Scars
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 48,055
- 116,512
Makala hii nitaiweka kwa vipande kuepusha kero ya usomaji.
Moja ya hoja maarufu kutoka kwa watu wanaoamini Mungu (Theists).
Ni hoja ambayo imelenga kuweka matumaini ya mwelekeo katika maisha ili kuwafanya watu waone kuamini Mungu yupo ndio uchaguzi bora zaidi (rational) kwasababu haitakupa matokeo mabaya mwishoni.
Hii ni Analogy iliyopata sana umaarufu miaka ya 1640s na muazilishi aitwaye Pascal Wager.
Huyu jamaa alihoji kuwa ni vyema ukaamini kuwa Mungu yupo ukafa na usimkute kuliko kutokuamini halafu ukafa ukamkuta.
Pascal analaani kuwa kuamini kuwepo kwa Mungu ni tendo la busara zaidi kuliko kutokuamini kuwepo kwake, hata kama hatuna uhakika kuhusu kuwepo kwake. Hii ni kwasababu zifuatazo.
Hivyo, Pascal anasema kwamba kuamini kuwepo kwa Mungu ni tendo la busara zaidi, kwasababu unaweza kupata thawabu ya milele na kuepuka adhabu ya milele, hata kama hatuna uhakika kuhusu kuwepo kwake.
Swali: Je Atheists hawatuogopi siku ya mwisho kukutana na hukumu ya Mungu na kutupwa kwenye moto wa milele?
Hatuogopi kubaini kuwa hadithi za mitume zinazosimuliwa kuhusu Yesu na Muhammad kuwa ni za kweli na kwamba tumepoteza nafasi ya kuishi maisha ya milele peponi kwa kutoamini?
Je isingekuwa vyema Atheists kuwa upande salama wa kumuamini Yesu, Muhammad na Mungu kama backup just in case?

- Kama Mungu yupo na tutamwabudu, tutapata thawabu ya milele (kama ushindi mkubwa).
- Lakini kama Mungu hayupo na hatumwamini, hatutapata chochote (kama hasara ndogo).
- Kwa upande mwingine, kama Mungu yupo na hatumwamini, tutapata adhabu ya milele (hasara kubwa).
- Lakini kama Mungu hayupo na hatumwamini, hatutapata chochote (ushindi mdogo).