Je, kweli ni ngumu kuishi na mwanaume aliyewahi kuoa?

Je, kweli ni ngumu kuishi na mwanaume aliyewahi kuoa?

Aaliyyah

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2022
Posts
19,041
Reaction score
46,239
Natumaini mkopoa?

Katika piatapita zangu nikakutana na mada Kwamba mwanamke kama hujawahi kuolewa bas usikubali kuolewa na mtu ambae alishawahi kuoa ama Kuishi na mwanamke Yani hata wale waliowahi Kuishi pamoja bila ndoa

Rafikiyangu ameolewa na mwanaume wa aina hiyo ambae alishakuwa na mke na ana watoto before hajamuoa

Katika mazungumzo yetu mara nyingi Huwa anasema ni ngumu Kuishi na mwanaume aliewahi kuoa ikiwa mwanamke pia hukuwah kuolewa

Mara ya pili akarudia neno hilo Hilo
Sikutaka kuhoji sana sababu nilishasikia mahali nimeona niliweke hapa Kwa wataalamu na watu wenye uzoefu

Je ni kweli Kuishi na mwanaume aliewahi kuoa au Kuishi na mwanamke ni changamoto?
Huwa wapoje Hawa watu ambao ndoa zao za mwanzo zimevunjika
 
Natumaini mkopoa?
Katika piatapita zangu nikakutana na mada Kwamba mwanamke kama hujawahi kuolewa bas usikubali kuolewa na mtu ambae alishawahi kuoa ama Kuishi na mwanamke Yani hata wale waliowahi Kuishi pamoja bila ndoa

Rafikiyangu ameolewa na mwanaume wa aina hiyo ambae alishakuwa na mume na ana watoto before hajamuoa

Katika mazungumzo yetu mara nyingi Huwa anasema ni ngumu Kuishi na mwanaume aliewahi kuoa ikiwa mwanamke pia hukuwah kuolewa

Mara ya pili akarudia neno hilo Hilo
Sikutaka kuhoji sana sababu nilishasikia mahali nimeona niliweke hapa Kwa wataalamu na watu wenye uzoefu

Je ni kweli Kuishi na mwanaume aliewahi kuoa au Kuishi na mwanamke ni changamoto?
Huwa wapoje Hawa watu ambao ndoa zao za mwanzo zimevunjika
Rafikiyangu ameolewa na mwanaume wa aina hiyo ambae alishakuwa na mume na ana watoto before hajamuoa
 
Inategemea alitokaje huko, anaweza chukua mda sana kukuamini, ili ukikaa naye kwa uvumilivu na upendo wa kweli, baadae atakutendea mema sana!

Mtu ambaye katoka huko kapatiwa matatizo anakujia akiwa makini, lakini mwanamke akitulia na kumwomyesha tumaini, anatulia haswa!

Shida ni: Kweli utaweza mngoja apone? Maana Amekaa mguu sawa kwa umakini asiingie kwenye mazingira aliyotoka!

Ila ni muhimu sana kujua:

1. Katokaje huko.
2. Je ni mke wa ngapi?
3. Lazima awe financial stable ( watoto)
4. Lazima aweke Msingi mzuri!
 
Asante kuniita Aaliyyah, nadhani hili linajibiwa vizuri na wanawake..wale waliopitia huu uzoefu.

Ila naweza kusema tu huenda hao wanaume wanakuwa na ile tabia ya kulinganisha, kwamba wewe sio bora kama ex wife, una madhaifu mengi ni bora yule wa kwanza, labda uchafu, huwezi kupika vizuri, hunipi kipapa vile nataka, una mdomo nk. Huwa kuna tabia ya kulinganisha...ni mawazo tu, sina uzoefu!
 
Dunia imebadilika, options zimekuwa nyingi, hata kwa hao ambao hawajawahi kuishi na wenza hapo awali, ndoa zao sio stable namna hiyo. Sikuhizi kwenye ndoa kila mtu anaingia akiwa na option B mfukoni. Inabidi mkubaliane na mabadiliko haya, ndoa za sikuhizi sio ndoa tulizokuwa tunaziona miaka ya 2005 kurudi nyuma
 
Kha! Hatari so in short ni kwamba mwanahme anakiwa anakumbuka mapenzi ya former wife🤣🤣🤣
Isije ikawa ata wakati wa kumgegeda current wife anavuta picha ya mbusush ya mke wa zamani 🤣🤣🤣🤣
Waoaji na waolewaje kazi tunayo
 
Back
Top Bottom