Je, kuna mtu yeyote aliyewahi kushuhudia na kuthibitisha uchawi? Njoo tuongee hapa!

Waganga hao hao walioshindwa kujua ugonjwa wa ukimwi ni nini nakusema watu wamelogwa na kutupiwa majini au waganga wapi mkuu?

Uzuri mmoja hizo experience zote nimezipitia
 
Mungu hawezi tengeneza kitu ili kimsumbue .

Yaani hai make sense kuwa Mungu ndo ana hold power ya Kila kitu then amuumbe shetani ili awe mpinzani wake

MTU mjinga pekee ndo atakuwa anamkemea shetani adui wa kubuni
Jibu swali nililo kuuliza kijana.

Usilete mambo ya Shetani na kumzulia Mungu uongo. Nani amekwambia ya kuwa Mungu anashindana na Shetani au Shetani amemshinda Mungu ?

Nataka uthibitishe nilichokuuliza usihamishe mada. Shida yenu mnaandika mambo msiyo kuwa na ujuzi wenu. Mkibanwa kidogo mnaruka ruka.
 
Tafuta mkuu , nishtue siku moja nije niruke
 
Hiv jf yote hii hakuna mchawi ajitokeze afanye demo moja ubishi uishe?

Ndugu zako hatutak ulogeke sana. Inabidi ajitokeze mwanamke mmoja wa JF akuloge. Uwe zuzu kabisa kwake. Tunakuacha miaka 2 ndio tunakuja kukuagua. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

sijui kaz hii nan ataiweza?.
Najua Seran atakuhurumia hurumia. Inabid tutafute mtu wa kazi
 
Sasa mkuu hata kama tajiri kwa imani yake anaamini katika mafanikio yake alifanikiwa uchawi pia umechangia unadhani atasema?
 
Ukisoma katika elimu mijadala suala la fasili ya mtu huwa lina mili kwa anayetoa fasili hiyo. Ndio maana huwa kuna marejeo ya kuhakiki hizo fasili.

Lakini msingi wa fasili ni kuwa fasili yoyote ya kitu fulani lazima izuie yote yasiyo husu hicho kitu kuingia na yaruhusu yale yote yahusuyo hicho kitu kuingia. Kwahiyo kutafautiana kwa maana si hoja ya kuwa kitu fulani hakipo. Zaidi ya hayo ndio maana huwa kuna kundi la watu hukubaliana juu ya maana fulani na hii huitwa Istalahi.

Ishu ya kupinga kuhusu nyeti inathibitisha vipi ya kuwa Uchawi haupo ?

Mangapi tumeyaona kwenye Sayansi ya uongo sio tu kwa uvumi bali ushahidi, je hii itathibitisha ya kuwa Sayansi haipo ?
 
Mkuu nikuambia mtaani kwetu kuna watu wananiita mchawi utaamini?
 
Labda kijijini kwao anavimba watu wanamuogopa ni mchawi
Hiv jf yote hii hakuna mchawi ajitokeze afanye demo moja ubishi uishe?

kila anayesema ni mtaalam hataki kueleza.

kuna sehemu jamaa kapiga mahindi mbolea, watu baadae wanakuja muuliza kaweka mbinu gani (ya kimazingira) wakatajiwa mbolea na mbegu nzuri mzuka umekata , wangeambiwa kuna mtaalamu wale watu wangepanda dau
 


Shetani hayupo na hajawahi kuwepo na hatokuwepo
 
Kama ulikuwa kipofu ukaenda kwa mganga ukaanza kuona, au ulikuwa kibogoyo ukaenda kwa mganga meno yakarudi au ulipata kazi serikalini ya mtu mwenye degree bila cheti au koneksheni baada kupewa dawa na mganga njoo tuongee kuhusu hiyo nguvu inayofanya vitu ambayo haielezeki.
 
Acha porojo na panic thibitisha uchawi upo na sio ujinga wako tu
Si umesema una mifano elfu moja. Tuwekee mitano tu. Hakuna porojo hapa, anaye kanusha huwa anatangulizwa kuthibitisha sababu hudhaniwa yeye ana elimu kubwa juu ya hilo kuliko anaye kiri.

Sasa usiletw utoto na kukimbia hoja ya msingi. Mnadai Uchawi haupo thibitisha hilo.

Uchawi unathibitishwa kwa mengi na kuanzia katika maana yake.
 
Shetani hayupo na hajawahi kuwepo na hatokuwepo
Naona unajifurahisha. Huenda Shetani humjui wala maana ya Shetani huijui.

Mkiwa mnaingia kwenye mijadala kama hii, hakikisheni mnakijua mnachokikanusha. Msiwe mnapotezea watu muda.

Hapa nimekuuliza swali dogo tu, tuthibitishie ya kuwa Shetani hayupo. Unashindwa.
 
Hiyo sio moro ?😁 nalima karibu na wazingua ukiwaona wanavyofanya utacheka sana, kuna ile miti ya mnyaa sijui kama unaijua , inakatwa inazungushwa kw3nye pembe za shamba, mimi nazingatia kanuni za kilimo , nikiwapiga bao utasikia usicheze na huyo mangi😁

Hakuna mtu anadhubutu kulisha mifugo kwenye mashamba yangu πŸ˜…πŸ˜…
 
Iki ndo kilichopo akili ya binadamu ni kubwa sana endapo MTU akiitumia ipasavyo anaweza kufanya mambo makubwa sana yasiyo elezeka .

Kule bukoba kwetu Babu yangu alikuwa anafanya kanuni za kilimo kama kutumia mbegu za kisasa mbolea na Kila mbegu mpya ikija anaiijaribu na kufata ushauri wa wataalamu .

Kilichotokea watu wakawa wanamtazama kama mfano na maafisa kilimo n.k shamba lake ndo lilikuwa likitumika kufundishia watu kilimo

Ila Kuna watu walikuwa wakiamini uchawi sikuona dawa zao kama zimewapa chochote

Shortly hauwezi ukafanikiwa kwa maombi Wala uchawi bila juhudi na kutumia akili vizuri

Jamii za watu duni ndo utawakuta wakiamini uchawi
 
Nikumbushe nilisema na mifano kuhusu nini
.uchawi unathibishwa weka hapa huo uthibitisho wako
 
Thibitisha kwanza wewe unayesema shetani yupo .

Mimi nasema hayupo kwakuwa haonekani.
 
Marekani kuna wachawi wale(wiccans) huwezi kuwafananisha na huku kwa sababu wale hawaamini uchawi kwa sababu ya kukosa elimu wapo katika jamii iliyoendelea.
Unajua kuwa Marekani wapo omba omba katika hiyo hiyo jamii iliyoendelea na niwazungu na wanaweza kukuomba mpaka wewe mmatumbi?
 
Zamani watu walikua wana amini magonjwa yanatokana na hewa chafu wanayoivuta( Miasma theory) na waliamin kwa mamia ya miaka.


Germ theory ikaja batilisha na kutoa sababu za magonjwa mbalimbali.
Yes, Like Cholera from Airborne to waterborne disease belief......

John Snow
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…