Je, kuna ushahidi Hayati Magufuli alimuua nani, aliiba nini na alimpora nani hela?

Usilolijuwa ni usiku wa kiza.

Kutesa kwa zamu.

Makonda yuko wapi?
 
Wale wote wanamsingizia hizo tuhuma wana upungufu wa akili au wana mtindio wa ubongo, yaani ni machizi au ni watu waliochanganyikiwa wenye laana, yaani ni lile kundi la watu wasio kuwa na material ya kawaida kwenye ubongo yaani kichwani hawana kabisa ubongo wa akili mradi mwili wanao tu na tundu la mdomo la kuropokea
 
Hivi aliyekuwa Waziri wa Fedha si yupo kwa nini isifunguliwe kesi mahakamani ili tusikie ushahidi kamilifu sio hizi ngonjera za kwenye kijiwe cha kahawa.
Hilo halitatokea. Ila kwa Tsh 1.5 Trillion ni dhahiri zililiwa na ndiyo sababu Serikali kilishindwa kuzi account na kutoa maelezo ya uongo eti Billion 250 zilipelekwa Zanzibar huku wakijua kabisa siyo kweli.
 
Kwenye masuala ya pesa za serikali, aA
aliyekuwa waziri wa fedha yupo aulizwe. Lazima mjue aliyekufa ni mmoja tu. Serikali nzima ipo
 
Na points zako umezisahau?
 
Mimi ninunuliwe bando? Nadhani huelewi unachosema, anyway bundle kuwa Yako au Ya Sukuma gang haimaanishi kuwa ni sahihi kuwaita wengine mashoga
 
Kuna level ya threat ukifikia wenyewe wanarecomend termination.

Wakikupenda sana watakuonya na ukikaidi utakutana nao hao wenye nchi yao halisi.
 
Unamuambia nani?
 
Hivi siku ile pale Chato, si mlisema mmempumzisha kwa amani au hastahili kupumzika huko alikokwenda na hata duniani pia. Nyie ndio mnaosababisha marehemu atukanwe kila siku humu.
 
Tutafika taratibu tu!!
 

Attachments

  • Screenshot_20230320-065508.png
    318.6 KB · Views: 3
Hizo ni propaganda tu Boss. Ili watu Fulani Fulani waonekane ni Malaika.

Hata Id Amin aliitwa joka kumbe Hata hakuwa joka
 
Sukuma gang mnalia lia nini? Asiyekuwepo na lake halipo.

Ndugai yuko wapi?
 
Kwenye masuala ya pesa za serikali, aA
aliyekuwa waziri wa fedha yupo aulizwe. Lazima mjue aliyekufa ni mmoja tu. Serikali nzima ipo
Jiwe alikuwa dikteta aliendesha nchi kwa amri zake utadhani familia yake. Ndiyo maana mama anapindua kila baya alillokuwa anafanya ibilisi yule
 

Mimi na ushuhuda jinsi Magufuli alivyonifanyia. Kabadilisha lifestyle ya Maisha kisa siasa. Mpumbavu Sana yule ibilisi. Unakubali kudestroy Maisha ya watu kwa sababu hawakuungi mkono?. Ngoja nisiongee mengi, ila siku anakufa nilishukuru Sana na kufurahia maana machungu yangu yamelipwa.
 
Kristo alitukanwa, alikashifiwa, alidhalilishwa (fikiria mpaka kuvuliwa nguo), alitemewa mate, na mwishowe aliuawa,lakini ndiye mkombozi wetu,Naamini Rais Magufuli alikufa akiwa na hakika anakwenda na Bwana Yesu,maana aliimba nyimbo kabla ya kifo chake,,aliwaita Mkuu wa Wakatoliki Kadrinali Pengo,na Mkuu wa Waislam,Mufti alikaa nao kwa ajili ya utakaso wa kiroho,hii ni neema wanaipata wachache na ukiipata basi jua kwamba Mungu alikufanya kuwa mwana na alishakuhesabia haki,hivyo basi atahahakikisha unatakasika kabla ya kwenda kwake.
 
Hivi aliyekuwa Waziri wa Fedha si yupo kwa nini isifunguliwe kesi mahakamani ili tusikie ushahidi kamilifu sio hizi ngonjera za kwenye kijiwe cha kahawa.
Jiwe hakuwa na serikali; mawaziri wake walikuwa kama wafanyakazi wa nyumbani kwake: shamba boys/house girls! Hawakuhusishwa kwenye maamuzi makubwa na ndiyo maana nao walikuwa wanamzungumzia mtu mmoja tu badala ya serikali. Alikuwa na kitchen cabinet ya vijana wake wanaofahamika kwa vitimbi na kufuru nyingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…