Je Kwanini USA wameruhusu Ukraine kupiga ndani ya Urusi?

Umewakilisha mawazo yako umeandika riwaya nzuri utapokuwa unarudia kuisoma iwe ina kufurahisha ila hujafanya tathimini ya vita na kama utashupaza shingo na kutoa macho kwa kusema umefanya basi itakuwa kishabiki sana ila wacha kupiga mayowe ulaya hawalali kwa kuogopa putin israel halali kwa kuihofia iran,israel ni dhaifu mwaka sasa wameshindwa kuimaliza palestina kujiingiza lebanon ni sawa wamepiga tiktaka na msuli bila kuvaa boxer korodani zote nje subiri ushuhudie uchizi wa putin na Ayatollah khamein utajua kama hujui!
 
Unapiga story badala ya kufanya analysis. Na huenda mengi yamekuoita bila taarifa.

Mpango wa Urusi, ilipoanzisha mashambulizi dhidi ya Ukraine, ilikuwa Serikali ya Ukraine iwe imeangushwa ndani ya siku 2, na wapinzani wa Serikali ya Ukraine wanaosaidiwa na Urusi ndiyo waongoze Serikali; na ilikuwa Rais wa Ukraine pamoja na maafisa wa juu kadhaa wa Serikali yake wauawe. Ili kutekeleza mission hiyo, Urusi ilipeleka askari wake maalum, wenye ujuzi wa hali ya juu kabisa, lakini wengi wao waliishia kuuawa, na waliosalia wakakimbilia mashariki mwa Ukraine waliko wapinzani wa Serikali. Kwa ujumla operation ya Putin ilishindwa vibaya, badala ya kumwua Zeleniskyy, walikufa maafisa wengi wenye ujuzi mkubwa wa kivita wa Urusi. Wakaamua kukimbia.

Kwa ujumla kwenye vita hivi Urusi imeshindwa vibaya, ndiyo maana imebakia kitishia kuwa itatumia silaha za nyuklia. Fikiria ulipanga umalize jambo ndani ya siku 2 halafu unaenda kwa karibia miaka mitatu, hukafanikisha ulichokuwa umekipanga!!

Russia ni dhahiri ina intelijensia duni sana. Ina maana haikujua uwezo wa Ukraine wala uwezo wa jeshi la Russia vs Ukraine. Ukraine ilikikimbiza kikosi cha makomandoo cha Urusi toka Kiev, wengine miili yao ikitapakaa mabarabrani, tena wakati huo wakiwa hawajapewa msaada wowote wa silaha kutoka nchi za magharibi!!

Urusi ina wanajeshi karibia mara 10 ya Ukraine, ina utajiri karibia mara 10 ya uchumi wa Ukraine. Ukraine ni Taifa changa kuliko hata Tanzania. Ukraine ni ndogo zaidi ya mara 10 ya Urusi, lakini imeisimamisha Urusi isifanye ilichokitaka. Mpaka hapo, ni mafanikio makubwa kwa Ukraine, na anguko kubwa kwa Russia.
 
 
Putin ameshashinda hiyo vita. !
Biden anataka kumwangushia gari bovu Trump kwa kuruhusu makombora ya USA yapige ndani ya Urusi !

Wajaribu waone mziki wa Russia !
World war 3 is imminent !
Kwani hiyo ni mara ya kwanza kwa Ukraine kupiga ndani ya Russia?
Mbona walishapiga hadi wakateka na kushikiĺia maeneo?
 
Nakukubaliana na wewe huwezi kwenda frontline bila intelligence information,
Ila analysis yako naomba niseme haiko sawa
Sehemu kubwa ya frontline ya Umraine ipo weak na near to collapse
Ukraine wana shortage ya manpower hasa wenye wazoefu
Kursk kuna askari wa Ukraine na Nato (Mercenaries) ambao wako trapped , maana hawaendi mbele wala hawawezi kurudi nyuma na wanazidi kufa kwenye counter offensive ya Russia, na logistic zote zimekatwa ya ku supply back au kufanya evacuation
Usisahau nyingi za Ulaya ziko kwenye hali mbaya kiuchumi, na ndio maana misaada inazidi kupungua kila siku na wanaanza kutofautiana, inamaana U.S, U.K, France na Poland (ling leader) wanatafuta namna ya kutoka kwenye hili saga bila aibu.
Na ndio maana zile missile ya jana ni kama test kuona Russian response,
ku demoralise na hofu kwa askari wa Urusi
Kushambulia ghala za silaha hasa zinazotumika ku support Kursk operation ili kuweza kuwaokoa askari wa Ukraine na NATO waliopo kursk na Russia asiwe na uwezo wa kuwashambulia.
kuzuia mashambulizi ya mji wa sumy ambao ni kama buffer zone kwa mji mkuu wa kieve
Nadhani huu ni mtego na Urusi nahisi hatajibu kitu zaidi ya kuzidisha mashambulizi front hasa chasiv yar na prokrovsk
All in all hakuna vita ya tatu ya dunia
 
Mkuu acha uongo nipe link Moja TU wachambuzi wabobezi wanaubeza jeshi la Russia.

Hebu tafuta clip ya secretary general wa NATO aliyestaafu October usikie anasema Nini kuhusu jeshi la Urusi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…