Ki ukweli tunajua ni mtu smart kichwani hata kipindi anatolewa ile issue ya Covid ya kwanza tulisikitika sana sababu tulijua alisimamia uweledi wake.
Alivyopewa Wizara hii inayogusa maisha yetu tukajua YES Wizara kapewa mjanja kumbe salaleeeee hizi pigo mbili tu za week hii ni hatari sana,first ile ya kuwaruhusu kampuni za simu kupiga hadi 9000 kwa gb 1 (alidai atapunguza bei za bundles kumbe kavurunda hatari).
Pili ni mambo ya whatsap call,dah Lord have mercy on us,these are the same people wanaotembelea ma v 8 na kutuambia tujiajiri,ukijaribu kujiajiri kwa kutumia teknolojia hii ya internet anatokea waziri na mipango ya kuweka vikwazo vya ajabu ajabu
Kwani mnataka kutengeneza jeshi la aina gani la ma jobless,jamani kama ni FRUSTRATIONS zimetoisha ,MMESHINDA NAMBA ZINASOMEKA HADI WATU WANACHANGANYIKIWA tuacheni tupumue basi..WE CANT BREATHE
Yaani hata kuingia YouTube kuangalia comedy clips kucheka nayo ishindikane?kuongea na mtu wa abroad via whatsapp call kuna watu roho inawauma?au ni chanzo cha mapato?
Imagine hii nchi hata PAYPAL hairuhusiwi hapo ndipo ninapowaonega wivu wakenya kwenye issues hizi za teknolojia BAADA YA VURUGU ZOTE HIZI UTASIKIA VIJANA WA IT WA TANZANIA MMELALA SANA JIAJIRINI
SO FAR NDIYE WAZIRI AMBAYE WANANCHI WAMESHINDWA KUMUELEWA HASWA WA MTANDAONI WANAMUONA KAMA ANA NIA OVU YA KUWAFANYA WASIWEZE HATA GHARAMA ZA KU SURF