Je, kweli ni bora kuamini Mungu yupo halafu siku ya mwisho usimkute, kuliko kutoamini halafu ukamkuta?

Je, kweli ni bora kuamini Mungu yupo halafu siku ya mwisho usimkute, kuliko kutoamini halafu ukamkuta?

...Hata wapumbavu huzeeka , usitegemee hekima kuikuta humo . Ndo wewe sasa umri mkubwa lakini unajizima Wi-Fi.

Kuhusu uwepo wa Mungu , Ni sawa na kumwaminisha mtu duni Sana anayeishi kijijini ndani ndani Huko kwamba Kuna watu hapa nchini Ni matajiri wakutupwa.

Kutokana na fikra zake na mazingira magumu ya kijijini ataamini Ni story tu za kusadikika , lakini haimanishi Hakuna matajiri , isipokuwa Ni yeye hawajui au hajashuhudia.

Ndo kwako wewe , miaka yote umekuwa namba moja kukosoa kumuhusu Mungu lakini kwa bahati nzuri Mungu anawapenda hata wamchukiao Kama wewe.

Uamini au usiamini haifanyi Mungu kutokuwepo. Mpumbavu husema moyoni mwake Hakuna MUNGU.
How old am I?
 
Kama yupo kila sehemu kwa nini anaachia watoto wa kule Gaza wauliwe na wengine kupewa vilema vya maisha?
Ana nguvu ya kumaliza vita ikiwa pamoja na kuwaokoa watoto wasife huko gaza
1734364188556.jpeg

Lakini badala yake anakuangalia unavyopiga puli

1734364125559.jpeg
 
Kwa andiko hili inamaana itakuwa sawa kama kila mtu atabaki kwenye anachokiamini.
Kusudio la andiko kwanza ni kuweka bayana utata wa kuchagua kuamini au kutokuamini sio uchaguzi wa mmoja kati ya mmoja.

Bali ni mmoja kati ya mamilioni.

Ulimwenguni kuna zaidi ya dini 5,000 ambazo zipo active zenye kuabudu maelfu ya Miungu tofauti tofauti. Ni yupi kati yao ambaye tunashauriwa kumuamini au kutokumuamini?

Uchaguzi ambao umepewa kati ya kuamini Mungu au kutokumuamini sio wa mmoja kati ya mmoja, ni mmoja kati ya mamilioni.

Kitu ambacho hata kwenye betting ni nadra sana kuweze kufanya uchaguzi sahihi.

Kuna mwamba anaitwa David Mitchell alishawahi kui-flip hiyo hoja ya Pascal Wager akauliza vipi kama peponi ni sehemu ambayo wanaruhusiwa kuingia atheists peke yao?

Hivi ndivyo itakavyokua

1. Kama hakuna Mungu, basi kutomuamini hakutaweza kukudhuru
2. Kama Mungu yupo, kutokumuamini kutakupa faida wewe kama atheist uweze kuingia peponi

Kwa hiyo ukitumia logic hiyo hiyo utajua tena kumbe haupaswi kuamini Mungu ili uingie peponi.
 
Aiseee!!

Kwanza natamani nikutane na huyo Mungu tufanye mjadala mkali.

Maana nina maswali mengi sana ya kumhoji na kujua uwezo wake wa kufikiri kama uko sawasawa kweli?

Na kama kweli yupo nitahitaji anipe majibu ya kueleweka.

Maana haiwezekani aumbe viumbe vije viteseke duniani, Halafu yeye anakula bata huko mbinguni halafu akiombwa aje atoe msaada japo kidogo hapa duniani haonekani kwenye jambo lolote kusaidia.

Watu wanazidi kuteseka na kuumia tu.

Sasa kama kweli Mungu yupo, Alituumba kwa nini?

Aje atutese duniani, Halafu baadae ndio tuje kui enjoy mbinguni!!!

Hivi hii ni akili ya namna gani kama sio makusudi haya?

Yani unaumba kiumbe ukitese kwanza, Halafu baadae ndio uje ukipe raha!!

Hivi hii ni akili au matope
Yani kama huyo Mungu yupo,

Anastahili kufurushwa kabisa maana hajielewi kabisa.
Mimi nafanya kazi, natafuta pesa, Nailisha familia yangu, sijaitelekeza japo sina nguvu kama zake.

Ajabu yeye mwenye nguvu kushinda mimi eti amekimbia majukumu, Ametelekeza watoto wake mwenyewe.
 
Ana nguvu ya kumaliza vita ikiwa pamoja na kuwaokoa watoto wasife huko gaza
View attachment 3178143
Lakini badala yake anakuangia unavyopiga puli

View attachment 3178141
Maelfu ya watoto wadogo wasio na hatia yeyote ile wamekufa sana huko Gaza na huyo Mungu anayedaiwa yupo anatuangalia muda wote na anatupenda, Hajafanya chochote kile kusaidia!!👇
JamiiForums1832832046.jpeg
 
Makala hii nitaiweka kwa vipande kuepusha kero ya usomaji.

Moja ya hoja maarufu kutoka kwa watu wanaoamini Mungu (Theists).

Ni hoja ambayo imelenga kuweka matumaini ya mwelekeo katika maisha ili kuwafanya watu waone kuamini Mungu yupo ndio uchaguzi bora zaidi (rational) kwasababu haitakupa matokeo mabaya mwishoni.

Hii ni Analogy iliyopata sana umaarufu miaka ya 1640s na muazilishi aitwaye Pascal Wager.

Huyu jamaa alihoji kuwa ni vyema ukaamini kuwa Mungu yupo ukafa na usimkute kuliko kutokuamini halafu ukafa ukamkuta.

Pascal analaani kuwa kuamini kuwepo kwa Mungu ni tendo la busara zaidi kuliko kutokuamini kuwepo kwake, hata kama hatuna uhakika kuhusu kuwepo kwake. Hii ni kwasababu zifuatazo.

  1. Kama Mungu yupo na tutamwabudu, tutapata thawabu ya milele (kama ushindi mkubwa).
  2. Lakini kama Mungu hayupo na hatumwamini, hatutapata chochote (kama hasara ndogo).
  3. Kwa upande mwingine, kama Mungu yupo na hatumwamini, tutapata adhabu ya milele (hasara kubwa).
  4. Lakini kama Mungu hayupo na hatumwamini, hatutapata chochote (ushindi mdogo).

Hivyo, Pascal anasema kwamba kuamini kuwepo kwa Mungu ni tendo la busara zaidi, kwasababu unaweza kupata thawabu ya milele na kuepuka adhabu ya milele, hata kama hatuna uhakika kuhusu kuwepo kwake.

Swali: Je Atheists hawatuogopi siku ya mwisho kukutana na hukumu ya Mungu na kutupwa kwenye moto wa milele?

Hatuogopi kubaini kuwa hadithi za mitume zinazosimuliwa kuhusu Yesu na Muhammad kuwa ni za kweli na kwamba tumepoteza nafasi ya kuishi maisha ya milele peponi kwa kutoamini?

Je isingekuwa vyema Atheists kuwa upande salama wa kumuamini Yesu, Muhammad na Mungu kama backup just in case?
Vipi wewe usiyeamini Buddhism? Hauogopi yatakayokukuta ukifa kwa kutoifuata imani hiyo? Kwa hivyo inakupaswa kuzifuata imani zote ili kuepuka what you call 'adhabu ya milele'?
 
Haya maneno ya Marcus Aurelius ni mazuri sana;

"Live a good life. If there are gods and they are just, then they will not care how devout you have been, but will welcome you based on the virtues you have lived by. If there are gods, but unjust, then you should not want to worship them. If there are no gods, then you will be gone, but will have lived a noble life that will live on in the memories of your loved ones.”
Umenikumbusha Euthyphro Dilemma

"The pious is loved by God because it's pious or The pious is pious only because it is loved by the gods?"

Mcha Mungu ungu anapendwa na Mungu kwasababu ni mcha Mungu, au mcha Mungu kawa mcha Mungu kwasababu tu Mungu kampenda?

Kama mcha Mungu anapendwa na Mungu kwasababu ni mcha Mungu, basi hoja ya kwamba Mungu anapenda watu fulani haiwezi kuelezea kwanini watu hao ni wacha Mungu.

Au kwa mtindo mwingine.

1. Mema ni mema kwasababu Mungu amesema ni mema?

2. Au ni mema na ndio maana Mungu amesema ni mema?

Kama kusema kwa Mungu kuwa mema ni mema kutafanya yawe mema basi ni wazi kuwa mema sio sababu pekee ya kuyafanya yawe mema.

Na kama yalikuwa mema na ndio maana Mungu akasema ni mema basi kumbe mema kuwa mema haiwezi kutokana na Mungu kuyasema ni mema kwasababu kuna viwango vya kupima wema vinavyojitegemea bila kuhusisha Mungu.
 
...Hata wapumbavu huzeeka , usitegemee hekima kuikuta humo . Ndo wewe sasa umri mkubwa lakini unajizima Wi-Fi.

Kuhusu uwepo wa Mungu , Ni sawa na kumwaminisha mtu duni Sana anayeishi kijijini ndani ndani Huko kwamba Kuna watu hapa nchini Ni matajiri wakutupwa.

Kutokana na fikra zake na mazingira magumu ya kijijini ataamini Ni story tu za kusadikika , lakini haimanishi Hakuna matajiri , isipokuwa Ni yeye hawajui au hajashuhudia.

Ndo kwako wewe , miaka yote umekuwa namba moja kukosoa kumuhusu Mungu lakini kwa bahati nzuri Mungu anawapenda hata wamchukiao Kama wewe.

Uamini au usiamini haifanyi Mungu kutokuwepo. Mpumbavu husema moyoni mwake Hakuna MUNGU.
Kwamba wewe mtoto wa mjini kwa elimu yako uliyonayo ni kweli utashindwa kuwathibitishia hao masikini kuwa huko town kuna matajiri na wakakuelewa?

Huoni kuwa wewe utayeshindwa kutumia resources za elimu yao kuweza kuwafanya hao watu wakuelewe kutokuwa na guts za kuwaita hao ni duni kwasababu elimu yako na ujuzi wako ni useless?
 
Kwa nini uhitaji kuamini Mungu yupo Badala ya kujua yupo?

Huyo Mungu kama yupo kwa nini anataka aaminiwe yupo, Badala ya kujulikana yupo kwa uhakika na uthibitisho?

Kama huyo Mungu yupo kwa nini anajificha ili aaminike yupo?

Kwa nini asijitokeze hadharani akajulikana yupo na kila mtu akajua yupo kwa uhakika kabisa, Bila utata na utofauti wa kiimani?

Huyo Mungu kama yupo anastahili bakora kabisa maana inaonekana hajielewi kabisa.

Yani anajificha halafu anataka sisi tuhangaike kumwamini na kumtafuta!!

Kwani sisi binadamu tukisha mwamini huyo Mungu, Yeye anafaidika nini?

Kama huyo Mungu yupo na alitaka aaminiwe yupo, Alishindwaje kuumba binadamu wenye imani ya kumwamini yupo siku zote?

Kama Mungu yupo na alitaka aaminiwe yupo na kila mtu, Na ni Mungu mwenye kujua yote tangu mwanzo na hata milele, Je HAKUJUA kwamba kuna watu watakuja kutokumwamini, Awadhibiti na kuwa angamiza mapema?
Na kwanini kwake iwe muhimu sana kuabudiwa wakati yeye amejitosheleza?
 
Back
Top Bottom