Je, kuna mbunge yeyote wa upinzani atarudi Bungeni 2020?

Je, kuna mbunge yeyote wa upinzani atarudi Bungeni 2020?

Jamani wananchi gharama zimepanda za maisha. Kuchukua majimbo ya kina Mbowe bado kutazaa ufisadi wa kutisha. Anhalau hao kina Mbowe wanasema na kutaja madhambi yanayofanyika, mkiwatoa mjue mtapelekeshwa na kubebeshwa gharama zisizo zenu. Haya\endeleeni
 
Ndivyo ilivyo, hatutaki wabunge wa Upinzani warudi Bungeni. Kama yule wa Ukerewe, kila siku kutuonya tuu kivuko kibovu, kivuko kibovu mpaka kimepinduka kabisa. Badala ya kuunga mkono juhudi yeye anakisemea kivuko, kwani ccm ndio malaika mzuia ajali? Hawarudi!
 
Wakuu,ninaendelea kutafakari juu ya siasa za hapa Tanzania kutokana na uminywaji wa demokrasia.

Maana tumeshuhudia matokeo ya marudio ya uchaguz kwenye zile kata 43.Ambapo CCM ilishinda kata 42 na upinzani kata 1 pekee.

Hali hiyo inanifanya nitafakari juu ya hatma ya wabunge wa upinzani kwenye uchaguzi ujao wa mwaka 2020,je kuna yeyote atafanikiwa kutetea kiti chake? Na hata kama akitetea je,atatangazwa mshindi?

Karibuni kwa mawazo yenu.


Mkuu mie nafikiri kutakuwepo na wabunge wa upinzani ambao watakuwa ni wachache tu na wengi wao watakuwa ni "wabunge pandikizi" na hili litafanyika ili ku justify demokrasia yetu kwenye macho ya Dunia kama yalivyofanyika Mbeya
 
Wakuu,ninaendelea kutafakari juu ya siasa za hapa Tanzania kutokana na uminywaji wa demokrasia.

Maana tumeshuhudia matokeo ya marudio ya uchaguz kwenye zile kata 43.Ambapo CCM ilishinda kata 42 na upinzani kata 1 pekee.

Hali hiyo inanifanya nitafakari juu ya hatma ya wabunge wa upinzani kwenye uchaguzi ujao wa mwaka 2020,je kuna yeyote atafanikiwa kutetea kiti chake? Na hata kama akitetea je,atatangazwa mshindi?

Karibuni kwa mawazo yenu.
Jamaa yangu hawewezi kurudi kwa tume hii kwanza wapinzani wakweli hawashiriki uchaguzi unasimamawa na watu wa ccm niujinga kusimamiwa na mpinzani wako alafu utegemee ushindi tuliambiwa miaka mingi katiba hii si nzuri sikuakiingia rais dikteta hatuchomoki ndio tumeyaona kwatume hii wapinzani watakao shiriki ni vibaraka nakama watashiriki nitasema niwaongo sana huwa hawaibiwi kura wanashindwa Kialali tu
 
Kuna tofauti kati ya kufanya uchaguzi wa jimbo moja moja na ule wa nchi nzima ambao unafanyika at par (Wahe.Wabunge na Mhe.Rais).Huu wa jimbo moja,unakuta kubwa kundi la viongozi wa vyama vya siasa linajirundika sehemu moja kumpigia kampeni mtu mmoja.Wakati wa uchaguzi mkuu 2020 kumbuka kila mgombea ubunge atakuwa anajiuza mwenyewe kwenye jimbo lake na msaada mkubwa tu pale mgombea URAIS wa chama chake atakapopita mara moja (mara moja) kumuuza.Hakutakuwa na wabunge kutoka sehemu Fulani kuja kumsaidia huyu wa mahali Fulani.Kila mtu atakuwa anapambana na hali yake.Binafsi nasema lolote laweza kutokea.Attend voir-Mungu ibariki Tanzania
 
Ester matiko fanya hima kibatali kisije kukuzimikia.
 
kwa kauli ile sidhani 'ma-DED nimewapa magari, mishahara minono, wapinzani wakishinda sitowaelewa'
 
Nafikiri wabunge wa CUF ya profesa kina Sakaya wao watapeta, may be na some from ACT but wabunge wa Chadema hakuna atakae rudi; kwa mujibu wa mtazamo wangu!
 
Tumuombe ALLAH atujaalie uwezo wa kuitambua HAKI ili tuifuate na uwezo wa kiuitambua BATWIL ili tuiache
 
Hata Museven haamini kinachotokea Uganda, nini Joseph Kabila bhana....
 
Tushajiandaa sasa tunasubiria uchaguzi wa oct 14 mshinde ushindi wa kishindooooooooo
 
Chaguzi ndogo zilizofanyika zimetosha kutoa picha ya uchaguzi mkuu 2020. Kwa mtazamo wangu kwa yanayoendelea na yanayofanyika itakuwa ngumu sana mbunge wa upinzani kutoboa 2020 kama hawatafanya mabadiriko yanayohitajika
Kitendo cha wao tu kuwa wapinzani ni ishara tosha kuwa kisaikolojia wako sawa kabisa.

Issue ipo kwa wananchi. Ni nani atakua mkombozi wao?
 
Chaguzi ndogo zilizofanyika zimetosha kutoa picha ya uchaguzi mkuu 2020. Kwa mtazamo wangu kwa yanayoendelea na yanayofanyika itakuwa ngumu sana mbunge wa upinzani kutoboa 2020 kama hawatafanya mabadiriko yanayohitajika
Wabunge wanaweza wasirudi lakini Wananchi wakaendelea kubaki kuishi Itikadi ya hivyo vyama pinzani

Na wakati huohuo ubabe una umri muda wake hata Farao alikuwa na wakati wake na kama una wakati wake yatosha kusema Wananchi wanaona pia wanajua na kama hayo yote yako hivyo wataendelea kuziishi Itikadi kwa ajili ya jambo muda

Misimamo ya watu ikiheahimiwa italeta umoja wa kitaifa pasipo mgawanyiko
 
Back
Top Bottom