi manii huendelea kuvuja ukeni sasa hiyo formula kakudanganya nani.

Mwanamke akiwa kwenye joto la mimba hata ukikojoa chini akazichota na kidole akaingiza ukeni anabeba mimba. Msicheze na manii za mwanaume mzima ni zaidi ya mabomu ya Kim.
Zipo njia za kuzuia kubeba mimba za kisasa na za kienyeji na kila moja ina madhara yake.

1.uzazi wa mpango.
i. Kalenda;hii ni nzuri kwa wasomi sana na ikiwa mzunguko wa mwanamke ni sawa haubadiliki ovyo.
Ni rahisi kubeba mimba hasa ukisahau au ukiugua ghafla tarehe zikachange.
Ni nzuri pia kwa kuwa kiafya utakuwa salama.

ii. Pills, sindano na vitanzi.
Zinafaa kwa wote wasomi na wasio wasomi pia husaidia kuondoa hofu kwa wazazi.
Husogeza kuzazi mbali kiasi kwamba mtu aweza acha kutumia ili azae na akashindwa kubeba mimba.
Hutungisha mauvimbe mwilini na kuleta kansa kadhaa mwilini ikiwa zimekutana na mpambano mwingine mwilini.
Nchi nyingi za ulaya huzalisha dawa hizi kama sehemu yao ya biashara na nchi nyingine zimepigwa marufuku kwa sababu za kiimani kidini au kiafya.

2.za asili.
i. Mitishamba.
Kuna imani kuwa mwanamke akishazaa hutumia baadhi ya mizizi ili kuzuia mimba. Hii haiko biologically sana kwa kuwa tafiti kamili hazijathibitika.

ii. Damu ya hedhi.
Matumizi ya damu ya hedhi ya awali ya mwanamke yanayowekwa pamoja na mizizi kadhaa ya mti unaoteleza kisha kuwekwa ktk tete na kufungwa juu na gundi ya nyuki ambapo mlengwa huamua kuficha kwa kufukia ardhini mahali atakapokumbuka au kuficha ajuavyo. Dawa hii huenda na manuizi.
Humhakikishia kutobeba mimba vyovyote iwavyo.
Madhara yake ni kwamba kuna wengine husahau alipofukia pindi atakapohitaji kupasua au kufunua ili abebe mimba na hivyo kuishia na idadi ya watoto alionao.

Mazingira aliyoficha mfano kufukiwa yaweza kuharibiwa bila yeye kujua na kujikuta kabeba mimba ikiwa kalikatwa alipoweka.

Ni mbinu inayoaminika sana japo haina biological facts sana zaidi ya kuonekana kama uchawi.
Asilimia kubwa ya watu wameshindwa kuzaa kubeba mimba kwa kuwa tu walishindwa kutunza nguo zao za bridi wakiwa mabinti hivyo kuchukuliwa na watu wabaya. Makabila yote huhimiza mtoto wa kike kuficha bridi yake nadhani siri yake ni hapo hapo.

Zipo mila ambazo zaweza kuwa dhambi na zile zisizo dhambi kwa MUNGU. Naomba nisifafanuliwe vibaya au kuonekana tofauti kwa ufafanuzi huu.

Mtu aliyeabudu dini zote anaujua ukweli zaidi kuliko aliyeabudu ktk dini moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom