Je, kuna uhusiano kati ya IQ ya mtu na kabila lake, umasikini wake au kimo chake?

Je, kuna uhusiano kati ya IQ ya mtu na kabila lake, umasikini wake au kimo chake?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
59,804
Reaction score
134,593
Wanabodi,

Usingizi umekata kutokana na mawazo ya huku kukaza kwa vyuma kwa baadhi yetu kwenye Tanzania hii ya Magufuli. Kiukweli kabisa, kuna watu tuna suffer!, mtu unalala ukiwa totally empty hujui kesho siku itaanza vipi!. Hivyo faraja yangu pekee ni JF. Nimesoma uzi fulani, nikaanza kuwaza na kujiuliza maswali huku mengine nikijijibu mwenyewe.

Huu ni uzi wa swali kuhusu IQ za baadhi ya watu wakiwemo wanasiasa wetu wanaotuhumiwa kuwa na low IQ, wakiwemo baadhi ya mawaziri, wabunge na wakuu wa mikoa, na vigogo wengine wengi wa vyama na serikali, hivyo swali la kwanza kujiuliza, ni, jee ni kweli hawa wanaotuhumiwa kuwa na low IQ, jee ni kweli wana low IQ, au ni mtu tuu ametoa mawazo tofauti na wewe huyapendi, ndio unamtukana ana low I.Q?.
I.Q Ni Nini?, na Inapimajwe?.
I.Q ni kifupi cha Intelligence Quotient ambao ni uwezo wa uelewa wa mambo wa akili ya binadamu, katika ufahamu, uelewa, kujieleza, kuchambua mambo, kujenga hoja, hekima, busara na mambo mengine yote yanayohusiana na kutumia ubongo, a,napo watu wenye IQ kubwa, hufanya vizuri darasani na kwenye mitihani, watu wenye IQ ndogo hufanya vibaya.

Kwa kawaida, IQ ya mtu hupimwa kwa vipimo mbalimbali, kipimo kikuu kikiwa ni kufanya aptitude test. Mimi nilipoajiriwa na FCO, ya UK, (Foreign Commonwealth Office), shortlisting tulikuwa watu 10, tukaitwa kwenye oral interview, tukabaki 5, tukaingia kwenye final aptitude test, nikapata kazi.

Test ninayoitumia hapa, ni matokeo ya ufaulu wa darasa la saba kuingia sekondari, na matokeo ya ufauli wa kidato cha nne, sio kwa mtindo wa data collection, bali general sampling. Kwa nini watu wa maeneo fulani fulani, wanafaulu zaidi kuliko watu wa maeneo mengine, au kwanini watu wa makabila fulani fulani, wana akili kuliko makabila mengine!.

Maswali ya Kujiuliza Uhusiano wa Akili na Eneo, Kabila, Umasikini na Kimo.
Ndipo nikaanza kujiuliza, jee kuna uwezekano watu wenye IQ ndogo ni kutokana na makabila yao, kiwango chao umasikini kwenye makuzi, au pia heights zao have something to do with low IQ, yaani mtu akiwa mfupi, anakuwa na akili fupi?.

Thread ya Kuulizia IQ ya Mtu.
Mtu wa kwanza kujiuliza kuhusu I.Q ta mtu sio mimi, bali kuna thread ilipanda humu!.
Naomba kukiri zaidi ya kukosa usingizi, nimekuwa inspired na motivated kupandisha bandiko hili kutokana na hoja za mwana jf huyu, jidu-la-mabambasi, katika bandiko lake hili
Juma Nkamia ana tatizo la msingi!
Jamani nijulisheni ,huyu Nkamia mbona ana IQ ndogo hivi?
Na anawawakilisha jimbo gani?
Mkuu Jidu, kwa vile mimi nimefanya kazi na Mhe. Juma Mkamia alipojoin RTD, hivyo naomba nisicomment kuhusu IQ yake, kwa sababu kupata kazi Tanzania, hakuna aptitude test, wala sijafanya nae test kujua scores zake, ila generally kuna uhusiano mkubwa kati ya kiwango cha IQ ya mtu nikimaanisha akili, na abject poverty. Maeneo yenye umasikini uliotopea, IQ za wengi ziko low!.

Umasikini na Ufaulu, Mkoa Tajiri Wanafaulu Sana, Mikoa Masikini Wanafeli Sana
Angalia level ya umasikini ukanda wa Pwani, including Zanzibar, mikoa ya Singida, Dodoma, Lindi na Mtwara, au makabila yenye umasikini uliotopea kama Wagogo, Warangi, Wanyaturu, Wabarbaig, Wasandawe, Wataturu, Wahadzabe, Wazaramo, Wandengereko etc, linganisha na mikoa yanye neema, Kilimanjaro, Bukoba, Mbeya, Iringa, Mwanza, etc, angalia IQ za Wachagga, Wahaya, Wanyakyusa etc, bila kusahau the royal tribe, Wasukuma, watu wanaokula vizuri, wanakuwa na IQ kubwa. Makabila ya mlo mmoja, wanakuwa na low IQ!.

Data Zangu ni Random Sampling ya Cut of Points za Kupasi ma Ufaulu wa Form IV
Data zangu ni kwa mujibu wa random sampling ya matokeo ya mitihani ya kidato cha 4!. Hili hata Mwalimu Nyerere aliliona, hivyo hadi leo, japo Tanzania nzima wanafanya mtihani mmoja wa darasa la saba lakini cut off points za kufaulu kwenda sekondari ni tofauti mikoa na mikoa ili Watanzania wote wapate fursa sawa za kuendelea kielimu. Tungetumia uniform cut off points, shule zote za sekondari nchini, zingejaa watu wa baadhi ya makabila tuu, au baadhi ya maeneo, wakiwemo Wachagga, Wahaya na Wanyakysa na kuna makabila na maeneo, wasingegusa kabisa secondary, saves for the exceptional to the case.

Kuna Primitive Tribes na Advanced Tribes
Tanzania japo tuna makabila 120, makabila haya hayalingani, kuna makabila makubwa, na kuna makabila madogo, the biggest tribe or the giant ni Sukuma, the smallest ni Hadzabe.

Uwezo wa akili za makabila haya unatofautiana, hivyo kuna advanced tribes, developed tribes na primitive tribes, hawa developed tribes wana akili zaidi za dasani kuliko the primitive tribes, lakini when it comes to intelligence, kuna primitive tribes wako more intelligent kuliko developed tribes, mfano the Masai are the best in alternative medicine, na ndio wana the best birth control, hawazaliwi vilema, wala zeruzeru!.

Baadhi ya advanced tribes hadi kuzungumza kwa kilugha wanachomekea kimombo kidogo, mfano " mugambire inafu", "anigambire fulishi infront of my wife", wengine.

Hawa developed tribes unakuta hadi vijijini wana nyumba bora, maji ya bomba na umeme, wakati wengine bado wanaishi kwenye tembe!. Jee akili zitafanana?.

Viwango Tofauti vya Ufaulu, Wengine Wana Akili, Wengine Vilaza!'
Tulipopata uhuru, nchi zote zinazotawaliwa na Uingereza, tulifanya mtihani mmoja tuu wa Cambridge, ulitungwa London, hivyo ni watu wa baadhi tuu ya makabila waliweza kufauli kuingia sekondari.

Tukadhania ni kwa sababu mitihani inatungwa London, hivyo tukaachana na mitihani ya London, tukaanzisha NECTA, tukatunga mitihani yetu, bado tukakuta ni baadhi tuu ya makabila wanafanya vizuri, hivyo tukiendelea hivi kuna makabila shule wataushia kuisikia tuu.

Ndipo Nyerere akaamua kubadili viwango vya ufaulu, ili kila Mtanzania asome na elimu ilikuwa bure.

Mwalimu Nyerere aliwahi kuwasomesha kwa nguvu watoto 4 wa kabila la Wahadzabe, wote walifeli darasa la saba, lakini akalazimisha waende sekondari kwa lazima. Wakasomea pale Pugu, na wote wanne walipata Divisheni Zero!.

Niliwahi kuuliza swali hili, sikupata jibu
Inawezekana Vipi Zanzibar Hakuna Div I, Div II, wala Div III , Wao ni Div IV na Div Zero Tuu?!.

Jee Kuna Uhusiano Kati ya Height ya Mtu na Akili Zake?.
Ila pia kuna uhusiano kati ya heigh ya mtu na akili zake, mtu akiwa mfupi, anakuwa na akili fupi!' Anza kuwa observe heights za waropokaji bungeni, utaniambia!'
Hili la watu wafupi, nililizungumza hapa, wanafanya vitu vya ajabu kutafuta recognition ili ku compensate inferiority complex yao inayosababishwa na height!.

Je, kuna ukweli watu wafupi wana inferiority complex hivyo kukasirika sana wanapohisi kudharauliwa?
Madhara ya Kisiasa ya Poverty Stricken Areas
Hili la poverty level na low IQ lina athari kubwa kisiasa, angalia levels za umasikini kwenye maeneo watu waliochagua upinzani, ulinganishe na ngome za CCM, utakuta kwenye umasikini uliotopea ndizo ngome za CCM, na kule kwenye ehueni, na maeneo ya mijini, ndio wamewachagua wapinzani, angalia Kilimanjaro, Bukoba, Arusha, Tanga, Iringa, Mbeya etc, mkoa kama Dodoma hauwezi kuchagua upinzani, they are just too poor to make an informed decision to understand wanachagua nini!, t-shirt, kofia na shibe ya siku moja, inatosha kushawishi wachague nini!. Hata Singida, Lissu is an exceptional case. Hivyo hii situation ya IQ level ina effects kwenye siasa zetu, hivyo kuendelea kushinda kwa CCM, has something to do with this na nilisema hapa
Watanzania ni ignorants au tumelogwa? October 25, tutafanya informed decision au tutachagua tuu?

Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi!

Ikitokea CCM ishinde, Je ushindi huo ni kutokana kuwekeza kwenye Maendeleo au kwenye Ignorance?

Kuichagua tena CCM, Je ni kielelezo cha kufanya informed decision, au ni Ignorance?
IQ za Watanzania ni za Ajabu, Zinabadilika Badilika!.
Hoja zote hizo zinauhusiano na I.Q, na kitu cha ajabu kabisa, ni kuwa I.Q is supposed to be constant, na static, lakini IQ za Watanzania no ni za ajabu sana, they are dynamic and hence they change with time and place, kwa kadri vyuma vinavyobana, ndivyo CCM inavyoimarika, hivyo 2020 mtashuhudia, karibu majimbo yote ya upinzani kama sio yote kabisa huku bara, yatairejesha CCM, upinzani utaanza tena 2025 baada ya rais Magufuli kuipeleka Tanzania kwenye uchumi wa kati, na kuumaliza umasikini.

Every General Rule, Has Exceptional To The Cases
NB. Kwenye every general rules, there is always exceptional to the case, hivyo hivyo kuna watu wa makabila masikini wenye high IQ, na kuna watu wafupi wenye akili ndefu na kuna mijitu mibonge yenye akili fupi and vice versa!.

Paskali
Rejea

Psychoanalysis: Superiority Complex ni Dalili ya Inferiority Complex!. Maneno Mafupi Vitendo Virefu.

Je, kuna ukweli watu wafupi wana inferiority complex hivyo kukasirika sana wanapohisi kudharauliwa?

Character Assassination ni Modus Oparandi ya Madikiteta Katili Wote Duniani!

Kuwa Kichaa Sio Mpaka Kuokota Makopo!. Jee Tanzania Tuna Vichaa Wengi Kuliko Tunavyojidhania?!.
------------

Mdau field marshall1 amepanua wigo wa mjadala huu. Unaweza kusoma hoja zake na kushiriki mjadala >> Tatizo la ufukara kwa baadhi ya makabila ni mfumo wa maisha (Lifestyles)
 
“IQ kubwa siyo aghalabu/kawaida, kupatikana kwenye umasikini”, nakubaliana na hoja.

Kwenye umasikini kuna mambo mengi yanayochangia low IQ.

Pia culture ina contribute hapo.

Kwenye kimo sidhani. However, kuna studies zinaonyesha watu wafupi kuwa na low self esteem.

People who experience social situations from a lower height - in other words short people - are more prone to feelings of paranoia, inferiority and excessive mistrust.

In a study in the journal Psychiatry Research, scientists showed that making a person's virtual height lower than it actually is can make them feel worse about themselves and more fearful that others are trying to harm them.
 
IQ za wanasiasa wa awamu hii zinadumazwa na woga. Wanasiasa hawajikiti kwenye kutafuta mbinu za kutatua matatizo ya wananchi bali wanashindana kumsifia na kumfurahisha magu ili wajihakikishie usalama na maslahi yao. Eti aongozewe muda, kwa kipi kikubwa alichowafanyia wananchi mpaka sasa?

Magu hata ateue ma PHd watupu kuongoza wilaya na mikoa na halmashauri zote bado haitaifanya awamu hii kuwa bora kiuchumi kuliko awamu zilizopita. Woga ndani ya umasikini hautaliacha taifa salama.
 
Notification ya hii thread imenifanya nishtuke usingizini,

Pascal ni kweli 100 percent, Niliwahi soma sehemu fulani Undergraduate level, Darasa nzima walijaa wanyakyusa na wachaga,

Kwenye kupanga groups zile Sir Name za wanyakyusa zinazoanza na "Mwa " hujikuta group moja wanaanza ongea kilugha kama wewe una kijina cha "mwa "halafu sio wa huko imekula kwako

Nakumbuka huo mwaka mpaka hicho chuo kikubwa hapa Tanzania wakaamua kufuta association zote za makabila maana weekend wakiitana vikao hapatoshi

Kwa hii mada sipingi nimeyaona mwenyewa na nimeishi na hao chagas na nyakyusa
 
Ndiyo kuna uhusiano mkubwa
✓Mtu mrefu kuliko kawaida akiwa amelelewa katika mazingira duni hakupata rishe bora I.Q yake inakuwa slow more nawengine hupitiliza nakuwa mbulura!
✓Kuhusu kabila yapo makabila yenye uelewa mdogo!
✓Umasikini uchangia hasa kuanzia ujauzito mama akikosa lishe lazima na mtoto ataathirika.
✓Naishia hapo.
 
Environmental Factors that affect IQ include:
  • modern media
  • education
  • breast feeding
  • womb conditions
  • nutrition
  • pollution
  • nurture and parenting
  • prejudices and self belief
  • national culture
  • head injuries
  • sleep problems
  • drug and alcohol abuse
  • mental illnesses:
  • stress and diseases:
 
Hayo mambo yalikuwa zamani dunia imebadilika n.a. maisha ni safari tumeoana sana kudilute umasikini ,IQ,n.a. Mila za makabila ndoto za mwalimu zimetimia kwa 70% hata wanaoleta ukabila Leo hawaijui tanzania, low IQ ya viongozi wengi kwa vile hawasimamii vilivyomo kichwani wanasimamia vilivyomo tumboni they don't stand on reality

Vilivyomo tumboni ni scalar quantity n.a. viliyomo kichwani ni vector quantity lazima I dot upata direction ukifikiria scalar quantity tu utakosa direction
Njaa ni asubuhi unakula mchana tena inarudi tena
 
Mkuu Pasco, usicheze na sisi watu wa Pwani. Huku Pwani ambae alikuwa na IQ ndogo ni Kawawa peke yake and probably kwa sababu ana damu ya bara (Ruvuma)!

I know you're smart enough to know kufaulu darasani; hususani kwenye elimu hii ya kukaririshana has nothing to do with IQ.

Sisi watu wa Pwani of course hatufanyi vizuri darasani ( sahau zile porojo za watu za kuhusisha madrasa. Ni Waislamu wachache sana wanaoenda madrasa na ukikutana na mtoto wa madrasa anayependa shule lazima awaburuze. Ikiwa mtu anameza Msahafu; atashindwa nini kumeza History book?) lakini sababu kubwa sio IQ but it's more historical.

Nitafafanua next time.
 
Sio kweli kuwa IQ ya mtu inakuwa influenced na Kabila.

" Kabila " has nothing to do with IQ.

Kuna wengine kujua tu lugha ndio kunamfanya awe wa kabila alilo nalo baas.

Ila nutrition au Diet inaweza kuinfluence IQ ya mtu hasa mtoto.

Kwa ulaya, karne nyingi za zamani ndizo zilizotoa geniuses wengi maarufu duniani na waliofanya gunduzi mbalimbali. Kama akina Michael Faraday, Albert Einstein, Aristotle, Alexander Bell, Isac Newton, Macnon na wanafalsafa mbalimbali wakubwa.

Miaka hii ambayo kwa ulaya na Amerika chakula kimeboreshwa sana kiubora hatuoni watu wenye IQ kubwa kama zamani.

Wajapan wana IQ kubwa mno na wanasema sababu ni kuwa wanakula sana raw marine organisms

Mtu mwenye IQ kubwa anaweza kuwepo katika kabila lolote lile kiasili ila anaweza asije kujulikana kwasababu ya mazingira yanayomzunguka na jamii anayoishi nayo.

Suala la Wachaga, Wahaya na Wanyakyusa kuwa wengi katika nyanja za elimu linatokana na suala la kihistoria ambalo ni

Uanzishwaji wa makanisa,hospitali, shule, na taasisi nyingi za kielimu katika ardhi yao, uliofanywa na wakoloni

Na ndio maana kuna idadi kubwa sana ya Wakristo walio wasomi kuliko Waislam tangu enzi hizo kwasababu taasisi hizo za elimu, dini na afya zilianzishwa katika mikoa yao, mfano Kilimanjaro, Mbeya, Kagera na hata Arusha pia kuna taasisi nyingi za elimu za wakoloni.

Mikoa yenye waislam wengi (kasoro wagogo tu) ndiyo uliyoiorodhesha katika list ya wenye IQ ndogo kama Mtwara, Lindi, Kondoa(kwa warangi), Wanyaturu.

Pia ingekuwa ni suala la chakula pekee iongezayo IQ basi wasukuma, wahehe na watu wa morogoro wenye vyakula haswa nao wangekuwa wengi vyuoni ila sivyo ilivyo mpaka sasa.

This case is mainly based on historical matter.
 
Mkuu Pasco, usicheze na sisi watu wa Pwani. Huku Pwani ambae alikuwa na IQ ndogo ni Kawawa peke yake and probably kwa sababu ana damu ya bara (Ruvuma)!

I know you're smart enough to know kufaulu darasani; hususani kwenye elimu hii ya kukaririshana has nothing to do with IQ.

Sisi watu wa Pwani of course hatufanyi vizuri darasani ( sahau zile porojo za watu za kuhusisha madrasa. Ni Waislamu wachache sana wanaoenda madrasa na ukikutana na mtoto wa madrasa anayependa shule lazima awaburuze. Ikiwa mtu anameza Msahafu; atashindwa nini kumeza History book?) lakini sababu kubwa sio IQ but it's more historical.

Nitafafanua next time.
Kawawa funika kikombe,
 
IQ ni mojawawapo ya basic superior qualities zinazorithiwa kutoka kwa wazazi.
Kuna kizazi (jamii) ambavyo gene ya high IQ ni dominant wakati vingine ni recessive.
Maeneo fulani yanatakiwa yafanye upgrading ya watu wao kwa kufanya crossbreeding na kwingine.

Hata hivyo, ni muhimu kutambua kuwa mambo yote ya kurithi ni ya asili na hivyo hubadlishwa kwa njia hizo hizo.
 
Tukiongelea umasikini wa Kanda na mikoa mleta mada aliyooridhesha hapa tuanzie na historia ya Tanzania na influence ya wakoloni.

Mikoa ya Bukoba, Kilimanjaro, Tanga, Mbeya ni mikoa iliiyobahatika kupata shule za kwanza baada ya wazungu kuleta elimu. Hata Zanzibar.

Tofauti kubwa hapa ni kuwa Zanzibar na Tanga ilimezwa na utamaduni wa ki Arabu kabla ya uzungu.

Pamoja na kuwa shule zilikuwepo lakini wazazi wengi walipata wakati mgumu kuchagua kati ya elimu dunia na elimu akhera.

Kwa dhana ya dini Tanga wamegawanyika sana. Unakuta ukoo mmoja wale walioamua kwenda katika shule za wamissionary walibadili dini.

Utamaduni waawaarabu kwa wakati ule ulikuwa ni biashara na biashara zao nyingi ilikuwa utumwa na kilimo cha minazi. Minazi ikitunzwa vizuri hukaa kwa miaka 50-100. Hivyo ili fanya wazee wapumzike.

Hata hivyo ninaamini mikoa ya Pwani imetoa wazee wengi wakiokuwa na mchango mkubwa katika taifa.
 
Back
Top Bottom