Je, kuna umuhimu wa kujua mpenzi wako alishakuwa na wapenzi wangapi kabla ya ndoa?

Je, kuna umuhimu wa kujua mpenzi wako alishakuwa na wapenzi wangapi kabla ya ndoa?

Ya nn kutaka kujua bomu wakati auna uwezo wakutegua bora usijue tu kuepuka mlipuko
 
Kuuliza sio tatizo, tatizo ni kujibiwa majibu ya uongo.Bora uulize tu historia yake uijue mapema kuliko kumuona safi halafu baadae unakuja kupewa stori kamili mpenzi wako ni nani na majirani. Faida ya kuuliza kabisa akikuzingua ukimfuma tu anakosa majibu anajipa talaka yeye mwenyewe. Usipomuuliza utakuwa anakujibu kwa ujasiri huyu alitaka kunioa,alikuwa mpenz wangu, nimesoma nae nk
 
Maisha ya safari ya kimapenzi kuelekea kumtafuta yule ambaye ameujaza moyo wako....ni safari ndefu sana...na iliyojaa misuko suko mingi sana.....misuko suko ambayo wakati mwingine inakufanya ukate tamaaa.....

Kila mtu anapenda kuwa na historia safi ya mapenzi....lakini kwenye nyakati hizi ambazo uongo na unafiki vimekuwa sehemu ya maisha yetu imekuwa ni ngumu...kumpata mtu ambaye anajisikia vile ambavyo wewe unajisikia juu yake........waongo na watu wema na wanafiki wote wanaongea lugha moja na kauli tamu.....kwa hivyo kuwagundua na kuwachambua kunataka uwezo wa ziada.....

Si vyema kumhukumu mtu kwa mambo amabayo ameyafanya kipindi cha nyuma....kwani hakuna mkamilifu kati yetu wa kuweza kumnyooshe kidole mwenzio.....

Kama umempenda mtu....na yeye anakupenda kwa dhati....nguvu zenu na akili zenu....zielekezeni kwenye kulijenga penzi lenu na sio kuangalia historia za mwenzako......
a718f5d383fe0111817e3b3076b566f4.jpg
Ila kaka hakuna kitu kibaya kama kumjua alieuona undani wa mpenzi wako........ pia maneno uliyoongea ni ya kweli
 
katika maswali yanayoudhi ni hiloo hapo, na kati ya wanawake au wanaume 10 , 7 huuliza hilo swalii, nahsi anataka ajithaminishe na huyo x wako

mi huwa nikiulizwa huwa najibu " hiyo ni past tense"
 
Kati ya vitu vinavyohafifisha mapenzi ni kujua idadi halisi ya wapenzi aliowahi kuwa nao mpenzi wako, lakini pia kwa upande mwingine wa shilingi ni heri ujue maana usipokuwa makini unaweza kuishi nyumba moja na mme/mke mwenzio ukiamini kuwa ni kaka/dada/wa mke/mmeo.

Swali hapa je kipi bora kujua ama kutojua?

Karibuni wakuu
Mapenzi ni hisia!kama hisia zako zipo kwake hutojali katembea na wangapi!Halafu mapenzi hayana makombo!
 
  • Thanks
Reactions: TAB
Mapenzi ni hisia!kama hisia zako zipo kwake hutojali katembea na wangapi!Halafu mapenzi hayana makombo!
Mkuu ukifuata haya mawazo yako kuna siku unaweza kulia,asipatikane MTU wa kukufuta machoz!!!..
 
Hakuna umuhimu kabisa

Ni kujiumiza roho milele, ikitokea namba imezidi mmoja halafu ukute hao uliotajiwa unawafahamu...
 
Ni mbaya sana kujua wapenzi wa nyuma wa mpenzi wako,ni sawa na kugundua umeathirika kwa HIV,unafahamu tatizo halafu huna uwezo wa kuliondoa! kila ukikutana na washkaji zake wa zamani unahisi jana walikula kitu,msongo wa mawazo unaanzia hapo na kuendelea mpaka miaka ya hamsini mwishoni.
 
Back
Top Bottom