This is...
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 5,198
- 5,454
acha mhemko wa chuki za kijinga. hivyo vphd hadi leo hamnao ktk ukoo wako wote.
Naunga mkono hoja, hili jambo niliwahi kulizungumza pia katika mabandiko hayaKuwa na hisa ndogo ya akili hakutokani na kukosa tu elimu ya Darasani japokuwa nayo huchangia bali hutokana na sababu nyingine nyingi kama vile Lishe duni, afya duni, aina ya genes tunazorithi toka kwa mababu zetu nk.
ujinga ni kitu cha kurithi na ni kama ugonjwa. Hili limeshawahi kudhihirishwa na nadharia nyingine nyingi za kisayansi na za kisaikolojia.
Kuna mambo mengi tu yanayodhihirisha ujinga wetu hata wewe comment yako pia inaweza kukutambulisha aina ya IQ uliyonayo.
Pascal umesahau takwimu ya udumavu Tz 60% au !!?? Maana ungekuwa umekumbuka usingeleta mada hii. Haswa ukizingatia Udumavu unaathiri mwili na akili mbaya zaidi ukishahathirika utotoni hakuna kubadilika ataa kama utapata lishe bora baadae .Lete mada ya kupigia chapuo Lishe bora iwe kipaumbile cha kwanza cha Taifa .kama Ujerumani walivyo fanya baada ya vita kuu .hii IQ uwezi pata ndani ya wadumavu aijalishi wa kabila au dini au eneo gani .kwa lugha ingine njaa haichagui [emoji23] [emoji23] [emoji23]Wanabodi,
Usingizi umekata kutokana na mawazo ya huku kukaza kwa vyuma!, mtu unalala hujui kesho siku itaanza vipi, ukiwa totally empty!. Hivyo faraja yangu pekee ni JF. Nimesoma uzi fulani, nikaanza kuwaza na kujiuliza maswali huku mengine nikijijibu mwenyewe.
Huu ni uzi wa swali kuhusu I.Q za baadhi ya wanasiasa wetu wanaotuhumiwa kuwa na low I.Q, wakiwemo mawaziri, wabunge na wakuu wa mikoa, na vigogo wengine wengi, hivyo nikajiuliza kwanza jee ni kweli hawa wanaotuhumiwa kuwa na low I.Q, jee ni kweli wana low I.Q, au ni mtu tuu ametoa mawazo tofauti, wewe huyapendi, ndio unamtukana ana low I.Q?.
I.Q Ni Nini?, na Inapimajwe?.
I.Q ni kifupi cha Intelligence Quonset, ambao ni uwezo wa uelewa wa mambo wa akili ya binadamu, katika ufahamu, uelewa, kujieleza, kuchambua mambo, kujenga hoja, hekima, busara na mambo mengine yote yanayohusiana na kutumia ubongo, a,napo watu wenye I.Q kubwa, hufanya vizuri darasani na kwenye mitihani, watu wenye I.Q ndogo hufanya vibaya.
Kwa kawaida, I.Q ya mtu hupimwa kwa vipimo mbalimbali, kipimo kikuu kikiwa ni kufanya aptitude test. Mimi nilipoajiriwa na FCO, ya UK, (Foreign Commonwealth Office), shortlisting tulikuwa watu 10, tukaitwa kwenye oral interview, tukabaki 5, tukaingia kwenye final aptitude test, nikapata kazi.
Test ninayoitumia hapa, ni matokeo ya ufaulu wa darasa la saba kuingia sekondari, na matokeo ya ufauli wa kidato cha nne, sio kwa mtindo wa data collection, bali general sampling. Kwa nini watu wa maeneo fulani fulani, wanafaulu zaidi kuliko watu wa maeneo mengine, au kwanini watu wa makabila fulani fulani, wana akili kuliko makabila mengine!.
Maswali ya Kujiuliza Uhusiano wa Akili na Eneo, Kabila, Umasikini na Kimo.
Ndipo nikaanza kujiuliza, jee kuna uwezekano watu wenye I.Q ndogo ni kutokana na makabila yao, kiwango chao umasikini kwenye makuzi, au pia heights zao have something to do with low I.Q, yaani mtu akiwa mfupi, anakuwa na akili fupi?.
Thread ya Kuulizia I.Q ya Mtu.
Mtu wa kwanza kujiuliza kuhusu I.Q ta mtu sio mimi, bali kuna thread ilipanda humu!.
Naomba kukiri zaidi ya kukosa usingizi, nimekuwa inspired na motivated kupandisha bandiko hili kutokana na hoja za mwana jf huyu, jidu-la-mabambasi, katika bandiko lake hili
Juma Nkamia ana tatizo la msingi!
Mkuu Jidu, kwa vile mimi nimefanya kazi na Mhe. Juma Mkamia alipojoin RTD, hivyo naomba nisicomment kuhusu I.Q yake, kwa sababu kupata kazi Tanzania, hakuna aptitude test, wala sijafanya nae test kujua scores zake, ila generally kuna uhusiano mkubwa kati ya kiwango cha I.Q ya mtu nikimaanisha akili, na abject poverty. Maeneo yenye umasikini uliotopea, I.Q za wengi ziko low!.
Umasikini na Ufaulu, Mkoa Tajiri Wanafaulu Sana, Mikoa Masikini Wanafeli Sana
Angalia level ya umasikini ukanda wa Pwani, including Zanzibar, mikoa ya Singida, Dodoma, Lindi na Mtwara, au makabila yenye umasikini uliotopea kama Wagogo, Warangi, Wanyaturu, Wabarbaig, Wasandawe, Wataturu, Wahadzabe, Wazaramo, Wandengereko etc, linganisha na mikoa yanye neema, Kilimanjaro, Bukoba, Mbeya, Iringa, Mwanza, etc, angalia I.Q za Wachagga, Wahaya, Wanyakyusa etc, bila kusahau the royal tribe, Wasukuma, watu wanaokula vizuri, wanakuwa na I.Q kubwa. Makabila ya mlo mmoja, wanakuwa na low I.Q!.
Data Zangu ni Random Sampling ya Cut of Points za Kupasi ma Ufaulu wa Form IV
Data zangu ni kwa mujibu wa random sampling ya matokeo ya mitihani ya kidato cha 4!. Hili hata Mwalimu Nyerere aliliona, hivyo hadi leo, japo Tanzania nzima wanafanya mtihani mmoja wa darasa la saba lakini cut off points za kufaulu kwenda sekondari ni tofauti mikoa na mikoa ili Watanzania wote wapate fursa sawa za kuendelea kielimu. Tungetumia uniform cut off points, shule zote za sekondari nchini, zingejaa watu wa baadhi ya makabila tuu, au baadhi ya maeneo, wakiwemo Wachagga, Wahaya na Wanyakysa na kuna makabila na maeneo, wasingegusa kabisa secondary, saves for the exceptional to the case.
Kuna Primitive Tribes na Advanced Tribes
Tanzania japo tuna makabila 120, makabila haya hayalingani, kuna makabila makubwa, na kuna makabila madogo, the biggest tribe or the giant ni Sukuma, the smallest ni Hadzabe.
Uwezo wa akili za makabila haya unatofautiana, hivyo kuna advanced tribes, developed tribes na primitive tribes, hawa developed tribes wana akili zaidi za dasani kuliko the primitive tribes, lakini when it comes to intelligence, kuna primitive tribes wako more intelligent kuliko developed tribes, mfano the Masai are the best in alternative medicine, na ndio wana the best birth control, hawazaliwi vilema, wala zeruzeru!.
Baadhi ya advanced tribes hadi kuzungumza kwa kilugha wanachomekea kimombo kidogo, mfano " mugambire inafu", "anigambire fulishi infront of my wife", wengine.
Hawa developed tribes unakuta hadi vijijini wana nyumba bora, maji ya bomba na umeme, wakati wengine bado wanaishi kwenye tembe!. Jee akili zitafanana?.
Viwango Tofauti vya Ufaulu, Wengine Wana Akili, Wengine Vilaza!'
Tulipopata uhuru, nchi zote zinazotawaliwa na Uingereza, tulifanya mtihani mmoja tuu wa Cambridge, ulitungwa London, hivyo ni watu wa baadhi tuu ya makabila waliweza kufauli kuingia sekondari.
Tukadhania ni kwa sababu mitihani inatungwa London, hivyo tukaachana na mitihani ya London, tukaanzisha NECTA, tukatunga mitihani yetu, bado tukakuta ni baadhi tuu ya makabila wanafanya vizuri, hivyo tukiendelea hivi kuna makabila shule wataushia kuisikia tuu.
Ndipo Nyerere akaamua kubadili viwango vya ufaulu, ili kila Mtanzania asome na elimu ilikuwa bure.
Mwalimu Nyerere aliwahi kuwasomesha kwa nguvu watoto 4 wa kabila la Wahadzabe, wote walifeli darasa la saba, lakini akalazimisha waende sekondari kwa lazima. Wakasomea pale Pugu, na wote wanne walipata Divisheni Zero!.
Niliwahi kuuliza swali hili, sikupata jibu
Inawezekana Vipi Zanzibar Hakuna Div I, Div II, wala Div III , Wao ni Div IV na Div Zero Tuu?!.
Jee Kuna Uhusiano Kati ya Height ya Mtu na Akili Zake?.
Ila pia kuna uhusiano kati ya heigh ya mtu na akili zake, mtu akiwa mfupi, anakuwa na akili fupi!' Anza kuwa observe heights za waropokaji bungeni, utaniambia!'
Hili la watu wafupi, nililizungumza hapa, wanafanya vitu vya ajabu kutafuta recognition ili ku compensate inferiority complex yao inayosababishwa na height!.
Je, kuna ukweli watu wafupi wana inferiority complex hivyo kukasirika sana wanapohisi kudharauliwa?
Madhara ya Kisiasa ya Poverty Stricken Areas
Hili la poverty level na low I.Q lina athari kubwa kisiasa, angalia levels za umasikini kwenye maeneo watu waliochagua upinzani, ulinganishe na ngome za CCM, utakuta kwenye umasikini uliotopea ndizo ngome za CCM, na kule kwenye ehueni, na maeneo ya mijini, ndio wamewachagua wapinzani, angalia Kilimanjaro, Bukoba, Arusha, Tanga, Iringa, Mbeya etc, mkoa kama Dodoma hauwezi kuchagua upinzani, they are just too poor to make an informed decision to understand wanachagua nini!, t-shirt, kofia na shibe ya siku moja, inatosha kushawishi wachague nini!. Hata Singida, Lissu is an exceptional case. Hivyo hii situation ya I.Q level ina effects kwenye siasa zetu, hivyo kuendelea kushinda kwa CCM, has something to do with this na nilisema hapa
Watanzania ni ignorants au tumelogwa? October 25, tutafanya informed decision au tutachagua tuu?
Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi!
Ikitokea CCM ishinde, Je ushindi huo ni kutokana kuwekeza kwenye Maendeleo au kwenye Ignorance?
Kuichagua tena CCM, Je ni kielelezo cha kufanya informed decision, au ni Ignorance?
IQ za Watanzania ni za Ajabu, Zinabadilika Badilika!.
Hoja zote hizo zinauhusiano na I.Q, na kitu cha ajabu kabisa, ni kuwa I.Q is supposed to be constant, na static, lakini I.Q za Watanzania no ni za ajabu sana, they are dynamic and hence they change with time and place, kwa kadri vyuma vinavyobana, ndivyo CCM inavyoimarika, hivyo 2020 mtashuhudia, karibu majimbo yote ya upinzani kama sio yote kabisa huku bara, yatairejesha CCM, upinzani utaanza tena 2025 baada ya rais Magufuli kuipeleka Tanzania kwenye uchumi wa kati, na kuumaliza umasikini.
Every General Rule, Has Exceptional To The Cases
NB. Kwenye every general rules, there is always exceptional to the case, hivyo hivyo kuna watu wa makabila masikini wenye high I.Q, na kuna watu wafupi wenye akili ndefu na kuna mijitu mibonge yenye akili fupi and vice versa!.
Paskali
Rejea
Psychoanalysis: Superiority Complex ni Dalili ya Inferiority Complex!. Maneno Mafupi Vitendo Virefu.
Je, kuna ukweli watu wafupi wana inferiority complex hivyo kukasirika sana wanapohisi kudharauliwa?
Character Assassination ni Modus Oparandi ya Madikiteta Katili Wote Duniani!
Kuwa Kichaa Sio Mpaka Kuokota Makopo!. Jee Tanzania Tuna Vichaa Wengi Kuliko Tunavyojidhania?!.
------------
Mdau field marshall1 amepanua wigo wa mjadala huu. Unaweza kusoma hoja zake na kushiriki mjadala >> Tatizo la ufukara kwa baadhi ya makabila ni mfumo wa maisha (Lifestyles)
Bila kusahau uchungu wa maisha na shida uondoa ufahamu a.k.a IQAkili nyingi ikizidi huondoa maarifa
hawa ni janga janga na ukoloni umewasupport sana kuwa juu Kielimu kinyume na hapo nothingSio kweli kuwa IQ ya mtu inakuwa influenced na Kabila.
" Kabila " has nothing to do with IQ.
Kuna wengine kujua tu lugha ndio kunamfanya awe wa kabila alilo nalo baas.
Ila nutrition au Diet inaweza kuinfluence IQ ya mtu hasa mtoto.
Kwa ulaya, karne nyingi za zamani ndizo zilizotoa geniuses wengi maarufu duniani na waliofanya gunduzi mbalimbali. Kama akina Michael Faraday, Albert Einstein, Aristotle, Alexander Bell, Isac Newton, Macnon na wanafalsafa mbalimbali wakubwa.
Miaka hii ambayo kwa ulaya na Amerika chakula kimeboreshwa sana kiubora hatuoni watu wenye IQ kubwa kama zamani.
Wajapan wana IQ kubwa mno na wanasema sababu ni kuwa wanakula sana raw marine organisms
Mtu mwenye IQ kubwa anaweza kuwepo katika kabila lolote lile kiasili ila anaweza asije kujulikana kwasababu ya mazingira yanayomzunguka na jamii anayoishi nayo.
Suala la Wachaga, Wahaya na Wanyakyusa kuwa wengi katika nyanja za elimu linatokana na suala la kihistoria ambalo ni
Uanzishwaji wa makanisa,hospitali, shule, na taasisi nyingi za kielimu katika ardhi yao, uliofanywa na wakoloni
Na ndio maana kuna idadi kubwa sana ya Wakristo walio wasomi kuliko Waislam tangu enzi hizo kwasababu taasisi hizo za elimu, dini na afya zilianzishwa katika mikoa yao, mfano Kilimanjaro, Mbeya, Kagera na hata Arusha pia kuna taasisi nyingi za elimu za wakoloni.
Mikoa yenye waislam wengi (kasoro wagogo tu) ndiyo uliyoiorodhesha katika list ya wenye IQ ndogo kama Mtwara, Lindi, Kondoa(kwa warangi), Wanyaturu.
Pia ingekuwa ni suala la chakula pekee iongezayo IQ basi wasukuma, wahehe na watu wa morogoro wenye vyakula haswa nao wangekuwa wengi vyuoni ila sivyo ilivyo mpaka sasa.
This case is mainly based on historical matter.
Mkuu Paskali una-instigate uhutu na ututsi katika nchi hii. Please stop this. Haisaidii chochote, watanzania hatutakubali kuona watu wanajaribu kujikuza over others. Take it from me, hatutakuwa tayari kabila moja lijitukuze at the expense ya makabila mengine hapa Tanzania. Kabila la wasonjo ni dogo lakini likiona kuna ndivyo sivyo kwa minajili ya ukabila litafight hadi mwisho. Be composed when writing to mass.
Ndugu Jorojik, Thank you very much kwa ukweli ulituwekea hapa. Ndugu Pascal anaendelea kujivunjia hadhi na heshima, japokuwa ni mwandishi mzuri na mwenye maono mazuri ya kisiasa, lakini naona amejiunga na kundi linalosemekana lina mipango ya kutuletea siasa za kiKENYA nchini kwetu.
Ndugu Pascal yumo kwenye siasa za kidini na kikabila, hili jambo limenishtusha na kunisonesha sana, i was a great follower of his writings, but now am very disappointed.
Ninamuombea mungu amrudishe kwenye fikra za kizalendo na amuepushe na ukabila na udini.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu Pascal, I truly hope unasome post zote katika uzi huu.
JEE huoni kama umetukosea sana Watanzania kwa kuutukuza ukabila na udini?
JEE huoni kama kuna wengi hapa JF walikuwa wapenzi wa michango yako mizuri na post zako nyingi zilizokuwa na mafunzo, ukweli na upendo.
I believe you need to sit down na kutafakari na ujirekebishe.
Ndugu Ukabila hauna maendeleo wala faida, nadhani hakuna anayefaidika kwa ukabila , it has never put any food in your plate nor supported your family.
Ndugu tuangalie yaliyotokea Somalia, hii ni nchi yenye watu wa Lugha Moja, dini moja tena madhehebu moja, lakini kilichoiteketeza somalia ni ukabila.
Tusisahau yaliyotokea Rwanda, Burindi, Kenya, Central Africa Republic, Myanmar na yanayo endelea leo India, bila kusahau Iraq na Syria.
Jee utafurahia hayo yakitokea Tanzania?
Sent using Jamii Forums mobile app
Karibuni na pande hii huu pia unaweza kuwa ni ukabila?.Kiukweli Pascal huwa ananisikitisha kwa posts zake za kikabila na ukanda. Sijui anajaribu kuleta ujumbe gani kwa Taifa?! Wacha tuangalie.
Mkuu Naunga mkono Hoja Pwani wapo watu Smart tu Angalia akili kubwa kama Hon.Jakaya kikwete ila pia watoto wengi wa Mjini ni wa Pwani asilia. Watu kama wasukuma au wanyakyusa wanakuja tu mjini na akili za kukariri na kuvukia barabara kidogo wachagaMkuu Pasco, usicheze na sisi watu wa Pwani. Huku Pwani ambae alikuwa na IQ ndogo ni Kawawa peke yake and probably kwa sababu ana damu ya bara (Ruvuma)!
I know you're smart enough to know kufaulu darasani; hususani kwenye elimu hii ya kukaririshana has nothing to do with IQ.
Sisi watu wa Pwani of course hatufanyi vizuri darasani ( sahau zile porojo za watu za kuhusisha madrasa. Ni Waislamu wachache sana wanaoenda madrasa na ukikutana na mtoto wa madrasa anayependa shule lazima awaburuze. Ikiwa mtu anameza Msahafu; atashindwa nini kumeza History book?) lakini sababu kubwa sio IQ but it's more historical.
Nitafafanua next time.
I.Q ya mtu huezi kupima kwa kutumia bunge la JMT na mithani ya bongo mzer. Halafu inamaana Ruvuma IQ yao Ni ndogo kuliko mikoa ya pwani, sio kweli broo km utakuwa umemuelewa Pascal mayallaMkuu Pasco, usicheze na sisi watu wa Pwani. Huku Pwani ambae alikuwa na IQ ndogo ni Kawawa peke yake and probably kwa sababu ana damu ya bara (Ruvuma)!
I know you're smart enough to know kufaulu darasani; hususani kwenye elimu hii ya kukaririshana has nothing to do with IQ.
Sisi watu wa Pwani of course hatufanyi vizuri darasani ( sahau zile porojo za watu za kuhusisha madrasa. Ni Waislamu wachache sana wanaoenda madrasa na ukikutana na mtoto wa madrasa anayependa shule lazima awaburuze. Ikiwa mtu anameza Msahafu; atashindwa nini kumeza History book?) lakini sababu kubwa sio IQ but it's more historical.
Nitafafanua next time.
Achana na sukuma/nyamwezi.Mkuu Naunga mkono Hoja Pwani wapo watu Smart tu Angalia akili kubwa kama Hon.Jakaya kikwete ila pia watoto wengi wa Mjini ni wa Pwani asilia. Watu kama wasukuma au wanyakyusa wanakuja tu mjini na akili za kukariri na kuvukia barabara kidogo wachaga
Chakula kweli kingi ila Sijui kama ni bora. Protein from 0 To 5years old mazingira yanayomsungukaSio kweli kuwa IQ ya mtu inakuwa influenced na Kabila.
" Kabila " has nothing to do with IQ.
Kuna wengine kujua tu lugha ndio kunamfanya awe wa kabila alilo nalo baas.
Ila nutrition au Diet inaweza kuinfluence IQ ya mtu hasa mtoto.
Kwa ulaya, karne nyingi za zamani ndizo zilizotoa geniuses wengi maarufu duniani na waliofanya gunduzi mbalimbali. Kama akina Michael Faraday, Albert Einstein, Aristotle, Alexander Bell, Isac Newton, Macnon na wanafalsafa mbalimbali wakubwa.
Miaka hii ambayo kwa ulaya na Amerika chakula kimeboreshwa sana kiubora hatuoni watu wenye IQ kubwa kama zamani.
Wajapan wana IQ kubwa mno na wanasema sababu ni kuwa wanakula sana raw marine organisms
Mtu mwenye IQ kubwa anaweza kuwepo katika kabila lolote lile kiasili ila anaweza asije kujulikana kwasababu ya mazingira yanayomzunguka na jamii anayoishi nayo.
Suala la Wachaga, Wahaya na Wanyakyusa kuwa wengi katika nyanja za elimu linatokana na suala la kihistoria ambalo ni
Uanzishwaji wa makanisa,hospitali, shule, na taasisi nyingi za kielimu katika ardhi yao, uliofanywa na wakoloni
Na ndio maana kuna idadi kubwa sana ya Wakristo walio wasomi kuliko Waislam tangu enzi hizo kwasababu taasisi hizo za elimu, dini na afya zilianzishwa katika mikoa yao, mfano Kilimanjaro, Mbeya, Kagera na hata Arusha pia kuna taasisi nyingi za elimu za wakoloni.
Mikoa yenye waislam wengi (kasoro wagogo tu) ndiyo uliyoiorodhesha katika list ya wenye IQ ndogo kama Mtwara, Lindi, Kondoa(kwa warangi), Wanyaturu.
Pia ingekuwa ni suala la chakula pekee iongezayo IQ basi wasukuma, wahehe na watu wa morogoro wenye vyakula haswa nao wangekuwa wengi vyuoni ila sivyo ilivyo mpaka sasa.
This case is mainly based on historical matter.
Dah....ila Kuna uhusiano mkubwa Kati ya ulaji wa ugali wa mahindi na IQ [emoji2960]
Sent using Beretta ARX 160
DuhMkanganyiko unaanzia hapo kwenye kuitafsiri IQ yenyewe. Kuna mtu ana uwezo mkubwa wa kupambanua mambo na uelewa wa hali ya juu hata kabla ya kwenda shule.
Kuna kundi la pili wamejikuta wapo kwenye mazingira ya shule inabidi wajifunze mambo kwa mfumo wa darasani.
Nnachoweza kusema, IQ mtu anszaliwa nayo, iwe ndogo au kubwa, ila mazingira, malezi ndio vinachangia kuikuza au kuididimiza.
Ni kweli wanyaturu wengi hawakwenda shule hapo awali lakini wachache walioenda wanafanya vizuri sana darasani. Hali kadhalika watu wa Zanzibar, ukimpata aliyeamua kusoma, hawakamatiki.
Naomba tuanzie kuelewa vizuri IQ kwa mapana yake.
Pascal nakubaliana na wewe kwa upande mmoja ila napingana na wewe kwa sehemu kubwa.
Hasa kwenye suala la umasikini. Kwa hapa Tanzania kuna maeneo yana umasikini wa kutisha ila ni maeneo yanayofahamika kuwa na watu wenye akili sana.
Mf. Nyasa, kwa wanyasa na Ukerewe kwa wakerewe. Haya ni maeneo ya watu wenye akili sana kwa sababu tuliosoma mashuleni na vyuoni tumekutana nao na tumewaona ila pia maeneo yao yana umasikini wa kutupwa.
Kwa mtazamo wangu, Umasikini Tanzania unatokana na Sababu Mbili kuu ambazo ni Ushirikina na Wivu wa Kijinga.
Kwa Historia maeneo mengi ya wachaga tangu miaka ya zamani hawakuwa na tabia za kishirikina hivyo kupelekea watu kupaendeleza sana kwao kwa sababu watu hawana hofu ya kupaendeleza kwao. Vilevile hawana wivu wa kijinga kwamba mtu akijenga nyumba nzuri kwao basi wanamfanyia fitna na mambo ya ajabu.
Tuseme ukweli paskali maeneo mengi ya Tanzania yapo nyuma kwa sababu ya ushirikina. Watu hawataki kupaendeleza kwao, kuendeleza maeneo yao kuogopa kurogwa au kufanyiwa mambo ya ajabu.
Kuanzia Mtwara, Lindi, Njombe Mf Ludewa hadi mkuu wa Wilaya alienda kuwatolea uvivu wananchi kwa tabia zao za kijinga za kuroga maendeleo, Dodoma,Singida, Rukwa, Katavi, Mbeya, Iringa, mikoa ya kanda ya Ziwa ni ushirikina na umefanya jamii hizi kuwa masikini na kutokuwa na maendeleo.
Kuna Taasisi moja ilifanya utafiti na ikagundua kuwa Tanzania ndo inaongoza wananchi wake kuamini kwenye ushirikina. Kwenye ushirikina watu hawana maendeleo, hawawezi kufikiri vizuri na umasikini lazima utamalaki.