mimi binafsi bado ninaona tunao uwezo wa kupata njia nzuri zaidi ya kudeal na huu ugonjwa.
bado ninabaki na msimamo kuwa partial lockdown, isolation of the sick ones na followup kwa contact person wa victims ni suluhisho. huku tukiendelea kupractice safe practices kama kunawa mikono na kuvaa barakoa kila mara.
Kuna makosa mengi kwenye dhana yako, hata tarakimu ulizoweka kueleza 'model' kwa Tanzania hazikubali; aaah, lakini hii ni JF kila kitu kiakwenda.
Kwa mfano, utaweka 'partial lockdown' sehemu yoyote ya Tanzania kwa manufaa gani?
Kwa nini uongeze gharama za kuwatafuta watu (contacts), wakati huu, maelfu kwa maelfu kama sio mamilioni kwa mamilioni!
Hizo gharama zinahitajika sana kununua barakoa, kuhakikisha 'social distancing' inatumika vipasavyo na hata kuweka maji , sabuni, sanitizers kila sehemu.
Kueleimisha wananchi kuachana kabisa na mikusanyiko ya aina yoyote, kama kwenda makanisani/misikitini, n.k.
Hivi nikuulize. hiyo dhana (theory) ya 'herd immunity' ulishasikia ikitumika nchi gani popote duniani?
Hivi juzi tu hukusikia habari WHO wakisema kuna uwezekano wa ugonjwa huu wa COVIT - 19 kujirudia kwa mgonjwa yule yule alisha uugua hapo mwanzo?
Haya 'herd immunity' na malaria yetu ipoje mkuu gfsonwin'?
Mambo mengine tuwe tunajingeza kidogo kabla ya kuyafikiria. Huu ni ugonjwa mpya, hakuna anayejua mwelekeo wake, pamoja na kwamba ni 'virus'; lakini hatujui huyu kirusi yupoje!
Sasa tunatafuta njia za kuhalalisha vitu hata visivyoeleweka ili serikali ionekane inafanya kitu?
Silengi kukulalamikia wewe juu ya hili, lakini kwa ujinga walionao wahusika watalilrukia na kulifanya kuwa sababu/kisingizio cha kutowajibika ipasavyo kulinda maisha ya waTanzania.