Je, kweli ni bora kuamini Mungu yupo halafu siku ya mwisho usimkute, kuliko kutoamini halafu ukamkuta?

How old am I?
 
Kwa andiko hili inamaana itakuwa sawa kama kila mtu atabaki kwenye anachokiamini.
Kusudio la andiko kwanza ni kuweka bayana utata wa kuchagua kuamini au kutokuamini sio uchaguzi wa mmoja kati ya mmoja.

Bali ni mmoja kati ya mamilioni.

Ulimwenguni kuna zaidi ya dini 5,000 ambazo zipo active zenye kuabudu maelfu ya Miungu tofauti tofauti. Ni yupi kati yao ambaye tunashauriwa kumuamini au kutokumuamini?

Uchaguzi ambao umepewa kati ya kuamini Mungu au kutokumuamini sio wa mmoja kati ya mmoja, ni mmoja kati ya mamilioni.

Kitu ambacho hata kwenye betting ni nadra sana kuweze kufanya uchaguzi sahihi.

Kuna mwamba anaitwa David Mitchell alishawahi kui-flip hiyo hoja ya Pascal Wager akauliza vipi kama peponi ni sehemu ambayo wanaruhusiwa kuingia atheists peke yao?

Hivi ndivyo itakavyokua

1. Kama hakuna Mungu, basi kutomuamini hakutaweza kukudhuru
2. Kama Mungu yupo, kutokumuamini kutakupa faida wewe kama atheist uweze kuingia peponi

Kwa hiyo ukitumia logic hiyo hiyo utajua tena kumbe haupaswi kuamini Mungu ili uingie peponi.
 
Mimi nafanya kazi, natafuta pesa, Nailisha familia yangu, sijaitelekeza japo sina nguvu kama zake.

Ajabu yeye mwenye nguvu kushinda mimi eti amekimbia majukumu, Ametelekeza watoto wake mwenyewe.
 
Ana nguvu ya kumaliza vita ikiwa pamoja na kuwaokoa watoto wasife huko gaza
View attachment 3178143
Lakini badala yake anakuangia unavyopiga puli

View attachment 3178141
Maelfu ya watoto wadogo wasio na hatia yeyote ile wamekufa sana huko Gaza na huyo Mungu anayedaiwa yupo anatuangalia muda wote na anatupenda, Hajafanya chochote kile kusaidia!!👇
 
Vipi wewe usiyeamini Buddhism? Hauogopi yatakayokukuta ukifa kwa kutoifuata imani hiyo? Kwa hivyo inakupaswa kuzifuata imani zote ili kuepuka what you call 'adhabu ya milele'?
 
Umenikumbusha Euthyphro Dilemma

"The pious is loved by God because it's pious or The pious is pious only because it is loved by the gods?"

Mcha Mungu ungu anapendwa na Mungu kwasababu ni mcha Mungu, au mcha Mungu kawa mcha Mungu kwasababu tu Mungu kampenda?

Kama mcha Mungu anapendwa na Mungu kwasababu ni mcha Mungu, basi hoja ya kwamba Mungu anapenda watu fulani haiwezi kuelezea kwanini watu hao ni wacha Mungu.

Au kwa mtindo mwingine.

1. Mema ni mema kwasababu Mungu amesema ni mema?

2. Au ni mema na ndio maana Mungu amesema ni mema?

Kama kusema kwa Mungu kuwa mema ni mema kutafanya yawe mema basi ni wazi kuwa mema sio sababu pekee ya kuyafanya yawe mema.

Na kama yalikuwa mema na ndio maana Mungu akasema ni mema basi kumbe mema kuwa mema haiwezi kutokana na Mungu kuyasema ni mema kwasababu kuna viwango vya kupima wema vinavyojitegemea bila kuhusisha Mungu.
 
Kwamba wewe mtoto wa mjini kwa elimu yako uliyonayo ni kweli utashindwa kuwathibitishia hao masikini kuwa huko town kuna matajiri na wakakuelewa?

Huoni kuwa wewe utayeshindwa kutumia resources za elimu yao kuweza kuwafanya hao watu wakuelewe kutokuwa na guts za kuwaita hao ni duni kwasababu elimu yako na ujuzi wako ni useless?
 
Na kwanini kwake iwe muhimu sana kuabudiwa wakati yeye amejitosheleza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…