Lord Denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 23,491
- 57,973
Ni Kweli kabisa ndugu. Ushirikina umerudisha sana nyuma maendeleo ya nchi yetu. Watu wanaamini katika ushirikina na imepelekea jamii zetu kuwa nyuma sana.Nakubaliana na wewe. Tuseme utamaduni wa watu unahusiana sana maendeleo yao. Kuna mtu namfahamu leo hii namshauri ajenge kibanda cha rumu japo mbili cha tofali anasema nataka afe! Maana jamaa zake wote hawana. Ukoo mzima hakuna mwenye elimu na mzazi kumwambia mtoto asiende shule ni kawaida tu. Watu wanalima hawaoni umuhimu wa mbegu bora au mbolea na dawa.
Suluhisho ni kuwabadili watu kupitia elimu.
Kwa nini maeneo mengine watu wana IQ kubwa kuliko mengine?
Kuna suala la lishe pia. Maeneo hayo utakuta yana hali ya hewa nzuri chakula ni kingi, samaki nk. Watoto wanazaliwa na kupata lishe bora kuloko maeneo mengine.
Pia urithi. Jamii yenye uwezo mkubwa wa akili huwarithisha vizazi na vuzazi.
So, utamaduni, lishe na urithi ni factors chache zinafanya jamii kutofautiana katika kiwango cha maendeleo na akili
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna haja kubwa ya kuweka mkakati maalum ukihusisha Serikali na Viongozi wa Dini ili kuzibadilisha jamii zetu kifikra.