Je, kuwa na gari ni kivutio kwa wadada katika mahusiano?

Je, kuwa na gari ni kivutio kwa wadada katika mahusiano?

Sijui kwa wengine hili limekaaje ila binafsi naona gari nalo ni kivutio kwa hawa dada zetu, Kuna binti hapa mtaani enzi hizo sina gari aliniwekea ngumu ila mwaka jana nilivyomiliki gari yani alilegeza hata sikuamini,

I mean kuna siku kuna bidada anajiheshimu sana tu nlimpa lifti tukabadilishana contacts kesho yake kiutani nikamwambia tumeet akakubali fasta yani nikawa nacheka tu maana ilikuwa natania,

Kuna matukio mengi sana ambayo yalinithibitishia kuwa hawa dada zetu wana kaugonjwa kwa wanaume wenye magari, Japo haya matukio huwa yananitokea mimi najiheshimu na nampenda sana mpenzi wangu sipo tayari kutake advantage kwa hawa mabinti wa lifti,

So mimi ninachokiona kuna uwezekano mkubwa kwamba ukiwa na Gari wanawake utakuwa kivutio kwao....Ni fikra tu
Sawa tumeshajua km una gari
 
Rubbish. Gari ndo inaendesha ndoa ? Labda uniambie gari kwa ajil ya kufanyia biashara kama teksi, kubebea mizigo na business za aina hio
Lakin gar ya starehe ama ya kutembelea?
Kama mtu amekupenda kwa ajil una gari huyo hakupendi ni ujinga ...ujinga kabisa...
Fake love ...kama mdada unataka gari nunua ya kwako jivutie wewe mwenyewe na hilo gari likuoe kabisa
Wanazungumzia wale wa starehe tu si wajua wengi hawana ndoa na hawependi mapenzi ya kudum
 
Mkuu ushamba wa gari bongo bado sana kuisha, ushamba wa tv ndio umefanikiwa kuisha, ukiwa na gari hata la mkopo unaonekana una hela kuliko mtu mwenye hela halafu hana gari. Ukiwa na hela halafu unasugua bomba kwenye daladala unaonekana ndo 'walewale'. Kama unahela nunua gari uheshimiwe
Ni kweli screpa.Tuna safari ndefu sana.GARI ni LIABILITY(kama deni vile).Nyumba ni bonge la asset(Kitega uchumi?).Lakini wadau wanasema nyumba huwezi kwenda nayo bar,nyumba haipigi honi nk Wanataka kitu ambacho watakuona nacho mtaani.Kwa vijana mnaochipukia milikini nyumba kwanza badala ya magari
 
Back
Top Bottom