Je, kuna Mkazi yeyote yule wa Jimbo la Kawe aliyeanza kuzishuhudia ahadi lukuki za maendeleo za Mbunge Askofu Gwajima?

Je, kuna Mkazi yeyote yule wa Jimbo la Kawe aliyeanza kuzishuhudia ahadi lukuki za maendeleo za Mbunge Askofu Gwajima?

ka aliahidi na hafanyi ..huenda ata pale madhabahuni hujinenea moyonii
"wajinga ndo waliwaoo"
 
Huyu jamaa aliwahi kuhojiwa kuhusu maendeleo ya kawe 'akasema maendeleo sio lazima yawe ya kuonekana mana yeye bado anawatembelea watu kujua shida zao'
 
Nikiwa kama Mmoja wa Wavuvi wa Ununio nimeshaandaa Siku nyingi sana Picha zangu 4 za Passport kwa ajili ya Pasi ya Kusafiria ili anikatie VIZA na Mbunge Askofu Gwajima atupeleke nchini Marekani kama alivyotuahidi na kutuhakikishia pia.

Askofu Gwajima USA unatupeleka lini?
Kwa hivo kabisa Krav nawewe uliafiki kuamini kabisa maneno hayo kutoka kwenye kinywa cha anayejiita mwanasiasa akisaka tonge?

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Huyu mh. Mbunge wa kawe watu wanamtafuta Kawe sokoni aliahidi ujenzi wa soko na barabara kuelekea kanisa la KKKT lakini wapi hata kupita kusalimia haonekani nadhani ataonekana tena 2025.

Watu wa Makonde Kwenye shule karibu nne wanamtafuta awaeleze ni kwanini Lami iliishia Shopperz tu ilihali nao ni walipakodi wazuri lakini lami haikuendelea mpaka makonde haonekani. Watu wamtafuta wamuulize ni kwanini Lami inaelekea kwa Lukuvi na Chibu dangote lakinj mitaa yenye mabepari ya kina Temu lami haikupigwa na ndio walipa kodi wakubwa haonekani

Ccm mlikosea sana kumsimika huyu mchunga kondoo wa bwana kwani jimbo lake watu wanamuulizia na barua,email wanamtumia mheshimiwa vipi vyuo vya uvuvi, miundombinu mbona kimya hata greda la manispaa lipite tuu lichonge barabara yeye kajichimbia Dar au dodoma . Mh mtume hata Metuselah aje aseme na wananchi wenyeviti wanafunga ofisi wanaogopa maswali magumu.
Duh
 
Nikiwa kama Mmoja wa Wavuvi wa Ununio nimeshaandaa Siku nyingi sana Picha zangu 4 za Passport kwa ajili ya Pasi ya Kusafiria ili anikatie VIZA na Mbunge Askofu Gwajima atupeleke nchini Marekani kama alivyotuahidi na kutuhakikishia pia.

Askofu Gwajima USA unatupeleka lini?
Ukimuamini Askofu Rashid Gwajima utaamini kuwa Afghanistan iko Latin America.
 
Askofu Gwajima, katika ahadi zako ulituhaidi vijana wa kawe kuwa utatupeleka jimbo la Birminghama Marekani ili tukabadilishane ujuzi na vijana wa huko kwaajili ya manufaa ya kawe,

vile vile mbali na hilo ulituhaidi kutupatia chuo cha uvuvi,

sasa tunaona siku zinaenda tu umekalia kisabengo kushadadia vitu usivyokua hata na ujuzi navyo,

tunaomba utupe tamko vijana wako wa kawe tuendelee kujiandaa, ni lini hasa safari ya Birmingham itakua tayari
FB_IMG_16285171716045313.jpg
 
Tafuta hela mkuu mawazo yabadilike..uanze kuwaza mambo mengineyo
 
Oyaaa panga nguo kabisa safari imeiva, muda wowote vijana wa jimbo la ufufuo na uzima mnaondoka ....
 
Back
Top Bottom