TUNAPOICHUNGUZA QUR'AN
Mada yetu itatokana na aya Quran 2:34 ambayo kwa mtu makini sana anaweza kupata maswali mengi na mengine yakamtoa katika usingizi wa madanganyo naam , kumbuka Yesu anasema kupitia Mtume Yohana kuwa tunapaswa kuzichunguza roho (aina yoyote ya mafundisho ya kiroho kutoka chanzo chochote ) maana udanganyifu upo
1 Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.
1 Yohana 4:1
Hebu tuisome aya kwa mtiririko mzuri na aya zinazofuatia ili tujifunze na waislamu nini nilikusudia katika swali langu la siku tatu zilizopita
Quran 2:34.
Na tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam, wakamsujudia wote isipo kuwa Iblis, alikataa na akajivuna na akawa katika makafiri.
Aya hii imeacha utata nao ni huu
i) Mungu aliwaamrisha Malaika wamsujudie Adamu wakati tunajua fika Mungu anataka kusujudiwa Yeye peke yake hapo kuna kitu cha kutazamwa sana
ii) Malaika wote wakamsudia isipokuwa Ibilisi , yeye alikataa na akajivuna na hivyo akawa katika makafiri (hii inamaanisha Ibilisi si kiumbe wa kwanza kuasi) katika imani ya waislamu maana neno makafiri maana yake ni hii
"asiyefuata maelekezo ya Mungu au aliye kinyume na Mungu"
Katika aya ya Quran 18:50 imeandikwa baada ya Ibilisi kugoma kumsujudia Adamu akawa miongoni mwa makafiri maana yake ni kwamba tayari viumbe waliokuwa wakimpinga Mungu walikuwepo sasa jaribu kuwatafuta ni viumbe gani maana Adamu alikuwa hajaasi
Quran 18:50.
Na tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam! Walimsjudia isipo kuwa Iblisi. Yeye alikuwa miongoni mwa majini, na akavunja amri ya Mola wake Mlezi. Je! Mnamshika yeye na dhuriya zake kuwa marafiki badala yangu, hali wao ni adui zenu? Ni ovu mno badala hii kwa wenye kudhulumu.
Ukiisoma aya hiyo kwa umakini unagundua kumbe Ibilisi alikuwa ni jini ila amri ya kusujudu waliagizwa Malaika ila Ibilisi akatiwa hatiani kwa kugoma kwake.
Je, ni sahihi kumwadhibu mtu kwa kosa lisilo mhusu? Yaani waambiwe madaktari wote walete vyeti wewe ni mwalimu nae ubebe cheti na ukikataa kuleta utiwe hatiani
Adhabu hii haikuwa na logic na aya ya 18:50 inazaa utata zaidi kuwa:-
i) Ibilisi alikuwa jini aliyeishi na Malaika (kivipi mie na wewe hatuna majibu)
ii) Huko peponi kwa Mungu wa waislamu ndiko alikoumbiwa Ibilisi na Adamu huku makafiri wengine wakiwa hawatajwi ni akina nani na walikuwa wapi
Je,ni wanadamu au majini peke yake? Na kama ni majini majini yote yaliasi lini na ilikuwaje jini moja tu ndilo lionekane huko likiwa halijaasi mengine hayatajwi yalikuwa wapi wala kuasi kwao ni kupi!?
Usichoke twende kwenye point
Juzi niliuliza swali
"BUSTANI YA EDENI ILIKUWA WAPI(ILIKUWA DUNIANI AU MBINGUNI?)
Mwislamu mmoja akajibu kuwa Bustani husika(ya Edeni) ilikuwa mbinguni nami nikakubali sawa ili tukutane kwenye mada hii vizuri ,hebu tujisomee aya zaidi kutoka Quran 2 hiyo hiyo zikielezea kilichoendelea
Quraan 2:35
Na tulisema: Ewe Adam! Kaa wewe na mkeo katika Bustani, na kuleni humo maridhawa popote mpendapo, lakini msiukaribie mti huu tu; mkawa katika wale walio dhulumu.
Take a note: Baada ya Ibilisi kuwa kafiri na kuwa miongoni mwa makafiri ambao hawajulikani ni viumbe gani Mungu aliendelea na Mipango yake kwa Adam na mkewe ,akawapa bustani na akawaambia ikiwa wataukaribia mti (ambao hautajwi) watakuwa kati ya wale waliodhulumu maana yake ni kuwa waliodhulumu walikuwepo mbinguni nje ya Ibilisi kama tulivyoona hapo juu sasa kitu cha kufikirisha kwa kina kikawa ni hiki, naomba usome kwa umakini
36.
Lakini Shet'ani aliwatelezesha hao wawili na akawatoa katika waliyo kuwamo, na tukasema: Shukeni, nanyi ni maadui nyinyi kwa nyinyi. Katika ardhi yatakuwa makaazi yenu na starehe kwa muda.
Shetani (ambaye) hatajwi ni kiumbe gani aliwatelezesha (aliwafanya Adamu na mkewe wavunje amri ya Mungu ) akawa amefanikiwa kuwatoa humo bustanini kisha mungu wa waislamu akawaambia washuke (watoke mbinguni huko ) na watambue wazi watabaki kuwa maadui yaani Shetani na Adamu na mkewe watakuwa maadui ,
Nilipouliza swali nilitaka tu nijue somo hili kama waislamu washalifikiria vizuri na majibu yao yalikuwa ndiyo yanazalisha utata zaidi maana kama Bustani ya Edeni ilikuwa mbinguni , shetani akawadanganya akina Adam na mkewe hukohuko means kumbe Shetani alikuwa akiishi mbinguni kwa muda mrefu tena huku akiwa kafiri (yaani Mungu alikuwa anaishi na kafiri Ibilisi hukohuko mbinguni)
FIKIRI KWA KINA SASA
Shetani alikuwa anaishi mbinguni yeye na Malaika na Mungu hadi akaenda kuwadanganya watu humohumo mbinguni na baada ya hapo ndipo Mungu akawatimua huko mbinguni Shetani na Allah wana ushirika? Maana muasi alikaa na Mungu mbinguni hadi akaleta mambo ya ajabu zaidi na Mungu yupo anamtazama.
Upi ulikuwa ni mpango wa Mungu juu ya kuiumba dunia maana baada tu ya kuasi kwa Adamu na mkewe ndipo wakaletwa duniani kama adhabu.Yaani kwa kifupi kama Adamu asingeasi basi Shetani, Mungu na Wanadamu wote wangekuwa wanaishi pamoja mbinguni.Umeelewa utata huo?
Aliyewadanganya Adamu na na mkewe ni Shetani, hatuambiwi Ibilisi ambaye nae aliwekwa miongoni mwa makafiri alipotelea wapi maana walifukuzwa watu watatu tu Shetani (kafiri mmojawapo) kati ya makafiri wengi waliokuwa mahali pasipotajwa ,Adam na mkewe.
ADAM AKAFUNDISHWA KUOMBA MSAMAHA NA AKAKUBALIWA TOBA
37.
Kisha Adam akapokea maneno kwa Mola wake Mlezi, na Mola wake Mlezi alimkubalia toba yake; hakika Yeye ndiye Mwingi wa kukubali toba na Mwenye kurehemu.
Yaani Mungu aliyekosewa akamfundisha Adamu namna ya kuomba msamaha Adamu akaomba msamaha akakubaliwa ila bado akatimuliwa mbinguni.Ipi ilikuwa sababu ya Adamu kuendelea kupewa adhabu sawa na Shetani wakati ameshaomba msamaha? (Fikiria mwenyewe) kuna uhakika upi kuwa hata wewe mwislamu utasameheka mbele za Allah kama tu Adam aliyefundishwa hata namna ya kuomba na akafanya hivyo aliishia kutupwa duniani ?
Kumbe duniani tuko katika adhabu wapendwa kwa mujibu wa Allah kumbe sisi ni waasi A-Z nje ya hapo tungekuwa tupo mbinguni sasa na ninaposema uhakika wa uzima haupo upande wa waislamu warejee tu kesi ya Adamu na Shetani kwa urahisi
Aya hii haikupi uhakika wa maneno ya Allah
38.
Tukasema: Shukeni nyote; na kama ukikufikieni uwongofu utokao kwangu, basi watakao fuata uwongofu wangu huo haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika.
Mungu anawatimua afu anawaambia kama uongofu utakuja kwenu kutoka kwangu ufuateni wakati huo Adamu alishaomba msamaha palepale mbinguni akakubaliwa toba yake ila akatimuliwa kama kawaida.Je, huo ni msamaha kweli?Kwangu huu si msamaha .
Mambo muhimu zaidi kuyajua yanapaswa kuwa ni :-
Inawezekana kabisa mbinguni kwa Allah bado kuna makafiri wengi tu maana hakuna aya inayoonesha makafiri wa mwanzo kabla ya Ibilisi kuwa kafiri walikuwa wanaishi wapi ila kafiri mmojawapo ndiye huyo alikuja kumdanganya Adam na mkewe na hao watatu wakatupwa duniani kama adhabu that means walikuwa wanaishi mbinguni na ikiwa Ibilisi ndiye shetani basi itakuwa hivi
1.Ibilisi aligoma kutii amri ya Allah , akawa kafiri ila bado akawa yupo mbinguni tu na akaamua kuwadanganya Adam na mkewe ndipo akatimuliwa kuja duniani
2.Ibilisi yeye ana jinsi mbili yaani Ke na Me maana majini mengine yanayonenwa katika Quran 72 yalitoka wapi wakati jini lilikuwa moja huko mbinguni na lilitimuliwa huku duniani lilipata vipi uzao?
3.Ibilisi aliye jini aliweza vipi kuishi na Malaika kama ni viumbe tofauti ?
4.Ikiwa shetani aliyemdanganya Adamu na mkewe si Ibilisi basi Ibilisi anaishi na Allah peponi huko sasa ipi ni kesho ya waislamu maana kwetu Ibilisi ni shetani mwenyewe
9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
Ufunuo wa Yohana 12:9
TAFAKARI