Je, kuna uhakika wa Mwigulu Nchemba kurudi Iramba?

Je, kuna uhakika wa Mwigulu Nchemba kurudi Iramba?

Baada ya kufuatilia kwa kina siasa za kimajimbo na kuangalia nyadhifa za kiwaziri nikagundua kuwa tangu kuanze kwa utawala wa kibunge ni Mbunge mmoja tu aliwahi kushika nafasi ya ubunge kwa miaka 2o Jimbo la Iramba - na hasa Iramba Magharibi ambaye ni aliyewahi kuwa Waziri wakati wa kipindi cha Mwinyi - yaani Nalaila Kiula. Huyu mzee kwa siku hizi sijawahi kumsikia tena ingawa kuna wakati niliwahi kumwona akishiriki katika Ibada Kanisa la Mchungaji Mama Rwakatare.

Je, Dkt. Mwigulu anaweza kufikia historia ya huyu Mzee kwenye ubunge katika jimbo hili ambalo watu wake hawapendi dharau na ni maskini jeuri? Kwa mwaka 2020 Mwigulu kiukweli kabisa na mimi nikiwa shahidi wa namna tulivyompitisha aliiba kura kuanzia zile za maoni kwani ni ukweli dhahiri bayana kuwa alishindwa kura hizo.
Hakuna maskini ambae ni jeuri


Watu wa huko iramba ni mapomole tu
 
Nimesoma na kutafakari andiko lako bilashaka unatamani Mwigulu Nchemba arudi tena Iramba na nikutoe shaka na kukurekebisha kwamba Mwigulu yupo Iramba na ndiye Mbunge halali wa Iramba ! Kurudi tena kivipi wakati ndiye Mbunge wa Iramba na wana Iramba wanafuraha kuwa na kiongozi kama yeye hapa pata kutokea kuwa na Waziri aliyeshika wizara Muhimu katika Nchi hii kutokea Iramba kama Mwigulu Nchi inamhitaji Mwigulu Nchemba sio Iramba tu ndugu !

Iramba kwa Mwigulu Nchemba ni njia tu kuelekea kuliongoza taifa letu la Tanzania kama afanyavyo sasa kuwa Waziri wa Fedha kwenye nyakati ngumu kama hizi sio mchezo lakini Mwamba anapeta tu anaenda tu hakwami hakika Iramba ina kila sababu ya kujivunia kuwa na mtoto wao Kipenzi kabisa na mwenye akili kama Mwigulu !

Nadhani andiko lako lingekaa namna hii ingependeza sana tunamhitaji Mwigulu Nchemba sana
Chawa
 
Ataongoza mawe labda. Mark my words, Mwigulu, January na Kigwa, hawatakaa kuwa namba 1 wa nchi hii. Hii nchi ina watu wanafanya kazi usiku na mchana. Haupewi tu namba 1 kirahisi rahisi.
 
Ataongoza mawe labda. Mark my words, Mwigulu, January na Kigwa, hawatakaa kuwa namba 1 wa nchi hii. Hii nchi ina watu wanafanya kazi usiku na mchana. Haupewi tu namba 1 kirahisi rahisi.
kama kikwete alipewa, hao nao wanaweza kupewa!
kumpa kikwete lilikua ndio hitimisho la anguko letu.........
heshima yetu ilipotea kuanzia hapo,
 
kama kikwete alipewa, hao nao wanaweza kupewa!
kumpa kikwete lilikua ndio hitimisho la anguko letu.........
heshima yetu ilipotea kuanzia hapo,
Kikwete hakupewa, alinyimwa wakati anastahili kuliko yeyote. Kwa sababu ya uvumilivu wake, akaja kula mbivu. Hao wengine hawastahili kabisa. Kuna Mengi huyajui kabisa kwenye hii nchi, kaa kwa kutulia.
 
Wabunge wa sisiemu hawashindwagi katika chaguzi weweeee
 
Back
Top Bottom